Wazo: Serikali iruhusu kilimo cha bangi chini ya utaratibu maalumu (Bangi ni Pesa)

Mcheza Piano

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2024
Posts
562
Reaction score
1,339
Bangi ni zao lenye thamani kubwa kutokana na faida zake lukuki ukilinganisha na mimea mingine. Watu wengi wamekaririshwa upande wapili tu wa zao hili (madhara ya matumizi haramu ya bangi)

Naomba tuelewane kuwa hata petrol ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wetu lakini wapo watu ambao huitumia kama madawa ya kulevya na imewaharibu, swali; je, tuache kutumia petroli kwasababu hiyo?

Turudi kwenye bangi, kwanza bangi ni mboga tamu mno na yenye manufaa mengi mwilini (ukiitumia kama mboga tafadhali kula siku hiyo hiyo uliyopika vinginevyo utakuja kuniambia).

Pili ni zao linalotumiwa na viwanda vya dawa za binadamu kutengeneza dawa mbalimbali kwaajili ya tiba ya mwanadamu... Swali je, hivyo viwanda vinatumia bangi toka wapi? Jibu, nchi zenye watu wenye akili kama Jamaica zinalima na kuwauzia.

Tatu mbegu za bangi hutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile biskuti na bidhaa hizi hutumika sehemu nyingi tu duniani.

Kwakifupi faida za bangi ni nyingi ukilinganisha na madhara yake endapo itatumika vibaya.

Pendekezo: Wale vijana waliopelekwa Dodoma kufanya shughuli za kilimo wasimamiwe walime bangi kwa majaribio kisha tuone pato litakalo patikana, endapo fedha nyingi zitapatikana basi kila mtanzania alazimishwe kulima ekari 1 ya bangi.

Baada ya mwaka 1 mtaandaa hafla ya kitaifa ya kunishukuru japo mimi sitaki.

==========
Majarida makubwa yanasemaje?
1. Business Inside: All The Reasons Pot Is Good For You
2. Forbes: Health Benefits Of Cannabis, According To Experts
 
Madhara SIO kiafya tu hata mazingira yanaharibika kuna interval ya ulimaji Pia yaan ukifanya research utagundua KILIMO cha Bangi ni hasara kuliko faida, nakumbuka kuna mdau yeye aliwahi kuingia field akafanya HUO mchakato Ila baadae akaja kugundua kua hakua sahihi
 
Kipi kilimfanya ajue hakuwa sahihi
 
Kipi kilimfanya ajue hakuwa sahihi
Baada ya kulima kwanza ZAO la Bangi SIO km mazao mengine namaanisha kwenye upandajwi na uvunaji ushaelewa pia Bangi ukilima inasababisha Jangwa na Ukame maana lazima ufyeke MITI mingi kupata eneo la kulima kwa HIO mpaka HAPO inapelekea mabadiriko ya tabia ya NCHI sababu ya ukatajwi wa MITI kingine watu wakiegemea ZAO la Bangi na kuacha kulima mazao mengine ya Chakula maana yake tutaingia kwenye scarcity ya Chakula hivyo itatulazimu kununua Chakula kutoka NJE sababu Ardhi yetu kwa kiwango kikubwa itakua inalimwa Bangi tu yaan HAPO nimekupa summary tu Ila hasara ni nyingi kuliko faida
 
Weed help connection or we can say meditation of internal things n tc a medical too n tc part of relaxing n thinking about our plans.
 
Baada ya kulima kwanza ZAO la Bangi SIO km mazao mengine namaanisha kwenye upandajwi na uvunaji ushaelewa pia Bangi ukilima inasababisha Jangwa na Ukame maana lazima ufyeke MITI mingi kupata eneo la kulima kwa HIO mpaka HAPO inapelekea mabadiriko ya tabia ya NCHI sababu ya ukatajwi wa MITI kingine watu wakiegemea ZAO la Bangi na kuacha kulima mazao mengine ya Chakula maana yake tutaingia kwenye scarcity ya Chakula hivyo itatulazimu kununua Chakula kutoka NJE sababu Ardhi yetu kwa kiwango kikubwa itakua inalimwa Bangi tu yaan HAPO nimekupa summary tu Ila hasara ni nyingi kuliko faida
Sikubishi, lakini tuone hapa pia[emoji116][emoji116]
[emoji117] Hakuna kilimo (estate) ambacho hakitahitaji ukatwaji wa miti, unless kiwe kilimo cha kujikimu
Hivyo bangi kuhitaji eneo kubwa ni sawa tu na korosho, ufuta, kahawa n.k
[emoji117] Watu kuegemea zaidi kwenye bangi na kuacha mazao ya chakula, huenda isiwe sababu ya msingi coz hapa Tz kuna mazao mengi yenye pesa pengine kuzidi hata bangi, lakini bado watu hawaachi kilimo cha mazao ya chakula
Mfano, ufuta, vanilla, parachichi, chai, miti n.k

Pengine hoja ibaki utafiti, kwamba wataalamu wetu hawajafanya utafiti wa kutosha kujua faida za bangi over hasara

Pamoja na hayo, siungi mkono bangi kuwa freely, coz sina ushahidi wa mazuri yake
 
Bangi ni zao lenye thamani kubwa kutokana na faida zake lukuki ukilinganisha na mimea mingine. Watu wengi wamekaririshwa upande wapili tu wa zao hili (madhara ya matumizi haramu ya bangi)

Naomba tuelewane kuwa hata petrol ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wetu lakini wapo watu ambao huitumia kama madawa ya kulevya na imewaharibu, swali; je, tuache kutumia petroli kwasababu hiyo?

Turudi kwenye bangi, kwanza bangi ni mboga tamu mno na yenye manufaa mengi mwilini (ukiitumia kama mboga tafadhali kula siku hiyo hiyo uliyopika vinginevyo utakuja kuniambia).

Pili ni zao linalotumiwa na viwanda vya dawa za binadamu kutengeneza dawa mbalimbali kwaajili ya tiba ya mwanadamu... Swali je, hivyo viwanda vinatumia bangi toka wapi? Jibu, nchi zenye watu wenye akili kama Jamaica zinalima na kuwauzia.

Tatu mbegu za bangi hutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile biskuti na bidhaa hizi hutumika sehemu nyingi tu duniani.

Kwakifupi faida za bangi ni nyingi ukilinganisha na madhara yake endapo itatumika vibaya.

Pendekezo: Wale vijana waliopelekwa Dodoma kufanya shughuli za kilimo wasimamiwe walime bangi kwa majaribio kisha tuone pato litakalo patikana, endapo fedha nyingi zitapatikana basi kila mtanzania alazimishwe kulima ekari 1 ya bangi.

Baada ya mwaka 1 mtaandaa hafla ya kitaifa ya kunishukuru japo mimi sitaki.

==========
Majarida makubwa yanasemaje?
1. Business Inside: All The Reasons Pot Is Good For You
2. Forbes: Health Benefits Of Cannabis, According To Experts
Yani ni kama kumwambia nyani akulindie shamba la mahindi. Au unamwacha houseboy unamwambia akulindie binti yako wewe unasafiri. Kwa kweli tutapata vichaa wengi. Labda kazi hii yapewe makampuni siyo raia wa kawaida
 
Hakuna kilimo (estate) ambacho hakitahitaji ukatwaji wa miti, unless kiwe kilimo cha kujikimu
Hivyo bangi kuhitaji eneo kubwa ni sawa tu na korosho, ufuta, kahawa n.k
Hujaelewa ni hivi hayo unayoyataja ni mazao ya Chakula Bangi SIO ZAO la Chakula Bangi ni Mhadarati Bangi SIO Mdalasini au Tangawizi
 
Bangi ni zao lenye thamani kubwa kutokana na faida zake lukuki ukilinganisha na mimea mingine. Watu wengi wamekaririshwa upande wapili tu wa zao hili (madhara ya matumizi haramu ya bangi)

Naomba tuelewane kuwa hata petrol ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wetu lakini wapo watu ambao huitumia kama madawa ya kulevya na imewaharibu, swali; je, tuache kutumia petroli kwasababu hiyo?

Turudi kwenye bangi, kwanza bangi ni mboga tamu mno na yenye manufaa mengi mwilini (ukiitumia kama mboga tafadhali kula siku hiyo hiyo uliyopika vinginevyo utakuja kuniambia).

Pili ni zao linalotumiwa na viwanda vya dawa za binadamu kutengeneza dawa mbalimbali kwaajili ya tiba ya mwanadamu... Swali je, hivyo viwanda vinatumia bangi toka wapi? Jibu, nchi zenye watu wenye akili kama Jamaica zinalima na kuwauzia.

Tatu mbegu za bangi hutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile biskuti na bidhaa hizi hutumika sehemu nyingi tu duniani.

Kwakifupi faida za bangi ni nyingi ukilinganisha na madhara yake endapo itatumika vibaya.

Pendekezo: Wale vijana waliopelekwa Dodoma kufanya shughuli za kilimo wasimamiwe walime bangi kwa majaribio kisha tuone pato litakalo patikana, endapo fedha nyingi zitapatikana basi kila mtanzania alazimishwe kulima ekari 1 ya bangi.

Baada ya mwaka 1 mtaandaa hafla ya kitaifa ya kunishukuru japo mimi sitaki.

==========
Majarida makubwa yanasemaje?
1. Business Inside: All The Reasons Pot Is Good For You
2. Forbes: Health Benefits Of Cannabis, According To Experts
Isafirishwe chini ya ulonzi wa jeshi kama uranium inavyopewa escort,ilimwe ndani ya mbuga ya Serengeti,Mikumi,Nyerere na mbuga zote kwa usimamizi maalumu,tunaona serikali inavyoteseka kuhudumia watumishi na mengineyo Bora tuanze na bangi Baadae itapelekwa level ya jeshi pekee tuone kama pesa itaingia sababu Dhahabu imechemsha ,Gesi hola,almasi hola,tunaona makorokocho Ripoti ya CAG na hakuna la maana lolote,watu wanaishia kwa kiwango cha chini ,ingawa silaumu mtu ila tuchukue hatua sahihi.Parachichi pia halina SOKO,mahindi yanaharibika na hatuoni kitu,tunataka mipango kuelekea uchumi wa kati,china wanakuza uchumi kwa kutuuzia mavitu feki na makamali kila pahala,mifugo imechemsha,tazama imechemsha,mikopo kila siku kwanini tusitafute majibu muafaka.
 
Watu kuegemea zaidi kwenye bangi na kuacha mazao ya chakula, huenda isiwe sababu ya msingi coz hapa Tz kuna mazao mengi yenye pesa pengine kuzidi hata bangi, lakini bado watu hawaachi kilimo cha mazao ya chakula
Mfano, ufuta, vanilla, parachichi, chai, miti n.k
Sababu ya Msingi IPO sababu ili upate magunia mengi ya Bangi utahitaji hekari nyingi za kulima Bangi yaani let say ukitaka magumuni 5000 utahitaji hekari za kutosha za Ardhi, kingine usichoelewa Bangi bei yake ni nzuri Pamba, Mbaazi na Korongo zinasubiria KILO 1 ya Bangi bei yake IPO Juu kupita hayo mazao na mazao mengine yote unayojua yanauzwa bei Juu, sasa TATIZO linakuja Wapi? Let say tusema KILO 1 ya Bangi Mimi nitakuja nakwambia nainunua kwa 10,000, ushaelewa HUKU korosho KILO 1 inauzwa 2500 Pamba KILO 1 inauzwa 3000 Mbaazi KILO 1 inauzwa 2300 let say, Wewe kwa mawazo yako unafikiri watu watakimbilia kulima Nini km SIO Bangi? NCHI nzima watu watalima Bangi na HAPO ndipo tatizo linapokuja kuonekana
 
Pengine hoja ibaki utafiti, kwamba wataalamu wetu hawajafanya utafiti wa kutosha kujua faida za bangi over hasara

Pamoja na hayo, siungi mkono bangi kuwa freely, coz sina ushahidi wa mazuri yake
Ndio nimekueleza baadhi ya hasara zake kuliko faida mfano MTU kaja anakwambia anataka TAN 500 za Bangi unafikiri ni MITI kiasi gani itakatwa ili watu walime Bangi? HUONI km tutakua tunajitengenezea Jangwa na kuukaribisha Ukame wenyewe?
 
Labda ilimwe Zanzibar maana watu wa kule sio wadokozi na hawatumii bhangi. Imagine huku bara Kuna shamba la serikali la bhangi maeneo ya Tarime au Arusha, si itabidi tuongeze magereza.
 
Isafirishwe chini ya ulonzi wa jeshi kama uranium inavyopewa escort,ilimwe ndani ya mbuga ya Serengeti,Mikumi,Nyerere na mbuga zote kwa usimamizi maalumu,tunaona serikali inavyoteseka kuhudumia watumishi na mengineyo Bora tuanze na bangi Baadae itapelekwa level ya jeshi pekee tuone kama pesa itaingia sababu Dhahabu imechemsha ,Gesi hola,almasi hola,tunaona makorokocho Ripoti ya CAG na hakuna la maana lolote,watu wanaishia kwa kiwango cha chini ,ingawa silaumu mtu ila tuchukue hatua sahihi.Parachichi pia halina SOKO,mahindi yanaharibika na hatuoni kitu,tunataka mipango kuelekea uchumi wa kati,china wanakuza uchumi kwa kutuuzia mavitu feki na makamali kila pahala,mifugo imechemsha,tazama imechemsha,mikopo kila siku kwanini tusitafute majibu muafaka.
Wazo bora sana mkuu
 
Labda ilimwe Zanzibar maana watu wa kule sio wadokozi na hawatumii bhangi. Imagine huku bara Kuna shamba la serikali la bhangi maeneo ya Tarime au Arusha, si itabidi tuongeze magereza.
Hahahaaaa, watazoea tu mkuu
 
Ndio nimekueleza baadhi ya hasara zake kuliko faida mfano MTU kaja anakwambia anataka TAN 500 za Bangi unafikiri ni MITI kiasi gani itakatwa ili watu walime Bangi? HUONI km tutakua tunajitengenezea Jangwa na kuukaribisha Ukame wenyewe?
Yapo mashamba mengi yanalima mazao yasiyo na tija yanayotesa wakulima kama katani, hayo ni kufyeka na kupanda bangi
 
Back
Top Bottom