TANZIA Waziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba afariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19

TANZIA Waziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba afariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19

Kutokana na maneno ya kipumbavu aliyoongea.
Kukaa kimya nako Ni busara lkn ma CCM hawakujui Hilo.
Bilioni 11 zilimfanya ajisahau kabisa (sio Mimi, mahakama ilidhibitisha)

..sijui kwanini wenzangu mnaumizwa zaidi na maneno ya kipumbavu ya Mramba, kuliko maamuzi mabaya ya Mkapa.
 
Niache kwanza natesti mitambo

..hivi unafahamu nani alikuwa Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo?

..Ninapenda kumjua kwasababu yeye ndiye Waziri aliyekuwa na dhamana ya manunuzi ya ndege ya Raisi.
 
Unaweza kuishi maisha ya kuwajali wengine (kuwapenda kama unavyojipenda mwenyewe) na ukawa umefanya jambo kubwa kuliko hata kujenga nyumba za ibada mia moja. Siyo kwamba napingana na wewe ila nataka tu kuonyesha kuwa siku hizi watu wamekuwa kama wanyama na hawathamini binadamu wengine na ndipi hasa tatizo linapoanzia. Ukiwapenda wenzako hutawafunga jela bila sababu, wala hutaiba fedha zilizotengwa kununua dawa za hospital, wala hutajenga hutatembea na mke wa mtu.....mambo ni mengi.
Mwafrika atakuwa na maendeleo pale siku ile roho ya ubinafsi ikimtoka
 
..hivi suala la ununuzi wa ndege ya raisi kwanini analaumiwa mramba peke yake?

..kwanini rais mkapa, na waziri wa uchukuzi[ anayehusika na ndege] wa wakati huo, hawalaumiwi?
Mramba ndie kiranja mkuu
 
Mwafrika atakuwa na maendeleo pale siku ile roho ya ubinafsi ikimtoka
Ni kweli iliyoje? Mwafrika anajifikiria yeye tu! Na hasa mtanzania. Kama siku umezuka mtindo wa kujipendekeza na kuabudu viongozi wa nchi kwa mambo ya kijinga kabisa ili kusaka vyeo. Huu mtindo umekolea zaidi enzi za Magufuli.
 
Ni kweli iliyoje? Mwafrika anajifikiria yeye tu! Na hasa mtanzania. Kama siku umezuka mtindo wa kujipendekeza na kuabudu viongozi wa nchi kwa mambo ya kijinga kabisa ili kusaka vyeo. Huu mtindo umekolea zaidi enzi za Magufuli.
Hapa ni mfano halisi hapa rungu akiabudiwa Ili utumbuzi usimpate,waziri hapo anaangalia pesa

IMG-20210817-WA0003.jpg
 
..hivi suala la ununuzi wa ndege ya raisi kwanini analaumiwa mramba peke yake?

..kwanini rais mkapa, na waziri wa uchukuzi[ anayehusika na ndege] wa wakati huo, hawalaumiwi?
Hivi ilikuwa ndege au ni ile rada?
 
Waziri wa Zamani, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo agosti 17 akiwa anapatiwa matibabu regency hospital. Mramba alilazwa wiki mbili zilizopita kwa maradhi ya COVID-19.

Kifo chake kimesababishwa na Mshituko wa Moyo(Cardiac arrest)

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa fedha, pia Waziri wa viwanda, biashara na masoko

View attachment 1895289
Basil Pesambili Mramba

Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered.

Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy.

We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage.

The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen.

Godfrey B. Mramba


======
Huyu ndiye Basil Pesambili Mramba

Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa UVIKO-19.

Akiwa ni mmoja wa mawaziri waliowahi kufungwa kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa kwenye nafasi zao za uongozi.

Mramba ambaye amewahi kufungwa miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka alizaliwa mwaka 1940 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda na kupata shahada ya kwanza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha City London kilichopo Uingereza na kupata Shahada ya Uzamili katika Biashara.

Amefanya kazi Serikalini katika nyadhifa mbalimbali. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

Mwaka 2006, Mramba aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2008 ambapo alibaki kuwa mbunge wa kawaida.

Julai 7, 2015, Mramba na Yona walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Kesi yao ilitokana na makosa waliyofanya wakati Mramba akiwa Waziri wa Fedha na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hata hivyo, Februari 6, 2016, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwabadilishia adhabu viongozi hao wastaafu na kuwa kifungo cha nje wakiwa tayari wametumikia miezi saba gerezani.

Katika kutekeleza adhabu hiyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti na kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza – Palestina kila siku siku asubuhi kwa miezi tisa. Walitekeleza adhabu hiyo mpaka walipokamilisha Novemba 5, 2016.

Tangu walipomaliza adhabu hiyo, Mramba hakuonekana hadharani kama ilivyo kwa wastaafu wengine maarufu. Amekuwa kimya kwa kipindi kirefu mpaka alipofariki leo Agosti 17 katika hospitali ya Regency kutokana na maradhi ya UVIKO-19.
Naona umesahau kuwa aliwahi kuwa Mfungwa Bandia wakati wa Kikwete. Pia aliteuliwa kuwa msimamizi wa usafi hosipitali ya Sinza.
 
Back
Top Bottom