Wazo la kufungua barabara ya Makambako to Mlimba

Wazo la kufungua barabara ya Makambako to Mlimba

Naunga mkono hojaa, hii barabara ijengwe haraka sanaa.
Kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa maeneo husika.
Kunamahala mkuu inabidi tupafanye papitike tu maana kuna sasa na hapo baadae, kuliko kugawanyisha mikoa bora hiyo pesa wangeboresha hizi njia za kuiunganisha hii mikoa.
 
Mimi binafsi nakubaliana na mleta mada kabisa tunapashwa kuzitengeneza njia nyingi zinazoiunganisha Nchi pande zote hiyo ndio njia mojawapo nzuri ya kuleta maendeleo ya ndani ya Nchi. Kuto kuzijenga itakuwa sawa sawa na kile wanachokipata DRC maana upande mmoja hakutani na mwingine kwa urahisi.
NI SAHIhi hii ni moja ya njia ya kukuza uchumi sio kutegemea njia moja na umuhimu wakuwa na njia nyingi umeonekana mwaka huu baada baadhi ya Barabara kukata mawasiliano kukiwa na njia nyingi inasaidi kuwa mbadala
 
Ni Muda mwafaka tanroad kuifungua Barabara ya makambako hadi mlimba kuungana na iliyotoka Ifakara kwa ni wananchi wengi kipande hichi wamekuwa wakitumia treni kama ndo usafiri wao na kwanini wafungue hii Barabara kwanza ni Barabara itakayo kuwa na km chache kama 160 ukilinganisha na ya lupembe km 224 mbili itasaidia kuwaunganisha wakazi wa ifakara mlimba nk na mikoa ya nyanda za juu kUsini iringa, Njombe ,ruvuma,mbeya ,songwe ,rukwa nk tatu itakuwa ndo njia mbadala ya kwenda dsm itapunguza msongamano tazam road ,

Itawarahisishia kutanuka kwa soko la mazao yao wananchi wa mlimba na mwisho naona juhudi zimeanza kuonekana ya kupanganfa kukifungua kipande Cha uchindile hadi mlimba na ndo kipande kilicho kuwa kimesalia hongereni tarura kwa maono hayo👇♨️♨️♨️♨️👇

Nao wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa wamekiri uboreshaji wa miundombinu katika halmshauri zao huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa kupitia TARURAna kwamba Halmashauri ya mlimba inatarajia kuchonga barabara ya Mlimba - Uchindile yenye km 80 ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kuzunguka View attachment 2972329View attachment 2972330View attachment 2972331View attachment 2972332
Mkoa wa Morogoro nafikiri Ni mkubwa sana, unapaswa kugawanywa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii hususani ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuunganisha na mikoa mingine yote inayopakana nayo.
 
Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ifakara hadi Mbingu yenye urefu wa kilomita 62.5 utatumia Bilioni 97.178

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imebainisha kuwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Henan Highway Engineering Group Co. Ltd ya kichina imepewa zabuni ya kujenga barabara ya Ifakara-Kihansi yenye urefu wa kilometa 124 sehemu ya kwanza Ifakara-Mbingu ya kilometa 62.5 kwa kiwango cha lami.

Akizungumza mara baada ya kukagua hatua zinazoendelea za kuanza ujenzi wa barabara hiyo mara baada ya mvua kubwa za El-Nino kuanza kupungua Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba amesema kuwa kilio kikubwa cha wananachi ni kupata barabara ya lami ambapo kwa sasa kimepatiwa majawabu kwa serikali ambapo tayari imetoa fedha na mkandarasi yupo eneo la mradi kwa ajiili ya ujenzi huo.

Mhandisi Kyamba amesema kuwa mradi huo utasimamiwa na kitengo cha usimamizi wa miradi cha TANROADS (TECU) na kwa sasa mkandarasi ameanza kufanya matengenezo ili barabara inayotumika sasa ianze kupitika kwani hilo ni jukumu lake kwa mujibu wa mkataba.

Ameeleza kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo za kilimo kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro pamoja na mkoa wa Njombe kupitia Ifakara, Mlimba, Kihansi hadi Makambako Mkoani Njombe.
1715858191582.jpg
1715858181724.jpg
 
Barabara HiYo imeoneshwa kwa rangi ya blue
IMG-20240709-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom