Wazo kwa TTCL: Kuwepo kampuni ndogo nyingi ndani ya TTCL

Wazo kwa TTCL: Kuwepo kampuni ndogo nyingi ndani ya TTCL

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Direct to point
Kutokana na changamoto ya mashirika ya umma kusua sua kutoa huduma kwa wananchi na kuwepo kwa ufanisi mdogo wa mashirika haya. Lakini mbali ya hapo haya mashirika yameendelea kula ruzukunza seikali miongo na miongo bila ya kuzaa matunda mfano posta, ttcl, tanesco, tazara, air tanzania n. K
Nashauri kuwepo na makamluni madogo ndani ya mashirika haya ambapo makampuni haya yatakuwa yanatoa huduma kwa jamii kwa ushindani sana.

Mfano ttcl uoande wa fiber kukawa na kampuni 4 zote za kusambaza fiber majumbani ila yote yawe chini ya ttcl na malipo yote yatafanywa kwa control number za account ya serikali isipokuwa kuna mgawanyo wa asilimia za mapato mf. Kwa asilimia za mapato kati ya kampuni (mtoa huduma) na taasisi (mwenye huduma yake).

Nimeliona hili Tanesco kwani kwa dsm pekee wilaya ya ubungo nmeona kuna makampuni ma3 hv. Moja wapo likiitwa MKOMBOZI jingine nmelisahau.

Umeme ukiomba leo ndani ya siku 3 surveyor kafika na ndani ya wiki tyr wameshakuja kukufungia umeme na hata baada ya kufungiwa umeme bado hadi unapigiwa simu kuulizwa kama kuna eneo jingine labda unataka au unaonaje huduma. Nmeomba umeme sehemu 3 tofauti wilaya tofauti nmeliona hili swala. Ni zuri sana

Ni rai yangu kwa mashirika mengine vichomi kama ttcl, posta na airtanzania na tazara na kadharika
Nawasilisha wazo zuri hili kwa viongozi wangu wapiga dili. Ajabu wazo hili litaishia hapa hapa JF
 
Back
Top Bottom