Wazoefu nipeni ushauri. Shati la kitenge limeleta utata huku

Wazoefu nipeni ushauri. Shati la kitenge limeleta utata huku

Nilikuwa sijui haya Mambo ya dare ya vitenge Yana maana gani. Mchepuko wangu ulikomaa kinoma tushone Sare Sare, ila Mimi sio muumini wa hizi swaga. So, nikakataa. Kumbe ningeshona Tu, ingekula kwangu Kwa mother house. Shati la kitenge Kwa mwanaume kumbe halivaliwi hovyohovyo.
Ndio hivyo mkuu ,tumejifunza
 
Usivae kama huyo siyo chaguo lako, kuvaa share ina kubwa kwenye mahusiano, haivalini tu ili mradi mpendeze bali unaijulisha jamii inayowazunguka kwamba nyinyi mapenzi yenu ni kitu kimoja
 
Hakuna kitu nisichokipenda kama kuvaa na mpenz wangu shati la kitenge
 
Kubaliana yaishe, vaa tu hakuna tatizo kawaida ya mapenzi kuridhishana nawe mridhishe, wapuuze kwa muda wanaosema unabuluzwa🤣🤣🤣🤣 kwani ukibuluzwa siku moja Kuna shida😂😂😂😂..palilia penzi mkuu.
Jamaa anawaza atawezaje kuomba namba za simu za visu vikali kwenye sherehe 🤣🤣🤣
 
Sasa wakati Kama huo ndio tunawakumbuka wale panya wanaokula nguo..😂
Unatamani atokee aitafune kwenye mgongo au kwenye kola au kwenye mabega! Na sahivi watokee wapi wakati ulishawauwa..😅

Mkuu kama unatumeno twa panya ifanye hiyo kazi mwenyewe.. tatua tatizo .
 
Umenikumbusha mbali mkuu, kuna jamaa mmoja (classmate) wangu tumepiga nae chuo, alikuwa na manzi wake yan alikuwa akija kwa msela (kutoka mkoani) anakuja ameshona sare za vitenge na bwana ake, asiee huyo jamaa alikuwa hahemi kwa dem wake, boom likiingia lote dem ndo anamiliki ATM card, jamaa alitoka chuo weupe hana hata mia.na walishaachana mpaka.sasa.
Mkuu umeamua kuja kunisema [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siipendi hii minguo ya vitenge
Ni mchumba bado sijamuoa sasa basi, kuna sherehe tumealikwa inabidi niende naye sasa ananilazimisha nivae sare na yeye. anishonea shati la kitenge

Sasa wadau hii ishu siielewi nimekataa kanuna mbaya?

Wazoefu wa kupigilia sare za vitenge nipeni uzoefu kwa mke nahisi ni sahihi lakini kwa mchumba kwangu bado ni utata.
 
Mi binafsi sipendi nguo yoyote ya kitenge kwa mwanaume nacsitakaa Nivae kitenge ila kama anataka sare mnaweza mkapiga took flani mkali tu ila mka match color either ya shat or suruale . Mwanaume sio kuendeshwa mwanaume ni kuwa na msimamo ila msimamo wenye suluhu . Toa alternative ya kitenge
 
Vaa tu
Tena mtapendeza mno,ndio fasheni mpya siku hizi
 
Back
Top Bottom