Waziri wa zamani wa Masuala ya kigeni Ethiopia auawa na Jeshi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jeshi la Ethiopia limetangaza kwamba limemuua waziri wa zamani wa mambo ya nje Seyoum Mesfin, mmoja wa wanachama waanzilishi wa chama Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Bw.Seyum, ambaye alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa kutoka mwaka 1991 hadi 2010, aliuawa pamoja na wanachama wengine wa ngazi ya juu TPLF kaskazini mwa jimbo la Tigray, wanajeshi walisema.

Serikali ilikuwa imetoa waranti ya kukamatwa kwake- pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu katika chama hicho – kufuatia oparesheni ya kijeshi ya mwezi Novemba eneo la Tigray. Zawadi ya birr milioni 10 sawa na ($254,000; £187,000) iliahidiwa kutolewa kwa wale watakaotoa taarifa zitakazosidia kukamatwa kwao.

Jeshi linasema kwamba liliwaomba wajisalimishe lakini wakakata kufanya hivyo. Makumi ya wancahama wengine wa TPLF waliuawa na wengine kukamatwa katika oparesheni ya hivi punde, iliongeza kusema.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamuru oparesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray mnamo Novemba 4 na kuiondoa madarakani chama tawala, baada ya vikosi vyake kuvamia kambi ya majeshi ya serikali.

1610603439487.png
 
Chuki hizo hazitakaa ziishe, wataendelea kuuwana tuu
 
Jamaa alianza vizuri

Now kaivuruga nchi ile mbaya
 
Ndo maana wanasema mwanadamu sio mtu wa kulizika hata kidogo, yani ushakuwa waziri iweje uanzishe uasi wa kujitenga.ni tamaa ya uchu wa madaraka inawasumbua
 
Mbona unaniangusha mkuu. Kwa hiyo akitokea kichaa mmoja mkoa wa Mara au Kigoma akatanga kujitenga utakubali aruhusiwe kuunda kundi la kigaidi na kuiba silaha kwenye kambi za JWTZ uku akiteka vijiji.
Namaanisha Huyo waziri wa zamani marehemu
 
Back
Top Bottom