Wazo Dokezi: Upigaji wa Uchaguzi Mkuu Utaanza "Soon"...

Wazo Dokezi: Upigaji wa Uchaguzi Mkuu Utaanza "Soon"...

Mzee mwanakijiji umerudi?
Amerudi Magufuli si hayupo msukuma mwenziwe,alikuwa Mkapa Mmakonde alikuwepo Kikwete ndio usiseme Magufuli mtakatifu kwake na ccm ilikuwa nzuri sasa huyu mzenji tena muislaam asirudi vipi?? Kazi kwelikweli waafrika, America haijambadirisha.
 
Ulitaka wapinzani wafanya nini ili kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Je,jukumu hilo nila umma wote au kundi la wachache.

Vipi wale wanao jifanya Wazalendo (DP) wamefika wapi au wamezidiwa akili na wanasiasa.
"Wale conservative waliopo st.peters wanaotaka Hali iendelee kubaki hivi hivi yaani kuwalinda wakubwa kwa kitabu kilichopo,watakaushwa kimya kimya"Tumia akili thread ya operation imesitishwa the state wamesema apewe muda!!Kasome mchango wa Tumia akili namba 129 kwenye uzi,utaona kwanini Kuna baadhi ya watu hatunao na wengine ni majasusi wabobezi na wengine tumewazika na wengine Kuna tetesi zinawahusu kwa sana!!

WE huoni hilo likitokea japo kiustadi sana!!?
 
Mpaka sasa wahafidhina wanaonekana kuwa wenye nguvu na weredi wa hali ya juu,ndio maana hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya maigizo ya kijinga tu.

Apewe muda na wakati huo huo hao wahafidhina ndo wamempa hiyo nguvu,hawezi pingana na ma-boss wake.

Ngoja tuone mchakamchaka wa 2025.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya vitu ambavyo huwa vinafanywa 'vizuri' na watawala wa watawaliwa unapoelekea mwaka wa uchaguzi ni jinsi gani huwa wanajipanga kujipendezesha kwa wakubwa wa dunia. Unajua pale nchi inapojisema tu kuwa ni ya "kidemokrasia" basi wakubwa wanaanza kuangalia vitu vinavyofanyika hasa linapokuja suala la uchaguzi. Uchaguzi unachukuliwa kama kipimo hasa cha ni jinsi gani nchi imekomaa kidemokrasia.

Inapotokea tu kuwa kuna figisufigisu fulani basi wakubwa wa dunia - US, UK, EU, UN na taasisi mbalimbali huwa na haraka ya kutuamulia kama uchaguzi ulikuwa huru na waki (free and fair). Lakini wao hawaanzii siku ya uchaguzi tu bali wanaangalia hata miezi michache nyuma. Na taasisi za ndani na za nje zote zinaanza kutoa "mafunzo" (training) kwa waangalizi wa ndani na wa nje. Waangalizi wa ndani ni wale wa taasisi za kiserikali na za nje ya serikali ambazo huwa zinafuatilia uchaguzi kuanzia maandalizi hadi utangwazaji wa matokeo ya uchaguzi na hata uapishaji wa uongozi mpya.

Zinapokuwepo taasisi za kidini na zisizo za kidini za ndani. Lakini linapokuja lile la waangalizi wa nje wao wanaweza kushirikiana na taasisi hizi za ndani au wakawa na watu wao wenyewe mara nyingi hawa huanza kuingia nchini kama miezi mitatu kabla ya siku ya uchaguzi mkuu. Wakiongozwa na utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi basi taasisi hizi hupewa uhuru wa kutembelea sehemu mbalimbali kuona maandalizi ya uchaguzi yanavyokwenda na wanalindwa na sheria na taratibu mbalimbali. Taasisi hizi huwekewa masharti ambayo wanatakiwa wayafuate.

Lakini kubwa linalotuhusu leo - ni jinsi gani - wakubwa wa dunia wanaweza kuizawadia nchi kwa kuandaa uchaguzi mzuri. Hivyo watawala wa watawaliwa hujitahidi saini kupambisha maandalizi ya uchaguzi ili jicho la wakubwa lianze kuangalia kwa mapenzi. Hili linatuleta kwenye mada ya leo.

Tunavyoelekea uchaguzi mkuu mwakani tutaanza kusikia na kuona jinsi watendaji wa serikali wa ngazi mbalimbali wakianza kuonesha na kuahidi jinsi gani uchaguzi wa mwakani utakuwa na tofauti kubwa na ule wa 2020. Unaweza kuamini kabisa - ukiwasikiliza sana - kuwa hiki chama kinachoenda kuandaa uchaguzi ujao sicho kilichoandaa uchaguzi uliopita na kuwa sasa wamepata akili ya kuendesha uchaguzi mzuri, usio kuwa na rabsha wala washawasha.

Kwa vile wakubwa wataanza kuvutiwa basi muda si mrefu tutaanza kusikia wakubwa wakitoa misaada ya kuandaa uchaguzi mkuu. Kuna fedha nyingi - mabilioni- ya maandalizi ambavyo yataelekezwa kwa vyama vya siasa na wanufaika wakubwa wakiwa ni chama cha watawala wa watawaliwa. Ikumbukwe kuwa katika fedha hizo kuna ulaji mkubwa unaofanyika kuanzia kwenye maandalizi ya makabrasha ya mafunzo, mafunzo yenyewe, uchaguzi wa nani atakuwa mwangalizi (ndugu, jamaa, na marafiki) na taasisi zao za NGO zikijiandiksha tume ya uchaguzi kuwa watakuwa ni sehemu ya waangalizi wa ndani au wa kimataifa.

Itaendelea...
Tukisema siasa ni ajira/ uwekezaji /biashara kuna wanaopinga
 
Mpaka sasa wahafidhina wanaonekana kuwa wenye nguvu na weredi wa hali ya juu,ndio maana hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya maigizo ya kijinga tu.

Apewe muda na wakati huo huo hao wahafidhina ndo wamempa hiyo nguvu,hawezi pingana na ma-boss wake.

Ngoja tuone mchakamchaka wa 2025.
Wahafidhina wanaondokewa ma watu muhimu,wengine wataugua na kupoteza kumbukumbu!!

Hai vijana machachari wenye ndoto kubwa kubwa wanaondokewa na watu muhimu (kuuguliwa pia) ambao na Wana sauti kwenye vikao vizito vya ushauri!!

Jamaa wameanza na mizizi halafu matawi yatakufa naturally!!!

Bado wawili TU wakiugua au mmoja akaenda bas hakuna hao madogo kufurukuta tena,na huyu alieshika strong hold hawezi toboa chujio la mwakani,Kuna team tatu zitasukwa zivurugane Ili kumpitisha mkusudiwa fulani lakini atapita mwingine na kusudi la Mungu litasimama vema!
 
Tumeshaanza kusikia kauli zikidai uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni mbaya kwani uliwagawa na kuwaogofya Watanzania..

Lakini wanaosema hayo ndiyo wale wale siku zote hawajakanusha tuhuma za wizi wa chaguzi kuu zilizopita.

Yetu macho kwenye hizi pilika za maandalizi

Yaani hapo wanataka kumtupia zigo lote Mwendazake as if wao hawakuhusika. Yaani Maza wanataka kumtoa kabisa wakati yeye binafsi alitamka hadharani kuwa hata kama tutachagua upinzani CCM ndiyo itakayoshinda ....!!
 
Wahafidhina wanaondokewa ma watu muhimu,wengine wataugua na kupoteza kumbukumbu!!

Hai vijana machachari wenye ndoto kubwa kubwa wanaondokewa na watu muhimu (kuuguliwa pia) ambao na Wana sauti kwenye vikao vizito vya ushauri!!

Jamaa wameanza na mizizi halafu matawi yatakufa naturally!!!

Bado wawili TU wakiugua au mmoja akaenda bas hakuna hao madogo kufurukuta tena,na huyu alieshika strong hold hawezi toboa chujio la mwakani,Kuna team tatu zitasukwa zivurugane Ili kumpitisha mkusudiwa fulani lakini atapita mwingine na kusudi la Mungu litasimama vema!
Huwezi tegemea jambo jipya kwenye mfumo ule ule ni kupoteza muda,yaani bado hao DP wanataka kutumia chama kile kile kutaka kuleta mageuzi ndani ya taifa hili,ambapo wameshindwa miaka 60s ya uhuru kufanya lolote huu ni uwendawazimu wa mchana kweupe.

Ndio maana nasema hakuna mwenye akili timamu anaweza amini hizo story,yaani utumie watu walewale kutatua matatizo yaliyo sababishwa na hao hao,hakuna watu smart uko zaidi ya kujaa sifa.

Huwezi niambie katika nyama vyote,hakuna watu ambao wanaweza kuleta mageuzi isipokuwa watoke huko huko kuliko jaa wezi na wapenda madaraka.
 
Ni mjinga tu anaweza kuamini huu UONGO
akina Thomaso kama wew ili waamini si mpaka waguse 🐒

sasa wakati huo utakapoona, utakapo jua, na kuamini kwamba uchaguzi ulikua huru na haki, lakini pia ni the most cridible elections in the world, uchaguzi wenyewe utakua umekwisha 🐒
 
..utakapo jua, na kuamini kwamba uchaguzi ulikua huru na haki, lakini pia ni the most cridible elections in the world, uchaguzi wenyewe..
Hahaha..
Yaani ccm hiyo hiyo na tume yake binafsi ya uchaguzi waendeshe "the most credible election in the world.."?
Naona una kipaji cha comedy broo!
 
Hahaha..
Yaani ccm hiyo hiyo na tume yake binafsi ya uchaguzi waendeshe "the most credible election in the world.."?
Naona una kipaji cha comedy broo!
kama kushinda uchaguzi halali kwa kishindo ni comedy,
hiyo tutaifanya kwa bidii sana katika kila aina ya uchaguzi ili kukuchekesha zaidi 🐒
 
Acha majungu we mzee, alipokuwa yule Dikteta mlikuwa kimya mkampongeza. Zile Fedha za plea bargain alikuwa anaweka akaunti gani?
 
Back
Top Bottom