Ukitaka kufanya kitu kwenye nchi kama Tanzania usianze kutafuta maoni au kuomba ushauri mitandaoni. Kama unajiamini komaa tafuta mwekezaji kimyakimya anza biashara. Ukitafuta maoni unakutana na watu wenye mawazo negative na ya kimaskini, mtu anakwambia utapotezwa ujikute Katavi!!???,. Kuna watu hata uwaombe ushauri gani wapo Duniani kwa ajili ya kukatisha wengine tamaa. Fanya kitu, ukifeli fanya tena, ukifeli fanya tena au jaribu kingine mpaka utafanikiwa. Ni siri ya matajiri wakubwa wote Duniani.