Wazo: Tanzania Ishirikiane na Cuba kwenye Suala la Chanjo

Pesa ndio sabuni ya roho. I hope something like this could be taken into consideration. Siamini kabisa chanjo za hawa wengine when it comes to Africa

Si wewe tu hata JPM hakuiamini chanjo kabisa.
 
Ila wasomi wetu ni wavivu tu,

Hakuna ambaye anajituma kabisa na kujitoa kufanya lolote lenye tija zaidi sana ya kukariri na kupata A hakuna ambaye kaonesha tija ya elimu yake.
Njaa na majukumu.

Utajitumaje kufanya tafiti wakati hata kula tu ni shida.
 
 
Napenda kufahamu, je huyu virus wa corona hana ubavu wa kuupenya mwili wa binadamu kupitia kwenye masikio na macho?
Na kama haiwezekani kitaaamu ni kwa msingi upi?
Isije kufunika pua na mdomo ni biashara tu wakati macho na masikio ni vitega uchumi wa biashara hii.

Comments waungwana:
 
Wenzio wameshaanza mchakato wa kuchukua pesa kwa mabeberu ww unawaletea mpango wa kushirikiana na wajamaaa 😂😂😂😂
Hakuna nchi maskini inanunua chanjo,kuna covax,kapu la pamoja la chanjo chini ya who na bilateral agreement kama mtoa mada anavyoshauri.

Tena saizi Wazungu wanataka watoe hatimiliki kwa Nchi 10 za Afrika zizalishe chanjo kwa niaba ya nchi za Afrika,shida ni je teknolojia,utaalamu na pesa za kuwekeza zipo?
 
Pamoja na kuvaa barakoa huruhusiwi kushika na uso, sasa watu wakishavaa barakoa hujisahau kuhusu kutoshika uso.
 
Naunga mkono hoja.
Tatizo ni kwamba watoa pesa ni mababeru, hawawezi kukubali watupe pesa zao halafu tuzipeleke Cuba. Wao watataka pesa zirudi huko huko kwao kwenye makampuni yao, sisi tubaki na madeni ya kuwarithisha wajukuu wetu!
 
Nakubaliana na hoja concerning Vaccine ya Cuba (aka Abdala)hawa jamaa wapo vizuri for ages kuhusu issues za Tina, tatizo ni kwamba WHO wameikubali? Kwa sababu hawa jamaa kama hawajai certify ni tatizo unaweza ukaipata hiyo Vaccine lakini usitambulike kama umechanjwa.
 
Ina maana hatuwaamini wa China na Urusi?
 



Sayansi haina undungu Mwanakijiji! kabla ya matumizi jopo ya kimataifa kama dawa nyingine lipitie data zote na kuhakiki majaribio kabla ya kuweka siasa kwenye afya za watu. Tuanze na chanjo ambazo zimeshatumika mfano hapa US wameshachanja watu zaidi ya milioni 170 hivyo tumeona chanjo ziko poa sasa kudandia chanjo kwasababu ya urafiki ya Nyerere na Castro wakati wa miaka ya 1960's sio sera nzuri ya kiafya. Ningeshauri Abdala waanze kuchanja wabunge na watoto zao kwanza na viongozi wa serikali kabla ya kuwapa watu wengine
 
Mzee Mwanakijiji ,

..umekosea kuleta hoja inayohusu ugonjwa wa corona.

..masuala yote yanayohusu ugonjwa huo yameingiliwa na SIASA.

..naamini ungeleta hoja inayohusu Tz kushirikiana na Cuba ktk utafiti wa madawa ktk ujumla wake ungepata muitikio mzuri zaidi.

..Cuba wako vizuri sana ktk utafiti wa madawa kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

..Nashauri serikali yetu iangalie uwezekano wa kuanzisha mahusiano ya kiutaalamu kati ya taasisi za utafiti wa madawa za Tz na zile za Cuba.

..Hapo chini kuna habari ya Cuba na Marekani kushirikiana ktk utafiti wa tiba ya maradhi ya Kansa.


 
Naongezea tu..Sasa urafiki wa nini kama huwezi kushirikiana na rafiki yako kukabiliana na janga linalokukabili?
 
Mama utamsikia 'tony blair was here'. Juhudi zote za kujitegemea kuhusu covid 19 kaweka kapuni kazi kushabikia wazungu kuongeza urefu kamba yake ya mbuzi ale urefu mkubwa.
Tungekua bado na jpm bila shaka ushirikiano na cuba ungetufungua macho kuhusu hilo gonjwa mabeberu wamelibeba kama mbeleko kuwanyonya nchi changa.
 
Magufuli kwanza alikuwa hakubali kuwa Covid ipo, alisema iliondolewa kwa maombi, sasa Cuba hawaamini huo upuuzi
 
Siyo kweli. Alikubali ipo, ndiyo maana akahimiza watu wajishonee barakoa.
===
Hivi wazo la mleta mada lilipewa kipaumbele na viongozi wa nchi hii?
Magufuli hajawahi kuhimiza watu kuvaa barakoa, wala hajawahi kuvaa barakoa

Kwenye vikao vyake Ikulu ilikuwa marufuku kuvaa barakoa, pia alikejeli viongozi wa dini waliokuwa wakihimiza watu kujihadhari na kusema kuwa hawana imani na kuwa Mungu ameondoa Covid Tanzania
 
Hivi, Mkuu, kwa nini unaona raha sana kusema uongo mbele ya jamii? Sasa teknolojia inakuumbua. Baki na aibu yako kwa sasa baada ya kumaliza kutazama clip hii hapa chini.
===
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…