Wazo la kibiashara: Wekeza 280,000 kwa mwezi katika ng’ombe wa maziwa, upate hadi 930,000!

Wazo la kibiashara: Wekeza 280,000 kwa mwezi katika ng’ombe wa maziwa, upate hadi 930,000!

Umejifunza Kitu Kwenye Huu uzi?

  • Ndio

  • Hapana


Results are only viewable after voting.
Ila unakubaliana namie kuwa jamaa anataka kupiga hela kwa greed za binadamu, yaani watu wanaona hela ya fasta, unakuta yeye hata hafugi Ila anauza elimu,.maneno na uelewe kuwa words are cheaper than actions
Kawaambia hivyo na walimu wako, waliofundisha engineers, doctors e.t.c na hawajawahi kua madaktari.
N:B Tunakukaribisha shambani ujionee
 
Tatzo Elimu yetu ya Chuo inatupotosha kiasi kwamba tunachukulia Ng'ombe kama kuku. Mimi nimezaliwa katika Mazingira ya ufugaji na hakuna mfugaji anaweza tumia Hizo ghalama zako Kwa mwezi labda anayefuga kuku. ukitaka kuamini Anza hiyo Biashara ndo utajua kuwa ulikuwa sahihi wakati unapotosha umma au ulikuwa wrong
Usahihi ni upi?
 
View attachment 3286792
Hivi karibuni tulitoa andiko kwamba ukifuga ng'ombe wa maziwa mmoja tu, unaweza kupata kati ya TSh 600,000 hadi 900,000 kwa mwezi. Pia, tulieleza jinsi hii ilivyo fursa kubwa kwa watu wengi, hasa wale wanaoishi mijini.

Leo hii nakuletea mchanganuo wa gharama, mapato na faida, ili uone mwenyewe jinsi unavyoweza kuanza na kufanikiwa katika ufugaji huu.

1️⃣ Gharama za Uendeshaji kwa Mwezi
Katika maeneo ya mijini kama Dar es Salaam, gharama za kumhudumia ng'ombe mmoja wa maziwa kwa mwezi zinajumuisha:
Chakula (nyasi na virutubisho kama pumba, mashudu, na mifugo feeds) – TSh 150,000 - 300,000
Matibabu na Chanjo
– TSh 10,000 - 20,000
Maji
– TSh 20,000 - 50,000
Ulinzi na Wafanyakazi
(ikiwa unamwajiri mtu) – TSh 100,000 - 200,000
Gharama nyingine
(banda, umeme, vifaa) – TSh 10,000+

💰 Jumla ya Gharama kwa Mwezi: TSh 280,000 - 570,000

2️⃣ Makadirio ya Mapato kwa Mwezi

Ng'ombe wa maziwa mwenye ubora mzuri anaweza kutoa wastani wa lita 15 - 25 kwa siku.
Kwa bei ya maziwa ya TSh 1,700 - 2,000 kwa lita, unaweza kupata mapato yafuatayo:
15 lita x 30 siku x 1,700 = TSh 765,000 kwa mwezi
25 lita x 30 siku x 2,000 = TSh 1,500,000 kwa mwezi

💰 Jumla ya Mapato kwa Mwezi: TSh 765,000 - 1,500,000

3️⃣ Makadirio ya Faida kwa Mwezi

Faida = Mapato - Gharama
Faida Ndogo (gharama kubwa, uzalishaji mdogo):
TSh 765,000 - 280,000 = TSh 485,000
Faida Kubwa (gharama ndogo, uzalishaji mkubwa):

TSh 1,500,000 - 570,000 = TSh 930,000

🚀 Kwa ng’ombe mmoja tu wa maziwa, unaweza kutengeneza faida ya TSh 485,000 hadi 930,000 kwa mwezi!

4️⃣ Faida Nyingine za Ufugaji wa Ng’ombe wa Maziwa
Kusindika maziwa
– Badala ya kuuza maziwa ghafi, unaweza kuzalisha bidhaa kama mtindi, siagi na jibini, ambazo huuzwa kwa bei ya juu.
Mbolea ya samadi – Samadi kutoka kwa ng’ombe wako inaweza kuuzwa kwa wakulima kama mbolea bora.
Ndama wa kuuza – Ng’ombe wako ataendelea kuzaa ndama, ambao unaweza kuuza au kuongeza idadi ya mifugo wako.
Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ni biashara yenye faida kubwa na inayotoa kipato endelevu kila siku. Ukiwa na mipango mizuri na maarifa sahihi, unaweza kukuza biashara yako kwa muda mfupi!

📢 BADO HUJAJIUNGA NA GROUP LETU LA MAFUNZO? WASILIANA NASI 0764 148 221
Jiunge leo upate elimu ya kina kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na mbinu za kuongeza faida yako!

#KilimoBiashara
#UfugajiWaNgombeMaziwa
#MaziwaYanafedha
#FursaZaKilimo
#ShambaDarasa
#JifunzeNaSisi
Ng'ombe mmoja anatoa lita 15? wangeweka maji? samhani sikuwepo
 
Back
Top Bottom