Waziri wa Utumushi, Mchengerwa: Maafisa utumishi wasiopandisha madaraja kutumbuliwa

Waziri wa Utumushi, Mchengerwa: Maafisa utumishi wasiopandisha madaraja kutumbuliwa

Maafisa utumishi wameanza kutuambia eti tupeleke barua za kuthibitishwa kazini na ilihali zipo kwenye faili za mtumishi hapo halmashauri[emoji38][emoji38],
Kazi za kiserikali huwa hazieleweki,unaweza ukamuuliza mwanao unaitwa Nani?[emoji848][emoji848]

Mi nilitakiwa nipande daraja Mara mbili sijui watapiga mseleleko au mi ndo sielewi!!!
Mimi nilikuwa kwenye bajeti ya 2018/2019 na mwaka jana nimekuja masomoni tangu 2020 nasubiri afisa utumishi aniteme niende Dodoma,
 
Mimi nilikuwa kwenye bajeti ya 2018/2019 na mwaka jana nimekuja masomoni tangu 2020 nasubiri afisa utumishi aniteme niende Dodoma,
Hapo sasa patamu. Kuna jamaa yangu ajira 2013 alienda masomoni mwaka 2017 lakini wenzake wakapanda 2019. Yeye hakupanda kwa kuwa yuko masomoni. Sasa amemaliza degree 2020 na HESLB wanamlima makato ya 15% kwa TGTS B yake. Huenda hayumo kwenye mpango wa wanaopanda
 
Well done Mchengerwa, upele umepata mkunaji, kuna baadhi ya taasisi za serikali zimejaa upumbavu ambao ni aibu kuandika humu. Ikibidi tutaandika
 
Hizi mbwembwe za awamu ya sita zipo kasi sana, anyway, yetu macho na masikio.

===

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa"

"Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo mara moja. Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja wakati anastaili, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo aliyemkwamisha mara mara moja. Haiwezekani mtumishi anaajiriwa leo, umempita miaka minne mnapokea mshahara sawa, haiwezekani. Serikali haitaki mtumishi wa umma aonewe, stahiki zenu ni haki yenu hampaswi kuziomba"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Nikipita katika sehemu zangu za kazi, nikikuta kero za watumishi, watumishi wanaandika barua hajibiwi miezi sita. Aliyekuwa katika mamlaka yangu nitatengua nafasi yake. Aliye nje nitaomba mamlaka ya uteuzi wamtengue. Watumishi wa umma mjipange, wizara hii sasa imepata kijana. Bahati mbaya sijui nzuri nilikuwa hakimu, ninapenda haki. Tuwasikilize wananchi wanaofika katika ofisi zetu.

Nikikuta wamesimama wanasubiri kusikilizwa na anayepaswa kusikiliza hayupo, nitamsikiliza Mimi"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Vipi kuhusu maafisa utumishi ambao huwa wanafanya mbinu za kushusha watu vyeo kisisriri, au wale ambao huwa wanapandisha watumishi madaraja halafu wanaanza kuwalipa mshahara wa daraja lililo nyuma yake? Mh Waziri inabidi awaangalie na hao pia, nao wapo. Vile vile inabidi awe mwangalifu na punguzo la kodi ya mshahara la mwaka huu ambalo ni asilimia moja (1%) na punguzo lililokuwepo siku zote la hayati JPM ambalo ni asilimia mbili (2%). Punguzo lote kwa ujumla wake kwa sasa kwa gross pay ya mtumishi yeyote yule inabidi liwe asilimia 3. Wenye mshahara iliyo juu ya mshahara wa kima cha chni wanaweza wasifaidike na punguzo hili kwani watu walio wengi hawajui au huwa hawajishughulishi na mahesbabu haya madogo madogo, ya kuwawezesha wajue kodi za mishahara yao
 
Maswali:
1. Kwanini suala la kupandishwa madaraja lisiwe automatically?
Data zote za watumishi ziko kwenu.
2.Je, ni watumishi elfu 80 na ushehe tu ndio wanaostahili madaraja mapya?
Kama jibu yes, maana yake tayari maandalizi yalishafanyika sasa kwanini mtafute kiki kwa ma H.R?
Hapa kuna kauongo kanaandaliwa.
Haya ndio yale mauzauza ya Magufuli. Akishindwa jambo anamtafuta wa kumtumbua ili apate kiki
Leo ndio leo.
Mwisho wa kuingiza watumishi kwenye mfumo.Mbivu na mbichi kujulikana.
 
Back
Top Bottom