Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WAZULU WA IMHAMBANE, MOZAMBIQUE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Kisa hiki nimekitoa hapa hapa barzani nikizungumza na ndugu yangu Abdulkarim.
"Abdulkarim, jina hasa ni Saudtz Thomas Plantan.
Baba yake ni Thomas Saudtz Plantan na alikuwa Mwalimu Mkuu wa Mchikichini Primary School na kabla ya hapo alifundisha Dodoma.
Mmoja wa wanafunzi wake ni Job Lusinde aliyekuja kuwa waziri katika serikali ya Tanganyika.
Babu yake Sauti ni Chief Mohosh kutoka Shangaan Afrika ya Kusini.
Chief Shangaan na watu wake walikimbia kwao na kuingia Mozambique, Imhambane kukwepa vita vya Shaka.
Mjerumani Hermann von Wissman alifika Imhambane kijiji cha Kwalikunyi kutafuta askari mamluki waje Germany Ostafrika kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.
Hii ni baada ya Berlin Conference 1886.
Chief Mohosh na jeshi lake wakiongozwa na Wissman walikuja na manowari hadi Pangani na kuweka kambi hapo.
Katika jeshi hili la Wazulu alikuwapo Sykes Mbuwane ambae huko walikotoka dada yake aliolewa na Chief Mohosh.
Alikuwapo pia Ally Katini ndugu yake Sykes Mbuwane aiyekuwa kipofu.
Huyu Ally Sykes aliyekuja kuwa mtu maarufu sana jina hilo lake amepewa jina la huyu babu yake Ally Katini nduguye Sykes Mbuwane.
Huyu Sykes Mbuwane ndiye baba yake Kleist ambae mama yake ni Mnyaturu.
Kleist Sykes alizaliwa hapo Pangani 1894.
Hili jeshi lilikuwa pia na Wanubi kutoka Sudan wote wamechukuliwa na Wissman.
Wissman aliwaambia Wazulu katika mkataba wao kuwa wakishinda vita watatawala nchi kwa pamoja yaani Wajerumani na Wazulu watakuwa na madaraka sawa.
Ingawa Wajerumani waliweka ahadi hiyo jeshi hili maofisa walikuwa Wajerumani wenyewe na Wazulu walikuwa askari lakini kiongozi wao alikuwa Chief Mohosh ambae sasa akiwa katika nchi ya ugenini akabadili jina akawa Affande Plantan.
Baada ya kumshinda Abushiri ambae walimnyonga hapo Pangani jeshi likaelekea Kalenga kupambana na Mkwawa.
Vita hizi mbili zina historia kubwa lakini hapa naeleza kwa kifupi.
Wahehe wakashindwa vita na Mkwawa akajiua.
Wakati wanarudi kutoka Kalenga baada ya kushinda vita Sykes Mbuwane akafa maji Mto Ruaha akamwacha mwanae Pangani bado mdogo.
Haukupita muda na mama yake Kleist akafa.
Kleist akachukuliwa kulelewa na Affande Plantan.
Nchi ikatulia na hawa Wazulu na Wanubi wakawa ndiyo jeshi la kulinda himaya na likaitwa Germany Constabulary na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan.
Wajerumani walikuwa wanaliheshimu sana jeshi lao na waliliweka kambini na kutoa hudumu zote muhimu.
Wakajenga shule ilipo leo Ocean Road Hospital na katika shule hii ndipo walipowasomesha watoto wa askari wao.
Kwanza waliwafunza Kijerumani na elimu zote, pamoja na ufundi kisha wakawatia katika jeshi.
Hii ndiyo sababu watoto wote wa Affande Plantan: Thomas, Schneider, Mashado na Kleist walipata elimu ya juu kwa wakati ule na wote walikuwa askari jeshi.
Hawa wote walikuwa wakizungumza Kijerumani kama maji.
Hawa watoto wa Affande Plantan pamoja na mwanae wa kulea Kleist walipata fursa kubwa na walifanikiwa sana katika maisha yao hasa baada ya WWI Waingereza walipotawala Tanganyika kuanzia 1918.
Kleist alijulikana Dar-es-Salaam kama Kleist Plantan hadi alipofariki Affande Plantan ndipo alipochukua jina la baba yake mzazi, Sykes.
Watoto hawa walitawala siasa za Dar es Salaam wakati wa Waingereza na wakajenga msingi wa kudai uhuru wa Tanganyika kupitia African Association kisha TANU.
Kleist Sykes akaasisi African Association 1929 akiwa katibu muasisi na Mwalimu Thomas Plantan alikuja akawa rais wa TAA katika kipindi cha WWII.
Schneider Plantan yeye ndiye 1950 aliyeshinikiza TAA uongozi uende kwa vijana na akafanikiwa kuwatia Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes katika nafasi ya rais na katibu.
Historia hii ni ndefu na ina mengi.
Ikutoshe tu kuwa Schneider na Kleist Affande walivaa uniform ya Kaiser kupigana vita dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia 1914 - 1918."
Haya ndiyo aliyoandika Kleist Sykes na kutuachia kama urithi wetu kabla hajafa mwaka wa 1949.
Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes hadi alipofariki 1968.
Historia ina kawaia ya kujirudia.
Vita Vya Pili Vya Dunia Abdul Sykes na Ally Sykes, watoto wa Kleist na wajukuu wa Sykes Mbuwane walivaa unifomu ya Mfalme wa Uingereza kupigana dhidi ya Wajerumani wakiwa katika King's African Rifles (KAR) 6th Battalion.
Picha hiyo ya kwanza kushoto ni Kleist Abduwahid Kleist Sykes Mbuwane, Ebby Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane, Saudtz Thomas Saudtz Plantan, Abdulwahid Ally Kleist Sykes Mbuwane.
Hawa ni vitukuu vya koo mbili hizi za Sykes Mbuwane na Chief Mohosh kutoka Imhambane, Mozambique.
Picha ya pili ni Thomas Saudtz Plantan na ya tatu ni Kleist Sykes.
Picha ya nne kulia ni Abdul Sykes na Ally Sykes katika unifomu ya KAR wakiwa Burma katika Vita Vya Pili Vya Dunia.