Wazoefu wamikopo ya mabank nahitaji uzoefu wenu

N.m.b, t.p.b, crdb.je nyumba ina hati au leseni ya makazi?je unataka kuanzisha biashara au ulisha anza?kama unaanza usikope
Nilishaanza biashara zamani namtaji ninao ila nilitaka niongeze nguvu
 
Usikope kuanzisha biashara,kopa kuongezea kwenye biashara mkuu
 
Mkuu achana na mawazo ya kukopa benk bora uuze Nyumba mwenyewe kwa faida nenda kafanye biashara,,ukishaweka Nyumba dhamana hiyo siyo yako tena Mkuu.
 
Mkuu achana na mawazo ya kukopa benk bora uuze Nyumba mwenyewe kwa faida nenda kafanye biashara,,ukishaweka Nyumba dhamana hiyo siyo yako tena Mkuu.
Nikishaiuza ndio itaendelea kuwa yangu?
 
Naona michango mingi ni ya kumkatisha tamaa mleta mada. Kukopa ni moja ya njia ya kupata maendeleo. Matajiri wengi wanakopa. Kakope NMB mleta mkuu usikatishwe tamaa na wachangiaji
 
Naona michango mingi ni ya kumkatisha tamaa mleta mada. Kukopa ni moja ya njia ya kupata maendeleo. Matajiri wengi wanakopa. Kakope NMB mleta mkuu usikatishwe tamaa na wachangiaji
Nawashangaa kweli utadhani naenda kukopa mamilioni mengi, alafu wanadhani wao wanaakili nyingi sana kuliko mimi.

Biashara yangu ishaipima kuwa inaweza kurudisha marejesho vzr sanaaa
 
Nikishaiuza ndio itaendelea kuwa yangu?
Bora uuze mwenyewe utabaki na hela ya kununua kiwanja kingine siyo hao jamaa wa mikopo Mkuu,,nilikopa benk kama miaka kumi hivi mwisho kabisa ilibidi niuze Nyumba mwenyewe ili kumaliza deni,,kumaliza deni la mkopo salama ni ngumu labda uwe Mtumishi.
 
Nawashangaa kweli utadhani naenda kukopa mamilioni mengi, alafu wanadhani wao wanaakili nyingi sana kuliko mimi.

Biashara yangu ishaipima kuwa inaweza kurudisha marejesho vzr sanaaa
Mkuu nenda kakope utakuja hapa kuomba ushauri kwa yatakayokukuta,,hao matajiri wana biashara kubwa tena wengine wana makapuni na aset zao ni kubwa wewe una kanyumba hako kamoja unaishi na mama mkwe ndo unataka kwenda kukopea?naandika nachokifahamu mkuu
 
Dukani, Hahahaha nimecheka mkuu.... Ila mkuu sinakopa mkopo ambao upo ndani yauwezo wangu
 
Katika kufanya biashara leo, mtaji si tatizo, tatizo ni wateja. Mitaji inapatikana bank, na maafisa mikopo wako busy kutafuta wakopaji. Je biashara hiyo ina pato la kukidhi marejesho? Tafiti kabla ya kuomba mkopo, usije lia kilio cha mbwa mdomo juu.
 
Ndio nataka nikope kwaajili yakuongezea kwenye biashara
Una mawazo mazur sana kijana Ila kabla sijakushauri naomba kukuuliza swali

Je Hiyo biashara yako inamzunguko mkubwa sana kiasi kwamba unaona mtaji wako hautoshi mpaka uongeze mtaji kwa njia hatarishi?
 
buzitata, Sijibu.... Bila Shaka wewe nimuajiriwa namshahara wako hauzidi laki 7
 
Hahahaha nimecheka mkuu.... Ila mkuu sinakopa mkopo ambao upo ndani yauwezo wangu
Tatizo siyo kukopa kiasi unachoweza kulipa Mkuu,hiyo pesa mkopo hata kama ni kidogo haifai kabisa,ukizishika zinayeyuka zenyewe hutaamini.
 
buzitata, Sijibu.... Bila Shaka wewe nimuajiriwa namshahara wako hauzidi laki 7
Kwaiyo unataka kusema waajiliwa ambao mishahara yao haizid laki Saba hawawezi kukupa ushauri sahihi?

All in all nakushauri tu usikope ikiwa mzunguko wa biashara yako unaweza kuumudu kwa pesa ulonayo Ila ukiona demand ni kubwa kuliko mtaji ulonao Basi ruksa kukopa
 
Ni heri utafute njia zingine uongezee mtaji kuliko kukopa bank, Mkuu usikope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…