Wazo langu kuhusu mabishano yasiyoisha ya Qur'an na Biblia

Wazo langu kuhusu mabishano yasiyoisha ya Qur'an na Biblia

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Vita vya kubishania uhalali na uimara wa mistari ya kwenye hivi vitabu viwili vitakatifu imekuwa isiyo na mwisho, nimeikuta nilipozaliwa 80's na mpaka leo inaendelea. Siku za hivi karibuni na humu jf nayo imekumbwa na wimbi hilo! Katika mabishano hayo, nimegundua hayaishi leo, hayaishi kesho wala keshokutwa. Yapo haswa, yataendelea kuwepo haswaaaa. Sababu kuu ni hizi;

1. Watu hutafuta mistari ile tu yenye unafuu kwake basi, kwenye mafindofindo kidogo basi hufanya ujanja wa kuparuka au kuzungushazungusha hoja ilimradi lipite.

2. Uchambuzi huenda kiitikadi tu na si vinginevyo......hoja isiyo ya upande wake mtu ataibishia kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane hata kama itakuwa wazi kiasi gani.

3. Wapo waliojawa na chuki na kuaminishwa vibaya tu na upande fulani hivyo huingia mijadala hii kwa kebehi tu.

4. Mwenye uwezo wa kujieleza vizuri (unajua tumetofautiana uwezo wa kujieleza) basi hutawala mjadala hata kama reference yake ni dhaifu lakini asiye na kipaji huchukua muda mrefu kulielewesha jambo na hivyo mijadala kuendelea kila siku.

5. Kuna faida zinapatikana kwa baadhi ya watu kutokana na mabishano haya.....inaweza kuwa kujichekesha tu au faida ya mali kabisa. Mijadala zaidi, faida zaidi.

6. Kila siku wabishanaji huibuka na wazo tofauti la kubishana; verse iliyotafsiriwa hivi leo, inaweza ikaongezewa lile (lililokosekana jana (labda mzungumzaji hakufika huko kifikra)) kesho na hivyo kuifanya mijadala kuwa endless.

N.k

Sina shaka, kuwa mwisho wa siku Mwenyezi Mungu alidhamiria kutoa muongozo na kuyagusa, kuanzia chini kabisa, maisha ya mwanadamu ili awe na ustawi mwema kama binadamu. Kwa sababu hiyo, niwaombe, angalau kwa leo tu, tuhame katika ustadi wa kukariri vifungu hadi katika uhalisia wa vitabu hivyo huku mitaani.....yaani tuangalie ni kitabu kipi haswa kimejibu vema kabisa maisha halisi ya mwanadamu, kimemuondolea dhiki ya kuhangaika kama mnyama asiye na muongozo wowote. Naomba kwanza tujikite hapa Tanzania kwetu, tunapopafahamu A-Z. Kila mmoja wetu humu ana ujirani na mtu anayeamini katika kitabu todauti na yeye au anajua vema tu ni maeneo gani hapa tz yamekaliwa zaidi na watu wa kitabu kipi kati ya hivyo na maisha yao kwa ujumla.

Naomba pia, mjadala ujikite katika kuangalia mambo yafuatayo;

a) Mauaji
b) imani za kishirikina
c) Sintofahamu za mirathi na dhulma kwa yatima
d) Kusaidiana/ubinadamu
e) Stability ya ndoa na familia
f) Staha
g) Matunzo kwa wazazi na wazee
h) Wizi na ufujaji/kutojali mali ya umma (ubinafsi)
i) Uzinzi
j) Mazishi n.k

Kitabu cha Mungu, iwe binadamu anapiga kelele au la lazima kitatoa muongozo thabiti kuhusu hayo.....na reflection ya muongozo huo lazima ionekane kwenye jamii au mtu anayekiamini. Hebu leo tuvipime kwa hilo kwanza, karibuni waheshimiwa; tz mnaijua, Waislamu/Wakristo mnawajua na maeneo yanayokaliwa na Waislamu/Wakristo wengi pia mnayajua!!!

Angalizo: sio uzi wa kukashifiana huu....
 
Hivi vitabu vililetwa na meli; na wale wakoloni wakiwa na malengo yao., Inabidi turudi kwenye tamaduni zetu tu; hizi za warabu na wazungu tuwaaachie wao.
 
Back
Top Bottom