TANZIA Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda amefariki dunia

TANZIA Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda amefariki dunia

R.I.P Abdala Kigoda!! Mungu kama angeuliza ni nani amchukue badala yako ningemsotea Npe. Alikuwa mkimya,mpole,hana majivuno na hana kauli mbaya.
 
RIP KIGODA

Poleni familia na wana Handeni wote. Mungu awafariji
 
Hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Bunge; Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Balozi Kijazi amethibitisha taarifa hizi na familia imethibitisha kutokea kwa msiba huu.

Apumzike kwa amani

=======
UPDATES:

Toka Serikalini:

Kwa maskitiko makubwa serikali inatangaza Kifo Cha Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda MB. Waziri wa Viwanda na-Biashara kilichotokea katika Hospitali ya Apollo, New Delhi India leo.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu pamoja na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu-na mazishi- zitaendelea kutolea na serikali hapo mbeleni.

Sisi wote ni wa mwenyezi na kwake- tutarejea.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.

hawa CCM wameshindwa kuboresha huduma za afya hapa nchini lakini wao wakipiga chafya tu hukumbilia India kutibiwa. pamoja na telekeza wananchi huduma za hospitali kwa wananchi, kifo kikishawadia hakikimbiliki. Mungu ailaze pema roho ya marehemu. Amina.
 
Mungu akakukumbuke kwa wema wako juu ya wana Handeni na Taifa letu kwa ujumla.
 
RIP Kigoda, ola inakuaje taarifa hii itolewe na ofisi za bunge wakati bunge lilishavunjwa?
 
R.I.P Abdala Kigoda!! Mungu kama angeuliza ni nani amchukue badala yako ningemsotea Npe. Alikuwa mkimya,mpole,hana majivuno na hana kauli mbaya.
Aisee bro una roho mbaya, utaombeaje mtu flani afe ati kisa humpendi?
 
hawa CCM wameshindwa kuboresha huduma za afya hapa nchini lakini wao wakipiga chafya tu hukumbilia India kutibiwa. pamoja na telekeza wananchi huduma za hospitali kwa wananchi, kifo kikishawadia hakikimbiliki. Mungu ailaze pema roho ya marehemu. Amina.

Mbaya zaidi wakienda wanarudi kwenye jeneza. Lowasa wetu anadunda speed 120km/h
 
Pumzika salama Alhaji Abdalah Omari Kigoda. Sisis niwamwenyezi mungu na kwake tutarejea.
 
Alikufa zamani sana ila wabongo ubishi tu

Ina maana na hii taarifa nayo ni ya siku nying...?

attachment.php

R.I.P dr. Kigoda , ingawa ulikuwa chama la magamba ila
mimi kwa binafsi yangu nilikuwa nina kukubali sana.
 
Back
Top Bottom