Wazo gani bora la biashara kati ya hizi?

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Nina mdogo wangu ni mhanga wa ajira, amemaliza chuo tangu 2015, sasa amezichanga changa kwenye kilimo mpaka amefikisha million 10, sasa anaona aachane na kilimo afanye biashara. Ameniomba nimsaidie kumchagulia wazo bora kati ya haya ;

1.Kununua gari dogo aina succeed kwa ajili ya daladala, anasema eneo alilopo wanalaza 30 ~50 kwa siku.

2.Biashara ya nafaka kama mchele, maharage, soya, mahindi n.k, Awe ananunua toka eneo ambalo bei ipo chini anauza sehemu nyingine ambayo bei ipo juu.

3. Afungue duka la reja reja au vifaa vya pikipiki kwa gharama ya shilingi million 5 halafu tano nyingine anunue gari dogo kwa ajili ya uber/taxify.

4.Afanye biashara ya mbao toka vijijini kupeleka mjini kwenye mahitaji mengi.

Je, wazo gani ni bora kati ya hayo.
 
Hayo yote ni mawazo mazuri, ila tu biashara inategemeana na mambo mengi ikiwamo location, watu wanao kuzunguka, mazingira na vitu kama hizo.
 
Nina mdogo wangu ni mhanga wa ajira, amemaliza chuo tangu 2015, sasa amezichanga changa kwenye kilimo mpaka amefikisha million 10, sasa anaona aachane na kilimo afanye biashara. Ameniomba nimsaidie kumchagulia wazo bora kati ya haya ;

1.Kununua gari dogo aina succeed kwa ajili ya daladala, anasema eneo alilopo wanalaza 30 ~50 kwa siku.

2.Biashara ya nafaka kama mchele, maharage, soya, mahindi n.k, Awe ananunua toka eneo ambalo bei ipo chini anauza sehemu nyingine ambayo bei ipo juu.

3. Afungue duka la reja reja au vifaa vya pikipiki kwa gharama ya shilingi million 5 halafu tano nyingine anunue gari dogo kwa ajili ya uber/taxify.

4.Afanye biashara ya mbao toka vijijini kupeleka mjini kwenye mahitaji mengi.

Je, wazo gani ni bora kati ya hayo.
Mbao mkuu
 
Hayo mawazo yote ni mazuri,isipokuwa hapo kwenye namba 3 hiyo mambo ya Uber/Taxify sina uhakika kama yanaweza kumtoa...
 
Aendelee na kilimo tuu,aboreshe kilimo,afanye kwa akil,..
Ana experienc tayar na kilimo,..najua kimemchosha,ajipe mwez m1 wa kupumzika asfanye chochote akusanye nguv arud kilimoni

Hzo biashara nyingn ni pasua kichwa asijidanganye kabsaa,hyo hela itapotea huko na atajuta...labda kdogo nafaka ila hzo nyingne atajuta,..mi uber nshafanya upuuz mtup,.daladala mzee wangu alishafanya..so najua wat am sayn
 
Mawazo yote mazuri nahisi yeye pia atakuwa na kile anachokipenda zaidi hapo, mwambie yeye achague kipi anaona ni bora!
 
Na mbao pia usifanye hyo hela ndogo kutengeneza faida,na harakat za mbao had ukae sawa vibal vyake tuu uhangaikaj,hyo10mil itabak 7mil n less ..af ina utapel mwiiingiii,acha kabsa
 
Aendelee na kilimo, kama kaweza kupata iyo 10m, ivo akilima kisasa na kuongeza ukubwa wa mashamba atapata faida zaid.
 
Nikushauri tuuh sababu me in dereva wa uber iyoo namba 3 ungeitoa kabisa biashara kama utumwa gari zinachoka sana bei yenyewe mbuzi ili upate ela lazima upige Massa yao yote 12 na isiombee gar ianze kusumbua me gar la mkopo limenishinda unaeeza amka aunakaz wamekufungia mgomo mkubwa unafuata lbda kma watabdlika
 
Nina mdogo wangu ni mhanga wa ajira, amemaliza chuo tangu 2015, sasa amezichanga changa kwenye kilimo mpaka amefikisha million 10, sasa anaona aachane na kilimo afanye biashara. Ameniomba nimsaidie kumchagulia wazo bora kati ya haya ;

1.Kununua gari dogo aina succeed kwa ajili ya daladala, anasema eneo alilopo wanalaza 30 ~50 kwa siku.

2.Biashara ya nafaka kama mchele, maharage, soya, mahindi n.k, Awe ananunua toka eneo ambalo bei ipo chini anauza sehemu nyingine ambayo bei ipo juu.

3. Afungue duka la reja reja au vifaa vya pikipiki kwa gharama ya shilingi million 5 halafu tano nyingine anunue gari dogo kwa ajili ya uber/taxify.

4.Afanye biashara ya mbao toka vijijini kupeleka mjini kwenye mahitaji mengi.

Je, wazo gani ni bora kati ya hayo.

Namba 2 italipa zaidi.
 
Hapo biashara nzuri Ni hyo ya kuuza nafaka tu hizo zingine zilizobaki ni ubabaishaji tu Kama kamari.
Afanye biashara ya nafaka lkn pia hyo ya kilimo asiiache bali ajigawe kwenye kuuza nafaka na pia kulimisha watu na awe anaenda kukagua shamba mara moja moja hapo atatoboa.
 
Back
Top Bottom