Wazo la biashara kwa 100m

Wazo la biashara kwa 100m

Habar ndugu. Kwanza niwie radhi kwa neno la posho ya kikao limeleta sura ya kujimwambafai na kukosa humbleness, na nimefuta tayar, umenisuta kwa akili.
Pili, naomba idea ambayo ni sustainable. Kwa vile itakuwa kwa mfumo wa kampun uwe shareholder.
Hapana wala sijakusuta mkuu ila kweli nitaimic hiyo posho. Si unajua jinsi hela ya posho ilivyo tamu. Hizo zote mbili ni sustainable na ni promising kulingana na country's growth factors.
 
Naanza kupanda maharage ekari 500 Simanjiro nategemea kuvuna magunia 1500 minimum baada ya kuhifadhi kwa cost ya 15k kwa gunia ntauza mwezi February kwa 250k kwa gunia. Gharama ya kutunza ekari moja ni 150k. Achana na kuwekeza mijini njoo uvune faida rahisi shambani. BTW Niko Dar ila nalima huko na next week naweka kambi shambani.’
ekari 500? Shubhaaaamit watu mko na vision za mbali sanaaaaa
 
Njoo Kigoma nunua tangawizi mbichi kuanzia mwezi wa sita kwa Tshs 400 kwa kilo, kata kwa ajili ya kukausha mpaka mwezi wa Tisa then utaamua uuze kwa kati ya 1500/= mpaka2300/= kwa kilo au subiri mwezi wa pili uuze 3500/= kwa kilo.Huhitaji kusafirisha,leseni wala ushuru wa aina yoyote bali lorry linakufata popote ulipostore mzigo wako. Tangawizi kavu inatafutwa nyumba kwa nyumba na matajiri toka Burundi,Kenya,Rwanda na wenyeji pia wanojua masoko zaidi ndani na nje ya nchi. Wekeza hata million 40 tu utanishukuru badae utakapopata zaidi ya million mia moja ndani ya muda mfupi.Naongea kwa uzoefu mkubwa sana nikiwa eneo husika mpaka sasa na Mali bado inatafutwa kwa kasi ya ajabu sana mpaka Leo.Gharama ni turubai za kuanikia na pesa ya kuwalipa wakataj 4000/= kwa gunia la debe kumi ambalo linabeba zaidi ya kilo 150.mzigo unaletewa popote unapofanyia shughuli zako kwa gharama ya mkulima wewe kazi yako ni kusoma mzani tu. Kipindi hicho tangawizi ni ya kutosha hata ukihitaji tani 100000 unapata ndani ya siku chache tu.
Watu wanapiga pesa si kawaida huku. Fanya research then ukiridhika uamzi ni juu yako.
Wazo zuri.
Tangawizi pia zinalimwa Madaba,Ruvuma na Same .
 
Naanza kupanda maharage ekari 500 Simanjiro nategemea kuvuna magunia 1500 minimum baada ya kuhifadhi kwa cost ya 15k kwa gunia ntauza mwezi February kwa 250k kwa gunia. Gharama ya kutunza ekari moja ni 150k. Achana na kuwekeza mijini njoo uvune faida rahisi shambani. BTW Niko Dar ila nalima huko na next week naweka kambi shambani.’
Yakigoma mwana si Kala hasara
 
Nenda Morogoro, possibly Mlimba au maeneo mengine yanayolima mchele. Nunua mchele weka stock. Ndani ya miezi kadhaa tu, possibly baada ya miezi sita, hiyo mil 100 itakuwa imegeuka na kuwa mil 300!. Kama sivyo, basi the minimum ni mil 250+
Ubarikiwe
Sio rahisi kihivyo
 
Ngoja nikushauli ujinga ukiona umekosa cha kufanya anzisha mirad ya mashine za kusaga tafuta sehem nzuri iwe kukodi chumba au kujenga kibanda ukifanikiwa kuweka sehem 4 unauhakika wa kulaza kima cha chini laki 6 kwa kila wiki hadi uzeeni kwako na hiyo ni faida tu haina makato wala ushuru

Ukiona hiyo ishu ni pusi njoo tufanye biashara ya makaa ya mawe ruvuma to mwanza au mtwara to kenya toka kukod gar kuyanunua, vibari mpaka kuyapeleka sehem husika itakugharim m2 faida yake ni kama laki nne hivi yaani we ni kupakia mzigo sokoni kutokana na speed yako na mtaji kama unauwezo wa kufikisha sokoni gar tano zenye ujazo wa tan30 basi fanya laki nne mara tano hiyo ni faida kwa siku uliyopeleka soko uhakika kama hujaelewa nitafafanua
 
Wadau wanaoamini katika ubia natafuta wazo la biashara na uwekezaji usiozid milion 100.
Nina parameters zangu
1. Mwenye wazo awe shareholder wa biashara yenyewe hata kama hana mtaji wa pesa. Akili ni mtaji mkubwa
2. Biashara iwe ya uzalishaji wa product flani na sio biashara ya kununua na kuuza
3. Uzalishaji uwe dsm hata kama malighafi inatoka popote
4. Bidhaa iwe na faida inayodhirika na sio faida mtambuka. Kuwepo na uhitaji kidogo wa kusimamiana na auditing rahisi
5. Isiwe bidhaa ya msimu wala inayoleta faida kimagumashi. Isilete mgogoro na TRA.
Wazo zuri tutaanza kikao mara moja.
Habari Mkuu;
1. Spice, Herbs and Fruits value addition/processing.
a. Extracts (Spices, herbs and fruits)
Extract maarufu kuliko zoteni Vanilla, ingawa zinaweza andaliwa nyingine nyingi kama mango, apple/cider, tamarind, pineapple, orange, lime, lemon, lemongrass, cinnamon, mint, rubber vine fruit, ginger etc. Tanzania matunda yapo mengi(moja ya marketing ideas ni ku-provide a taste of ''exotic"). Malighafi zote zipo, na vitendea kazi vyote vinapatikana hapa bongo. M
Masoko ni mtu binafsi, mama/baba ntilie, bakery zinazofunguliwa kila siku, restaurants, hotels etc.

b. Essential Oils(Spices, herbs and some fruits(parts of a fruit(s)))
Essential oils ni mafuta yatokanayo na viungo na mitishamba mbalimbali, kama ganda la chungwa, limao(lime, lemon), cinnamon, cardamom, lemongrass, mint, eucalyptus leaves, pine needle leaves, ginger, garlic, rosemary, rose(the flower), na serikali ikija kuufikiria bangi(CBD essential oil) etc.
Matumizi ni Aromatherapy, Pharmaceutical na Food&Beverage sectors.
Masoko ni watu binafsi, vituo vya massage, wellness and relaxation Spa, kama ingrident ya sabuni na perfume (Essential oil tutakayozalisha ikiwa Aromatherapy grade).
Makampuni ya dawa(kama essential oil tutakayozalisha itakuwa Pharmaceutical grade).
Makampuni ya vyakula na vinywaji(food and beverage) kama essential oil tutakayozalisha itakuwa Food grade.

c. Oleoresins( Spices and herbs)
haya ni mafuta-mgando(semi-solid) yatokanayo na uchakataji wa viungo na mitishamba. Yanasifa ya kuwa na vitu vingi zaidi ya essential oils.
matumizi yake ni mengi kuanzia utengenezaji wa mabomu ya machozi (vurugu zitokeapo, yanatumika sana kote duniani) mpaka kwenye mapishi,vinywaji, rangi za chakula na vinywaji.
Mfano ni ginger, turmeric, garlic, onion, cinnamon, cardamom etc.

NB; Kama utakuwa huru na kukubaliana na uwekezaji katika maeneo mengi tanzania, nitatoa idea nyingi zaidi.
NB: Mtaji wangu ni idea(wazo), bado sijafanikiwa pesa.
Ahsante.
 
Ngoja nikushauli ujinga ukiona umekosa cha kufanya anzisha mirad ya mashine za kusaga tafuta sehem nzuri iwe kukodi chumba au kujenga kibanda ukifanikiwa kuweka sehem 4 unauhakika wa kulaza kima cha chini laki 6 kwa kila wiki hadi uzeeni kwako na hiyo ni faida tu haina makato wala ushuru

Ukiona hiyo ishu ni pusi njoo tufanye biashara ya makaa ya mawe ruvuma to mwanza au mtwara to kenya toka kukod gar kuyanunua, vibari mpaka kuyapeleka sehem husika itakugharim m2 faida yake ni kama laki nne hivi yaani we ni kupakia mzigo sokoni kutokana na speed yako na mtaji kama unauwezo wa kufikisha sokoni gar tano zenye ujazo wa tan30 basi fanya laki nne mara tano hiyo ni faida kwa siku uliyopeleka soko uhakika kama hujaelewa nitafafanua
Makaa ya mawe ungedadavua kidogo ingependeza mkuu
 
Kiwanda kidogo cha kutengeneza trays za (box/karatasi) za mayai.
Malighafi ni mabox yaliyokwisha tumika.

Hapo kwenye hiyo 100M na "chenji" inabaki.
 
Back
Top Bottom