Labda niwape chachu ambayo inatukumba watz kwenye project , mwana 2020 nilipata partner wa 3 wote walikuwa ni wamafasia na wanawasfa kwenye chuo flan. Niliwafuta nikaongea nao kuhusu eBook ambazo watakuwa wana andika na kupakia kwenye app wanafunzi wanasoma kwa kipia kama king'amuzi cha azam(subscription business model), tukaa kikao tukaongea kama intellectual , nikawaonesha pesa ilipo kama tutafanikisha swal la eBook app na contents( 100 ebook ziwe published kwenye app ndani ya siku 30).
Nikapewa task ya kutengeneza app ya eBook ambayo inapkia pdf na ina mfumo wa subscription model payment. Nilipewa siku 30 uku wao wakiandaa contents, nilipambana kwel sio kidogo nikadesign na ku implement kile tulichokubaliana kwenye kikao.
Nikapakia playstore mzigo ukabaki kuweka contents wanafunzi waanze kulipia na kusoma, kwa wakati huo niliweka GOOGLE PAY kama njia ya malipo maana kuna tigopesa, airtel money , mpesa na credit card ndani ya Google Pay.
Imefika siku 30 jamaa hata articles 20 hajafikisha ni excuses kibao mara nacte wakuja kukagua chuo mara nilitingwa blah blah blah.
Tulifel kwasababu ya contents, wanafunzi wapo chuon kwao sio ishu tena. Nilitumia nguvu nyingi kwenye hakuna, kuwa na watu smart ambao mko committed kufanya jambo lenye kuleta pesa ni kazi ngumu sana kwa nchi yetu.
Hapa uwaga namkumbuka Raisi Magufuli alipoenda airport nakukuta scanner mbovu toka miezi mitatu , akasema "Watanzania mna dhambi gani?".
Mm mwenye najiulizaga watz tuna dhambi gani tulifanya ambayo inatutafuna kizazi na kizazi.
Mtoa mada tegemea kupata wafuasi wengi sana uko whatsapp ila mwisho wa siku tegemea kuwa disappointed.
Watz tupo vzuri sana kwenye porojo na sio kwenye vitendo, lait tungekuwa watu wa vitendo tungefika mbali sana kama taifa.
Mtoa mada inabd ujifunze kuchagua watu ambao wako committed kufanya kitu kwasababu ya maisha yao ya baadae. Yesu mwenyewe alifanya machaguzi kwa wanafunzi ambao ataambatana nao.
Usije ukamweka friend , tafuta watu ambao ni smart ambao mtafit kwenye project ambao iko mbele yenu.
Unaweza kukuta group lina watu 100 wanaotoa maon yao ni watatu daily wengine wako kimya utasema wamelazimishwa kujiunga. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Watz ni watu wa ajabu sana ukija kwenye upande wa whatsapp group, mara nyingi najikuta kama admin inanilazim ni left [emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Mtoa mada nimekupa experience kidogo kuhusu wabongo kwenye mchongo wa pesa, be prepared for disappointed at the end...