TANZIA Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda amefariki dunia

TANZIA Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda amefariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Bunge; Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Balozi Kijazi amethibitisha taarifa hizi na familia imethibitisha kutokea kwa msiba huu.

Apumzike kwa amani
kigoda.jpg
Abdallah Omar Kigoda enzi za Uhai wake

=======

UPDATES:

Toka Serikalini:

Kwa maskitiko makubwa serikali inatangaza Kifo Cha Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda MB. Waziri wa Viwanda na-Biashara kilichotokea katika Hospitali ya Apollo, New Delhi India leo.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu pamoja na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu-na mazishi- zitaendelea kutolea na serikali hapo mbeleni.

Sisi wote ni wa mwenyezi na kwake- tutarejea.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.
 
Kuna bwana anaishi Handeni amenishtua kwa habari za kifo cha Kigoda muda huu wa saa 1.30 Tar 11/10/2015. Kama yupo mtu wa Handeni au anayejua taarifa hizi naomba ukweli wake.
 
WAZIRI KIGODA AFARIKI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu, Ofisi ya Bunge yathibitisha.
 
R.I.P. Ulichoweza kufanya ulifanya regardless of the results! We are also comming soon!
 
TANZIA:
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr Abdallah Kigoda amefariki dunia jioni hii nchini India.

Taarifa hizi zimethibitishwa na balozi wetu wa Tanzania nchini India, Mhe. Balozi Kijazi.

Mungu ailaze roho ya Dr Kigoda mahala pema peponi Ameen.
 
Aliekuwa waziri wa Viwanda na biashara na Mbunge wa Handeni DR Abdala kigoda amefariki dunia.

Taarifa zilizofika ofisi ya bunge zinasema Kigoda amefariki saa kumi na moja jioni katika hosptali ya Apollo nchini India.
 
Ndo raha ya uzushi. Muda tu unaamua km ni kweli au la au kuna dalili ikawa hivyo.

RIP Kigoda.
 
Back
Top Bottom