Wazo la biashara kutengeneza Umeme binafsi

Wazo la biashara kutengeneza Umeme binafsi

D-Smart

Member
Joined
Mar 23, 2023
Posts
77
Reaction score
204
Nina wazo la kutengeneza converter ya umeme kutoka chini ya 10V hadi 250V na angalau 2000W itakayokuwa portable na mfumo wa kujicharge.

Hii itakuwa ni inverter inayoweza kutumika kwa matumizi ya ndani na hata wale biashara za kuhama hama kama machinga nakadhalika pia kwa matumizi ya nyumbani unaweza ku iconnect kwenye wiring ya ndani maana itakuwa na umbo dogo mfano wa laptop.

Pia hii itakuwa msaada mkubwa kwa wapangaji wasiotaka kushare meter moja na mwenye nyumba.

Mradi huu unawezekana kwani nimejifunza vitu vingi kuhusu hii kitu nimewaza kuhusu uzalishaji wa kibiashara naona inalipa kama atapatikana mtu wa kuwekeza kwenye idea hii.
 
Mladi huu unawezekana kwani nimejifunza vitu vingi kuhusu hii kitu nimewaza kuhusu uzalishaji wa kibiasha naona inalipa kama atapatikana mtu wa kuwekeza kwenye idea hii.
Changamoto
- Vibali na leseni toka mamlaka husika.

Miradi midogo ya umeme (Small Power Projects - SPP): Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mradi wako unaweza kuangukia kwenye kundi la SPP. Kuna sheria na kanuni zinazosimamia miradi ya aina hii, ikiwemo Electricity (Development of Small Power Projects) Rules, 2019
Kama inverter yako itatumika kuzalisha umeme na kuunganishwa kwenye wiring ya ndani ya nyumba, unahitaji kufuata kanuni za usalama za umeme na kupata kibali kutoka TANESCO kabla ya kuunganisha kwenye gridi yao. Hii ni muhimu ili kuepuka matatizo ya kiufundi na kuhakikisha usalama wako na wa watumiaji wengine wa gridi ya taifa.
Anza kwa kuwasiliana na EWURA na TBS kwa maelezo zaidi kuhusu taratibu za kupata vibali na leseni zinazohitajika. Pia, wasiliana na BRELA kwa ajili ya usajili wa biashara yako.
 
Anhaaa, sawa. Ngoja nikusanye mtaji siku niwe angel investor.


Tunakuwa siriazi kabisa na timu ya watu wanaoweza kutafuta hivyo vibali na kila kitu. Na kunakuwa na wataalamu kuanzia wa afya na mainjinia na wahasibu yaani timu imekamilika kufanya uwekezaji kwa wabunifu wa ndani.


Inakuwa tu mradi huu umefadhiliwa kwa hisani ya Sahili (research & development) production and marketing.



Mradi na bidhaa zinauzwa halafu tunagawana asilimia. Kiasi kwa muwekezaji (Sahili) kiasi kwa mbunifu (wewe).


Halafu inawezekana tunazunguuuuka kumbe hela inayohitajika ikawa ya kawaida tu. Tuambie mradi unahitaji kama tsh ngapi? Je tukihitaji business plan hata ya kuanzia unaweza kushare na wadau.


Kama bado hujaandika business plan, chukua hii kama mfano uandike. Utapata wawekezaji siriazi hao ma angel investors waliopo tayari.
 
Tuambie mradi unahitaji kama tsh ngapi? Je tukihitaji business plan hata ya kuanzia unaweza kushare na wadau.
kwa mahesabu ya production moja inaweza kucost wastani wa tsh 100,000.
kwa kipindi cha mwanzo tunaweza kuanza kama wakala wa jumla na leja leja ili kukuza mtaji na kisha baadae kukata vibali kama producer kamili.
Pia tunaweza ku design vizuri kama bidhaa special zinazotoka china
 
Tengeneza Kwanza sample ndo utafute vibali, watu WA kutengeneza umeme specific wapo, kuna kipindi walijitokeza kwa umeme WA upepo sasa wewe ni umeme WA nini? Jipambanue Kwanza hapo utoe product yako.
 
Tengeneza Kwanza sample ndo utafute vibali, watu WA kutengeneza umeme specific wapo, kuna kipindi walijitokeza kwa umeme WA upepo sasa wewe ni umeme WA nini? Jipambanue Kwanza hapo utoe product yako.
Hii ni converter mkuu inayozalisha umeme wa 250V na inamfumo wa kujichaji yenyewe kwaio ni umeme usio isha mpaka kipindi cha kubadilisha battery endepo itakuwa imekufa
 
Kutoa cheap energy serikali itakuwekea kikwazo
Kwa maelezo yako nyumba nyingi hawatovuta umeme, and believe me ukifanikiwa kutengeneza hiko kifaa kitapigwa marufuku.
 
Kikubwa tu uwasiliane na mamlaka kwanza ila kwa ambavyo imezoeleka huenda ukawa ndio mwisho wako kuonekana si tu jukwaani bali hata hapa jijini😁

Welcome to Katavi national Park.
Kuna jamaa nadhani ni Zambia sijui, alitengeneza kifaa flani hakiishi umeme, una connect tv n.k, aisee alipewa sumu 😂😂😂

This is Africa...
 
Back
Top Bottom