Wazo la kufungua barabara ya Makambako to Mlimba

Naunga mkono hojaa, hii barabara ijengwe haraka sanaa.
Kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa maeneo husika.
Kunamahala mkuu inabidi tupafanye papitike tu maana kuna sasa na hapo baadae, kuliko kugawanyisha mikoa bora hiyo pesa wangeboresha hizi njia za kuiunganisha hii mikoa.
 
NI SAHIhi hii ni moja ya njia ya kukuza uchumi sio kutegemea njia moja na umuhimu wakuwa na njia nyingi umeonekana mwaka huu baada baadhi ya Barabara kukata mawasiliano kukiwa na njia nyingi inasaidi kuwa mbadala
 
Mkoa wa Morogoro nafikiri Ni mkubwa sana, unapaswa kugawanywa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii hususani ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuunganisha na mikoa mingine yote inayopakana nayo.
 
Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ifakara hadi Mbingu yenye urefu wa kilomita 62.5 utatumia Bilioni 97.178

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imebainisha kuwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Henan Highway Engineering Group Co. Ltd ya kichina imepewa zabuni ya kujenga barabara ya Ifakara-Kihansi yenye urefu wa kilometa 124 sehemu ya kwanza Ifakara-Mbingu ya kilometa 62.5 kwa kiwango cha lami.

Akizungumza mara baada ya kukagua hatua zinazoendelea za kuanza ujenzi wa barabara hiyo mara baada ya mvua kubwa za El-Nino kuanza kupungua Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba amesema kuwa kilio kikubwa cha wananachi ni kupata barabara ya lami ambapo kwa sasa kimepatiwa majawabu kwa serikali ambapo tayari imetoa fedha na mkandarasi yupo eneo la mradi kwa ajiili ya ujenzi huo.

Mhandisi Kyamba amesema kuwa mradi huo utasimamiwa na kitengo cha usimamizi wa miradi cha TANROADS (TECU) na kwa sasa mkandarasi ameanza kufanya matengenezo ili barabara inayotumika sasa ianze kupitika kwani hilo ni jukumu lake kwa mujibu wa mkataba.

Ameeleza kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo za kilimo kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro pamoja na mkoa wa Njombe kupitia Ifakara, Mlimba, Kihansi hadi Makambako Mkoani Njombe.
 
Barabara HiYo imeoneshwa kwa rangi ya blue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…