Hii nchi ni ya watanzania wote, wenye elimu na wasio na elimu, wenye uwezo wajuu kiuchumi na wale wachini kabisa kiuchumi. Niwakati sasa makundi yote haya yafikiwe nakujulishwa umuhimu wa mikataba mikubwa ambayo serikali inaingia.
Kuna mtanzania mmoja juzi aliamua kutumia Uhuru wake wakujieleza kwa kutuhumu kundi la watu aliowaita masikini kulalamikia sakata la bandari.Kwamtazamo wake anaona mtu ambae hana uwezo wakuagiza bidhaa kupitia bandari hatakiwi kulalamika badala yake asubiri wenye direct interests ndo waamue uhalali au uharamu wa sakata hili.
Hayo nimawazo yake yanabaki kama yalivyo, ila kwangu naona nimuhimu wananchi tufahamishwe nini faida na hasara za mikataba ya nchi ili hata ikitokea matokeo yasiyo mazuri tuwe tayari kubeba gharama.
Kuna wakati natamani ningemuona mbunge wangu nimuulize anachokitetea/kutokitetea kuhusu huu mkataba ni msimamo wa sisi wapiga kura wake au ni msimamo wa chama chake.
Nikweli serikali inafanya maamuzi kwa niaba ya wananchi lakini(kwa maoni yangu)sio busara jambo kubwa la kitaifa kama mikataba kuamuliwa na watu wasiozidi wanne(4),huku watu zaidi ya milioni50 wakibaki hawaelewi pakusimamia.
NB:Hao watu wanne niwale saini zao zinazoonekana kwenye mikataba.