Waziri wa Utumushi, Mchengerwa: Maafisa utumishi wasiopandisha madaraja kutumbuliwa

Mimi nilikuwa kwenye bajeti ya 2018/2019 na mwaka jana nimekuja masomoni tangu 2020 nasubiri afisa utumishi aniteme niende Dodoma,
 
Mimi nilikuwa kwenye bajeti ya 2018/2019 na mwaka jana nimekuja masomoni tangu 2020 nasubiri afisa utumishi aniteme niende Dodoma,
Hapo sasa patamu. Kuna jamaa yangu ajira 2013 alienda masomoni mwaka 2017 lakini wenzake wakapanda 2019. Yeye hakupanda kwa kuwa yuko masomoni. Sasa amemaliza degree 2020 na HESLB wanamlima makato ya 15% kwa TGTS B yake. Huenda hayumo kwenye mpango wa wanaopanda
 
Well done Mchengerwa, upele umepata mkunaji, kuna baadhi ya taasisi za serikali zimejaa upumbavu ambao ni aibu kuandika humu. Ikibidi tutaandika
 
Vipi kuhusu maafisa utumishi ambao huwa wanafanya mbinu za kushusha watu vyeo kisisriri, au wale ambao huwa wanapandisha watumishi madaraja halafu wanaanza kuwalipa mshahara wa daraja lililo nyuma yake? Mh Waziri inabidi awaangalie na hao pia, nao wapo. Vile vile inabidi awe mwangalifu na punguzo la kodi ya mshahara la mwaka huu ambalo ni asilimia moja (1%) na punguzo lililokuwepo siku zote la hayati JPM ambalo ni asilimia mbili (2%). Punguzo lote kwa ujumla wake kwa sasa kwa gross pay ya mtumishi yeyote yule inabidi liwe asilimia 3. Wenye mshahara iliyo juu ya mshahara wa kima cha chni wanaweza wasifaidike na punguzo hili kwani watu walio wengi hawajui au huwa hawajishughulishi na mahesbabu haya madogo madogo, ya kuwawezesha wajue kodi za mishahara yao
 
Leo ndio leo.
Mwisho wa kuingiza watumishi kwenye mfumo.Mbivu na mbichi kujulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…