Wazo langu kwa hawa wazazi wenzangu linaweza kuwa na faida?

Wazo langu kwa hawa wazazi wenzangu linaweza kuwa na faida?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Kutokana na harakati za maisha za hapa na pale, nimejikuta nimezaa na wanawake mbali mbali nje ya ndoa; na kabla ya wao kuingia kwenye mahusiano walijua kabisa mimi namilikiwa na mrs Equation x.

Ila kwa kutaka kupata chata tu ya equation x iliwalazimu wao wenyewe, kwa mida yao kujibebea mimba na hatimaye watoto wakazaliwa; Hii imepelekea kuwa na mtoto (binti) nje ya ndoa mkubwa wa kidato cha sita.

Mbaya zaidi mpaka na uzee huu nilionao, kuna pisi kali bado zinakuja kujirengesha ili nao wapate uzao wangu. Lakini kwa sababu tumepewa bure, ngoja nami niwapatie chata nzuri ili nao wafurahi.

Wazo langu nililonalo kwa sasa, ni kutaka kuwaunganisha pamoja bila wao kujuana.

Kuna biashara naifikiria, ambayo itahitaji kuwa na ‘distribution centre’ kadhaa katika ukanda wa Afrika mashariki.

Nitakuwa na ‘operation manager’ ambaye atawasainisha mikataba na kampuni, pamoja na namna ya kufanya kazi kwenye hayo maeneo yatakayoainishwa. Wao watakauwa kama mawakala kwenye hizo ‘centre’; lakini akili yangu kichwani ni kwa sababu ya watoto wa equation x.

Sijajua kama watanipa hasara ama vipi, ila watapimwa na menejimenti ya kampuni.

Lakini lengo kuu, ni wao wapate pesa nami pia nipate pesa.

Wakuu, wazo langu kwa hawa wazazi wenzangu linaweza kuwa na faida?​
 
20260410_183331.jpg
 
hahaha ni sawa mkuu, ila bdo hujajib my question.

Mpaka sasa umetengeneza masingo mother wangapi?
Sasa ni muda wa kutafuta wa kizungu, nikianzia pale Ukraine pale siwezi kosa.
 
Maisha mafupi haya, ni vizuri kuacha uzao utakaoendeleza kizazi chako, sio unakuwa na mtoto mmoja, akikata moto na jina lako linapotea. Swali, kizazi cha Isaac Newton kweli kipo?
Jina lako kupotea, lazima litapotea tu.

Ni suala la muda tu.

Vilembwe wako wala hawatajua kama uli exist hapa duniani.

Jina lako litakuwa limeshafutika.

Kama ambavyo wewe leo hii, hujui jina la babu wa babu yako, Hata Jina lako wewe lita sahaulika tu kwa uzao wao ujao.
 
Jina lako kupotea, lazima litapotea tu.

Ni suala la muda tu.

Vilembwe wako wala hawatajua kama uli exist hapa duniani.

Jina lako litakuwa limeshafutika.

Kama ambavyo wewe leo hii, hujui jina la babu wa babu yako, Hata Jina lako wewe lita sahaulika tu kwa uzao wao ujao.
Kufikiri hivyo ni ubinafsi, maandiko yanasema, nendeni duniani mkazae na muongezeke.
 
Back
Top Bottom