Wazoefu nipeni ushauri. Shati la kitenge limeleta utata huku

Wazoefu nipeni ushauri. Shati la kitenge limeleta utata huku

Mr mgeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,222
Reaction score
805
Ni mchumba bado sijamuoa sasa basi, kuna sherehe tumealikwa inabidi niende naye sasa ananilazimisha nivae sare na yeye. anishonea shati la kitenge

Sasa wadau hii ishu siielewi nimekataa kanuna mbaya?

Wazoefu wa kupigilia sare za vitenge nipeni uzoefu kwa mke nahisi ni sahihi lakini kwa mchumba kwangu bado ni utata.
 
Mkuu hapo tatizo liko kwako iwapo unaamini huyo mchumba sio wa kuoa au unahisi hupendezi na hicho kitenge au hujiamini na huyo mchumba, tofauti na hivyo hiyo hali ni kawaida sana kwa wapenzi wenye kuaminiana kwa maana kia mtu atapenda kuweka himaya yake wazi na ifahamike nani mmiliki wake. Mkuu tupia hicho kitenge na umsifie amependeza alaf enjoy moment ndo ubavu wako huo mkuu.
 
Kuna kauli nilisikia mahala" ukiona wapenz wamevaa sare iliyoshonwa kwa vitenge,kaa ukijua hapo mwanaume anaburuzwa!!".
Umenikumbusha mbali mkuu, kuna jamaa mmoja (classmate) wangu tumepiga nae chuo, alikuwa na manzi wake yan alikuwa akija kwa msela (kutoka mkoani) anakuja ameshona sare za vitenge na bwana ake, asiee huyo jamaa alikuwa hahemi kwa dem wake, boom likiingia lote dem ndo anamiliki ATM card, jamaa alitoka chuo weupe hana hata mia.na walishaachana mpaka.sasa.
 
Ni mchumba bado sijamuoa sasa basi,kuna sherehe tumealikwa inabidi niende nae sasa ananilazimisha Nivae sare na yeye .
kanishonea shati la kitenge .
Sasa wadau hii ishu siielewi nimekataa kanuna mbaya.
Wazoefu wa kupigilia sare za vitenge nipeni uzoefu kwa mke nahisi ni sahihi lakini kwa mchumba kwangu bado ni utata.
Mkuu usikubali upuuzi huo,
,wanawake wanaanzaga hivyo,,
kesho atakwambiya uvae visandle vya manyoya..
 
Umenikumbusha mbali mkuu, kuna jamaa mmoja (classmate) wangu tumepiga nae chuo, alikuwa na manzi wake yan alikuwa akija kwa msela (kutoka mkoani) anakuja ameshona sare za vitenge na bwana ake, asiee huyo jamaa alikuwa hahemi kwa dem wake, boom likiingia lote dem ndo anamiliki ATM card, jamaa alitoka chuo weupe hana hata mia.na walishaachana mpaka.sasa.
Nimejifunza kitu
 
Ni mchumba bado sijamuoa sasa basi,kuna sherehe tumealikwa inabidi niende nae sasa ananilazimisha Nivae sare na yeye .
kanishonea shati la kitenge .
Sasa wadau hii ishu siielewi nimekataa kanuna mbaya.
Wazoefu wa kupigilia sare za vitenge nipeni uzoefu kwa mke nahisi ni sahihi lakini kwa mchumba kwangu bado ni utata.
Nilikuwa sijui haya Mambo ya dare ya vitenge Yana maana gani. Mchepuko wangu ulikomaa kinoma tushone Sare Sare, ila Mimi sio muumini wa hizi swaga. So, nikakataa. Kumbe ningeshona Tu, ingekula kwangu Kwa mother house. Shati la kitenge Kwa mwanaume kumbe halivaliwi hovyohovyo.
 
Kubaliana yaishe, vaa tu hakuna tatizo kawaida ya mapenzi kuridhishana nawe mridhishe, wapuuze kwa muda wanaosema unabuluzwa🤣🤣🤣🤣 kwani ukibuluzwa siku moja Kuna shida😂😂😂😂..palilia penzi mkuu.
 
Back
Top Bottom