Wazo la leo wakuu!!!

1. Umia kadri ya kuumia lakini KIDONDA cha mapenzi hakifungwi bandeji.
2. Barabara nazo zina MATUTA lakini huwezi kupanda viazi.
3. Hata panga liwe KALI kiasi gani lakini haliwezi kukata kiu.
 
hata kinyozi uwe malamu kiasi gani kamwe huwezi nyoa kichwa cha habari cha gazeti
 
Maprosoo uko juu sana hhhahahah

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama umezaliwa na nyota ya mbwa, usishangae kufanya kazi ya ulinzi
 
kuna wimbo mmoja wa injili. Kaitwa baby, sweety na darling. Subiri kidogo nikutajie huo wimbo wenyewe

hapana bwana mi najua kaitwa dady na pedeshee
solomoni mukubwa ameimba kwenye nyimbo zake
 
Ukibebwa kunja miguu
piga uwa galagaza hakuna mbele wala nyuma ya mti
ukali wa nyuki ndio utamu wa asali yake
 
huwezi jenga nyumba juu ya jiwe la barafu
hakuna aliyeyashika wala kuyaona mapenzi,lakini yanaua
mkiwa wa mbuzi una kazi gani ,maana haufukuzi hata inzi
 
mwanamke hata awe baunsa kiasi gani kamwe hawezi pigana kavua sidiria
 
Hata uwe na heshina kiasi gani, huwezi kujiamkia mwenyewe
 
Wazo la siku zote.
MUNGU AKIWA DEREVA WA MAISHA YAKO KAMWE SHETANI HAWEZI KUOMBA LIFT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…