Wazoefu wa Aliexpress

Wazoefu wa Aliexpress

Hii kitu ndo nataka niagize na mimi ila nasita kwenye uhakika wa kuletewa,, vipi kodi makato yake ikishafika huku ni asilimia ngapi ya manunuzi?
Ondoa shaka mkuu, wapo vizuri sana, soma hata review zao. Mimi ndiyo niliagiza hiyohiyo tablet mkuu, na shipping ikachukua week mbili.

Hakuna malipo mengine yoyote sanasana nililipa 3000 tu pale posta baada ya mzigo kunifikia.
 
Mimi nahitaji mdhoefu anisaidie kuagiza bidhaa niitakayo maana kuagiza mimi binafsi naona siiwezi.
 
Logic sio free shipping bali nani analeta. Inaweza andikwa free shipping ila ikawa ni Aliexpress standard free shipping (kwa maana seller atalipa mwenyewe fees) na inaweza ikawa shipping ya bei ndefu ila ni Caniao. Hao caniao unaweza ukajuta, miezi kadhaa unasubiri mzigo.
Niliwahi agiza nao mzigo hao Caniao mwaka jana ni vi percels vidogo tu ila vilitumia mwaka mmoja na miezi 6 kuja TZ, nlkua nisha sahau kabisa kama nimeagiza mzigo Aliexpress mpaka meseji ya posta ikanikumbusha...
 
Niliwahi agiza nao mzigo hao Caniao mwaka jana ni vi percels vidogo tu ila vilitumia mwaka mmoja na miezi 6 kuja TZ, nlkua nisha sahau kabisa kama nimeagiza mzigo Aliexpress mpaka meseji ya posta ikanikumbusha...
Mimi pia mkuu, mzigo wa mwaka jana mwezi wa 9 nimepokea juzi tu hapa.
 
Siku hizi Mizigo haipitii posta. Inapitia speedaf Yani siku 7-14 mzigo unakua umekufikia. Lkn jaza postal address na namba. Kubwa zaidi jaza namba yako ya simu inayopatikana 24. Hawa jamaa wa speedaf wanakupigia simu direct
 
Fresh shipping ya cainiao utalia. Mzigo ukifika basi ni zaidi ya miezi 3. Ukikuta Free shipping ya AliExpress standard or AliExpress selection standard basi hapo uhakika
 
Sijajua shida ipo Posta au wapi, mwaka jana niliagiza bidhaa AliExpress kwenye tracking ilionesha bidhaa imefika nchini mwangu ila mpaka leo sijapokea,
Tangu lini huo mfumo wa posta ukawa reliable?..
Better DHL or other carrier unaletewa mpk mlangoni kwako
 
Back
Top Bottom