Wazo kwa Serikali yetu kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani

Wazo kwa Serikali yetu kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Kuundwe kikosi kazi madhubuti kwa ajili ya kupambana na majanga. Tumezoea kuona kuwa Jeshi la zima moto ndio liko kwa ajili ya kupambana na majanga hasa ya moto lakini kiukweli kuna majanga zaidi ya moto ambapo yanapotokea jeshi hilo haliwezi kuingilia kati.

Sasa nashauri hivi kama ilivyo kwa marekani kuna kikosi kinaitwa SEAL yaani Sea Land Air yaani hawa ni wanajeshi hatari sana ambao wana taaluma za ukomando wa hali ya juu majini nchi kavu na angani na ndio waliofanikisha kumuua Osama.

Anyway hilo ni jeshi lakini nimetoa mfano huo kwa sababu hata jeshi la zimamoto na lenyewe pia ni jeshi na wanapitia mafunzo ya kijeshi nadhani kama nimekosea nirekebishwe.

Sasa nilikuwa na wazo moja tutumie jeshi hili hili tulisuke zaidi kwa maana hiyo liongezewe majukumu na mafunzo ya hali ya juu kwa nyanja zote za uokoaji majini, angani na nchi kavu ikiwezekana wapitie mafunzo ya aina kama ya Ukomando japo dhumuni kuu sio mambo ya kivita lakini ni uokoaji katika kada zote nilizotaja tusiogope kusema ni gharama ikiwezekana hata mafunzo mengine yawe nje ya nchi sio vibaya.

Najiuliza hivi zimamoto wanajua kuogelea je zimamoto wanajua kuruka na parachute je zimamoto wakiwa porini au tuseme jungle wanawezaje kukabiliana na hatari za porini kimafunzo?.Je ikitokea watu wakifukiwa na kifusi migodini au kwenye kuchimba mawe je jeshi letu wana taaluma gani ya kukabiliana na hali hiyo.

Migodini lazima wakaguliwe na serikali kwa kupitia jeshi la zima moto lakini nakiri ni ukweli ulio wazo migodini wako vizuri mno kivifaa na hata kimafunzo kuliko hata hiyo serikali inayowakagua.

Nashauri kuwe na ushirikiano kati ya migodi na jeshi letu wawe wanafanya drills za mara kwa mara kubadilishana ujuzi kimafunzo.Ni ukweli ulio wazi migodi wana vifaa vya kisasa vya kuzimia moto kuliko jeshi letu mfano mzuri kuna vifaa automatic ambavyo moto ukitokea vinajifuatua vyenyewe kuzima mto na pia kuna alarm kila sehemu moto ukitokea unaonekana ni sehemu gani.

Mjiulize mbona majanga yakitokea kuna mahali tunatumia Jeshi letu la wananchi kusaidia? Wao wamekaa kivita zaidi lakini kiukweli wanatoa msaada mkubwa mno nawasifu kwa hilo.

Naomba kuwasilisha hoja
 
Back
Top Bottom