Wazo: Tanzania Ishirikiane na Cuba kwenye Suala la Chanjo

Linapokuja suala la chanjo tunaangalia nini ?
  1. Urafiki
  2. Ufanisi
  3. Uchumi
  4. Au
Binafsi chanjo yoyote ambayo ipo efficient hata akija nayo Lucifer its okay..., Pili kwa Corona sababu inabadilika sana sioni kama chanjo ndio mwarobaini pekee..., pia Chombo kitakachoamua ipi ina ufanisi ni WHO sababu wewe unaweza ukatumia hio Abdalla, Juma au Massanja.., kweli huenda ikakupa chanjo ila ukitaka kwenda Dubai kutembea sababu hawamtambui huyo Abdalla ukawa unatwanga maji kwenye Kinu...

In short binadamu tumekuwa wapuuzi sana badala ya kushirikiana kupambana na mazingira, tunatengana na kutafuta maadui katika binadamu wenzetu... (kumbe maadui wa kweli Virus na Bakteria wanafanya yao)
 
Kwenye mambo kama haya ndipo inapaswa wataalam waoneshe uzalendo wao.

Huko Kwa wenzetu Kila mtu anajitahidi kutengeneza chanjo yake Kwa ajili ya usalama wa Raia wake.

Sisi Kwa umaskini wetu tumtegemee sana Mungu.
 
Mojawapo ya mijadala mikubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi nyingine ni suala hili la chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Nchi mbalimbali zimejaribu na zile tajiri zimefanikiwa kwa haraka kujitengenezea chanjo zao na kujinufaisha wao wenyewe kwanza kabla ya wengine. Cuba ni miongoni mwa nchi zinazojitegemea kwa kiasi kikubwa sana linapokuja suala la afya na utaalamu wa tiba.

Kujitegemea huku kumeifanya Cuba kuwa miongoni mwa taifa yaliyofanikiwa sana linapokuja suala la tiba na afya. Kwenye suala la corona Cuba iliamua kutumia uwezo wake wa ndani wa kupambana na gonjwa hili na hili limekuwa kweli pia katika chanjo.

Nimefuatilia toka mwanzo walipoanza kutanganza kuwa wanatengeneza chanjo yao wenyewe Soberana 2. Serikali yao imetangaza jana kuwa tayari chanzo yao inaenda kufanyiwa majaribio ili kupima usalama wake na uwezo wake (safety and efficacy) katika kupambana na virusi vya corona. Wamesema wanaenda kujaribu kati ya watu wenye umri wa miaka 2-18. Ikumbukwe hii chanjo ni kwa ajili ya vijana na watoto. Kwa watu wazima Cuba inatumia chanjo iitwayo Abdala ambayo inaonesha mafanikio ya karibu asilimia 92 (inakaribiana na zile za Pfizer, Moderna na Astrazeneca na hata Sputnik ya Warusi.

Kutokana na ushirikiano wetu na udugu wa kihistoria kati ya Tanzania na Cuba; serikali ione jinsi gani inaweza kuzungumza na Cuba kuruhusu majaribio ya chanjo yao na endapo inafanya kazi ipasavyo kutumia njia hiyo badala ya kutumia njia ya COVAX na mitego mingine ambayo inaacha maswali kama ni suala la afya au ni mtaji fulani.

Kama tuna lengo la kuwalinda Watanzania tuone namna ya rahisi na salama zaidi kwa kushirikiana na Cuba. Na nina uhakika Cuba hawatochukua muda mrefu kushirikiana naasi hata kuzalisha chanjo hiyo hapa hapa nyumbani na kuwa namna ya kusaidia chanjo kwa bara letu badala ya kuwasubiri wakubwa watuamulie.

Ni wazo tu. Hakuna kujitegemea kwa maana zaidi kama kule kwa mawazo. Vinginevyo, wakubwa hawa watatubana na hatutajua nini... si tuna msemo "rafiki wakati wa shida..." Ninajua kuna masuala ya vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa na wakubwa uhusiana na Cuba... tuna uthubutu wa kushirikiana nao licha ya vikwazo?

Habari zaidi:

Mwanakijiji kama hiyo chanjo ya iitwayo Abdala ina asilimia 92 na unasema (inakaribiana na zile za Pfizer, Moderna na Astrazeneca na hata Sputnik ya Warusi) kwa hiyo bado haijazifikia hizo kiubora why nchi iopt kuchukua kitu cha chini kiubora wakati vyenye ubora vipo tayari? kisa urafiki ndo tuache kuchukua vie vilivyo bora zaidi?

Why Tanzania iwe sehemu ya majaribio maana unasema

"Kutokana na ushirikiano wetu na udugu wa kihistoria kati ya Tanzania na Cuba; serikali ione jinsi gani inaweza kuzungumza na Cuba kuruhusu majaribio ya chanjo yao na endapo inafanya kazi ipasavyo kutumia njia hiyo badala ya kutumia njia ya COVAX na mitego mingine ambayo inaacha maswali kama ni suala la afya au ni mtaji fulani."

Hivi ikitokea hayo majiribio yakiwa na athari kwa watanzania nani atawajibika?

Then unasema
"Kama tuna lengo la kuwalinda Watanzania tuone namna ya rahisi na salama zaidi kwa kushirikiana na Cuba". Mwanakijiji una uhakika/uthibitisho gani kuwa ni salama zaidi kushirikiana na Cuba.
 
Nazani wao ndio wanatutegemea zaidi, ila sisi uwezo wetu wa kufikiri ndio una shida!! maana karibu kila kitu wanakitoa kwetu!!
Huo uwezo wa kufikiri ndio asset kubwa zaidi kuliko madini, mbuga, gesi, mafuta et al.. Bila kuwa Sawa mfukoni na tumboni huwezi kujisimamia kwa chochote.

Na ili uwe Sawa tumboni na mfukoni lazima uwe vizuri kichwani. Kabla ya kutaka kuparurana na hao majamaa tujitahidi kujikwamua kwanza kutoka kwenye matatizo yetu.

Tunapoelekea huko utakuta kila chanjo unadungwa tu maana hutaweza kufanya movement yoyote bila kupigwa chanjo.
 
Chanjo ya nini wakati tuna mashine ya kujifukiza na chupa za madagaska ?, Bado tuna tangawizi, malimau , vitunguu maji na pili pili kichaa...tukomae na vilivyopo au kipindi kile tulikuwa tunadanganyana ?
 
Wazo zuri,

Lakini ukifuatilia mienendo na kauli za serikali ya JMT, ni kama tayari imeshajiweka kwenye targets za 'mabeberu'.

Wameanzia mbaaaali kuwalainisha wananchi kwa kauli na vitendo kadha wa kadha ikiwemo kuunda kamati/jopo la 'wataalamu' (wale ni washauri tu)
Kwani tunashindana na mabeberu ?

Kwanini masikini tunapenda sana kujipa umuhimu usiostahili ?

Tanzania ni kinchi ambacho watu hawajui hata kiko upande upi wa dunia eti tunahisi tunafanyiwa figisu.

Hebu tupunguze kujishuku, hakuna mwenye time na sisi.
 
Mojawapo ya mijadala mikubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi nyingine ni suala hili la chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Nchi mbalimbali zimejaribu na zile tajiri zimefanikiwa kwa haraka kujitengenezea chanjo zao na kujinufaisha wao wenyewe kwanza kabla ya wengine. Cuba ni miongoni mwa nchi zinazojitegemea kwa kiasi kikubwa sana linapokuja suala la afya na utaalamu wa tiba.

Kujitegemea huku kumeifanya Cuba kuwa miongoni mwa taifa yaliyofanikiwa sana linapokuja suala la tiba na afya. Kwenye suala la corona Cuba iliamua kutumia uwezo wake wa ndani wa kupambana na gonjwa hili na hili limekuwa kweli pia katika chanjo.

Nimefuatilia toka mwanzo walipoanza kutanganza kuwa wanatengeneza chanjo yao wenyewe Soberana 2. Serikali yao imetangaza jana kuwa tayari chanzo yao inaenda kufanyiwa majaribio ili kupima usalama wake na uwezo wake (safety and efficacy) katika kupambana na virusi vya corona. Wamesema wanaenda kujaribu kati ya watu wenye umri wa miaka 2-18. Ikumbukwe hii chanjo ni kwa ajili ya vijana na watoto. Kwa watu wazima Cuba inatumia chanjo iitwayo Abdala ambayo inaonesha mafanikio ya karibu asilimia 92 (inakaribiana na zile za Pfizer, Moderna na Astrazeneca na hata Sputnik ya Warusi.

Kutokana na ushirikiano wetu na udugu wa kihistoria kati ya Tanzania na Cuba; serikali ione jinsi gani inaweza kuzungumza na Cuba kuruhusu majaribio ya chanjo yao na endapo inafanya kazi ipasavyo kutumia njia hiyo badala ya kutumia njia ya COVAX na mitego mingine ambayo inaacha maswali kama ni suala la afya au ni mtaji fulani.

Kama tuna lengo la kuwalinda Watanzania tuone namna ya rahisi na salama zaidi kwa kushirikiana na Cuba. Na nina uhakika Cuba hawatochukua muda mrefu kushirikiana naasi hata kuzalisha chanjo hiyo hapa hapa nyumbani na kuwa namna ya kusaidia chanjo kwa bara letu badala ya kuwasubiri wakubwa watuamulie.

Ni wazo tu. Hakuna kujitegemea kwa maana zaidi kama kule kwa mawazo. Vinginevyo, wakubwa hawa watatubana na hatutajua nini... si tuna msemo "rafiki wakati wa shida..." Ninajua kuna masuala ya vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa na wakubwa uhusiana na Cuba... tuna uthubutu wa kushirikiana nao licha ya vikwazo?

Habari zaidi:

Naunga mkono hoja
 
Hivyo hivyo tulishirikiana na Madagascar kina Kabudi wakateketeza mafuta kufuata coca cola ..

Mwisho wa siku kesi za ugonjwa ziliwaelemea na ile coca cola hatujui iliishia wapi maana tuliambiwa ilienda kufanyiwa tafiti
 
Na yule ambaye tunaona anamahusiano na sisi ya kihistoria.

NIMRI kipindi cha mwendazake walituambia wanaandaa chanjo. Sijui imefikia wapi.

Vyuo vyetu vya tiba ni kama vimelala tu.
Kwenye mambo kama haya ndipo inapaswa wataalam waoneshe uzalendo wao.

Huko Kwa wenzetu Kila mtu anajitahidi kutengeneza chanjo yake Kwa ajili ya usalama wa Raia wake.

Sisi Kwa umaskini wetu tumtegemee sana Mungu.
 
Na yule ambaye tunaona anamahusiano na sisi ya kihistoria.

NIMRI kipindi cha mwendazake walituambia wanaandaa chanjo. Sijui imefikia wapi.

Vyuo vyetu vya tiba ni kama vimelala tu.
Tafiti ni pesa, sasa budget ya serikali kwenye mambo ya tafiti ni kiasi gani ?

Tafiti nyingi nchi hii ninavyojua ni ufadhili kutoka kwa hao hao mabeberu msiowaamini.
 
Hiyo chanjo ya Cuba (Abdala) haijathibitishwa na WHO. Hivyo hata ukichanjwa huwezi kuhesabika kama umepata chanjo. Pia hata hizo chanjo common 3 zinazotambulika Kuna ambazo zimepigwa pini kwa baadhi ya nchi. Haswa chanjo zinazotengenezwa India zimeanza kufanyiwa figisu.

Politics vaccination. Ukweli mchungu ni kwamba, hatuwezi kuwapiga "denge" itafika Mahali tu njia zitakutana na tutatii.
Nakubaliana nawe. WHO ndiyo benchmark ya mambo yote yahusuyo afya duniani. Kinyume na hapo tutakwama. Tuagize chanjo zilizoidhinishwa na WHO.
 
Tafiti ni pesa, sasa budget ya serikali kwenye mambo ya tafiti ni kiasi gani ?

Tafiti nyingi nchi hii ninavyojua ni ufadhili kutoka kwa hao hao mabeberu msiowaamini.
Ila wasomi wetu ni wavivu tu,

Hakuna ambaye anajituma kabisa na kujitoa kufanya lolote lenye tija zaidi sana ya kukariri na kupata A hakuna ambaye kaonesha tija ya elimu yake.
 
Tunatakiwa kuachana na mawazo ya kijamaa-jamaa eti ndugu wa kihistoria na kupenda vya bwerere. Kubwa zima kutaka kudoea Chanjo ya mtoto, kusingizia urafiki wa kihistoria.

Ni bora kuenda na hizi chanjo za 'mabeberu' kwa sababu zipo sokoni kwa muda kidogo kuliko za Cuba hivyo tumeweza jua vizuri madhara yake na ufanyaji wao kazi kuliko kurukia kitu kigeni kabisa. Mambo mengine ya kusema mitego nk ni paranoia zisizo na mashiko.

Huyu mzee mwenzangu simuelewi siku hizi. Yeye mwenyewe alikimbilia mbele kutafuta maisha..mbona hakwenda Havana au Moscow? yupo kwa Trump...?

duh za kuambiwa changanya na zako!
 
..sasa Mzee Mwanakijiji unataka Watanzania tufanyiwe MAJARIBIO na chanjo za Wacuba?

..wananchi hatuamini kwamba kuna Corona, unadhani ni kazi rahisi kutushawishi tufanyiwe majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo?
 
Hivi mfano, Africa ikaagiza chanjo kutoka India. halafu wao si hawaitambui chanjo ya mhindi, nasi useme. Umoja wa ulaya hakuna kuingia Africa, hawatalegeza masharti?
Ni sawa na kusema:

Hivi kwa mfano RC wa Dar awaambie watu wa Mwandiga, wasipofua nguo kwa sabuni ya omo, mbuni au foma, ni marufuku kuingia Dar; nao watu wa Mwandiga wakachukua majani pori ya kufulia nguo toka Nakapanya, halafu wakasema, ni marufuku watu wa Dar kwenda Mwandiga, watu Dar hawatalegeza masharti?
 
..sasa Mzee Mwanakijiji unataka Watanzania tufanyiwe MAJARIBIO na chanjo za Wacuba?

..wananchi hatuamini kwamba kuna Corona, unadhani ni kazi rahisi kutushawishi tufanyiwe majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo?
Sasa chango mnajuaje zinafanya kazi ni lazima zifanyiwe majaribio...mnataka watanzania wapewe tu...wengine wajaribiwe ili sisi tunufaike...wanasayansi wetu hawashiriki katika lolote? Ubaya wa Sísi kuwa sehemu ya majaribio upo wapi?
 
Nazani wao ndio wanatutegemea zaidi, ila sisi uwezo wetu wa kufikiri ndio una shida!! maana karibu kila kitu wanakitoa kwetu!!
Ndugu yangu, una uelewa mzuri kwenye mambo haya? Kwa mfano, ebu tutajie hata vitu vichache wanavyovitoa kwetu ambavyo tukizuia watajutia?
 
Sasa chango mnajuaje zinafanya kazi ni lazima zifanyiwe majaribio...mnataka watanzania wapewe tu...wengine wajaribiwe ili sisi tunufaike...wanasayansi wetu hawashiriki katika lolote? Ubaya wa Sísi kuwa sehemu ya majaribio upo wapi?

..Ndio.

..Ndivyo " Magulification " inavyotuelekeza.

..Kama kuna eneo Magufuli ameacha " legacy " basi ni ktk suala zima la ugonjwa uviko-19.

..Siyo kwamba hatutaki chanjo zao, hata mabarakoa yao hatuyataki.
 
Mojawapo ya mijadala mikubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi nyingine ni suala hili la chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Nchi mbalimbali zimejaribu na zile tajiri zimefanikiwa kwa haraka kujitengenezea chanjo zao na kujinufaisha wao wenyewe kwanza kabla ya wengine. Cuba ni miongoni mwa nchi zinazojitegemea kwa kiasi kikubwa sana linapokuja suala la afya na utaalamu wa tiba.

Kujitegemea huku kumeifanya Cuba kuwa miongoni mwa taifa yaliyofanikiwa sana linapokuja suala la tiba na afya. Kwenye suala la corona Cuba iliamua kutumia uwezo wake wa ndani wa kupambana na gonjwa hili na hili limekuwa kweli pia katika chanjo.

Nimefuatilia toka mwanzo walipoanza kutanganza kuwa wanatengeneza chanjo yao wenyewe Soberana 2. Serikali yao imetangaza jana kuwa tayari chanzo yao inaenda kufanyiwa majaribio ili kupima usalama wake na uwezo wake (safety and efficacy) katika kupambana na virusi vya corona. Wamesema wanaenda kujaribu kati ya watu wenye umri wa miaka 2-18. Ikumbukwe hii chanjo ni kwa ajili ya vijana na watoto. Kwa watu wazima Cuba inatumia chanjo iitwayo Abdala ambayo inaonesha mafanikio ya karibu asilimia 92 (inakaribiana na zile za Pfizer, Moderna na Astrazeneca na hata Sputnik ya Warusi.

Kutokana na ushirikiano wetu na udugu wa kihistoria kati ya Tanzania na Cuba; serikali ione jinsi gani inaweza kuzungumza na Cuba kuruhusu majaribio ya chanjo yao na endapo inafanya kazi ipasavyo kutumia njia hiyo badala ya kutumia njia ya COVAX na mitego mingine ambayo inaacha maswali kama ni suala la afya au ni mtaji fulani.

Kama tuna lengo la kuwalinda Watanzania tuone namna ya rahisi na salama zaidi kwa kushirikiana na Cuba. Na nina uhakika Cuba hawatochukua muda mrefu kushirikiana naasi hata kuzalisha chanjo hiyo hapa hapa nyumbani na kuwa namna ya kusaidia chanjo kwa bara letu badala ya kuwasubiri wakubwa watuamulie.

Ni wazo tu. Hakuna kujitegemea kwa maana zaidi kama kule kwa mawazo. Vinginevyo, wakubwa hawa watatubana na hatutajua nini... si tuna msemo "rafiki wakati wa shida..." Ninajua kuna masuala ya vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa na wakubwa uhusiana na Cuba... tuna uthubutu wa kushirikiana nao licha ya vikwazo?

Habari zaidi:

Chanjo si hiari?

Wanaosubiri ya Cuba au nyungu wengine inatuhusu nini?
 
Back
Top Bottom