Njoo Kigoma nunua tangawizi mbichi kuanzia mwezi wa sita kwa Tshs 400 kwa kilo, kata kwa ajili ya kukausha mpaka mwezi wa Tisa then utaamua uuze kwa kati ya 1500/= mpaka2300/= kwa kilo au subiri mwezi wa pili uuze 3500/= kwa kilo.Huhitaji kusafirisha,leseni wala ushuru wa aina yoyote bali lorry linakufata popote ulipostore mzigo wako. Tangawizi kavu inatafutwa nyumba kwa nyumba na matajiri toka Burundi,Kenya,Rwanda na wenyeji pia wanojua masoko zaidi ndani na nje ya nchi. Wekeza hata million 40 tu utanishukuru badae utakapopata zaidi ya million mia moja ndani ya muda mfupi.Naongea kwa uzoefu mkubwa sana nikiwa eneo husika mpaka sasa na Mali bado inatafutwa kwa kasi ya ajabu sana mpaka Leo.Gharama ni turubai za kuanikia na pesa ya kuwalipa wakataj 4000/= kwa gunia la debe kumi ambalo linabeba zaidi ya kilo 150.mzigo unaletewa popote unapofanyia shughuli zako kwa gharama ya mkulima wewe kazi yako ni kusoma mzani tu. Kipindi hicho tangawizi ni ya kutosha hata ukihitaji tani 100000 unapata ndani ya siku chache tu.
Watu wanapiga pesa si kawaida huku. Fanya research then ukiridhika uamzi ni juu yako.