Wazulu wa Imhambane, Kwalikunyu - Msumbiji katika kupigania Uhuru wa Tanganyika

WAZULU WA IMHAMBANE, MOZAMBIQUE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Kisa hiki nimekitoa hapa hapa barzani nikizungumza na ndugu yangu Abdulkarim.

"Abdulkarim, jina hasa ni Saudtz Thomas Plantan.

Baba yake ni Thomas Saudtz Plantan na alikuwa Mwalimu Mkuu wa Mchikichini Primary School na kabla ya hapo alifundisha Dodoma.

Mmoja wa wanafunzi wake ni Job Lusinde aliyekuja kuwa waziri katika serikali ya Tanganyika.

Babu yake Sauti ni Chief Mohosh kutoka Shangaan Afrika ya Kusini.

Chief Shangaan na watu wake walikimbia kwao na kuingia Mozambique, Imhambane kukwepa vita vya Shaka.

Mjerumani Hermann von Wissman alifika Imhambane kijiji cha Kwalikunyi kutafuta askari mamluki waje Germany Ostafrika kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Hii ni baada ya Berlin Conference 1886.

Chief Mohosh na jeshi lake wakiongozwa na Wissman walikuja na manowari hadi Pangani na kuweka kambi hapo.

Katika jeshi hili la Wazulu alikuwapo Sykes Mbuwane ambae huko walikotoka dada yake aliolewa na Chief Mohosh.

Alikuwapo pia Ally Katini ndugu yake Sykes Mbuwane aiyekuwa kipofu.

Huyu Ally Sykes aliyekuja kuwa mtu maarufu sana jina hilo lake amepewa jina la huyu babu yake Ally Katini nduguye Sykes Mbuwane.

Huyu Sykes Mbuwane ndiye baba yake Kleist ambae mama yake ni Mnyaturu.

Kleist Sykes alizaliwa hapo Pangani 1894.

Hili jeshi lilikuwa pia na Wanubi kutoka Sudan wote wamechukuliwa na Wissman.

Wissman aliwaambia Wazulu katika mkataba wao kuwa wakishinda vita watatawala nchi kwa pamoja yaani Wajerumani na Wazulu watakuwa na madaraka sawa.

Ingawa Wajerumani waliweka ahadi hiyo jeshi hili maofisa walikuwa Wajerumani wenyewe na Wazulu walikuwa askari lakini kiongozi wao alikuwa Chief Mohosh ambae sasa akiwa katika nchi ya ugenini akabadili jina akawa Affande Plantan.

Baada ya kumshinda Abushiri ambae walimnyonga hapo Pangani jeshi likaelekea Kalenga kupambana na Mkwawa.

Vita hizi mbili zina historia kubwa lakini hapa naeleza kwa kifupi.

Wahehe wakashindwa vita na Mkwawa akajiua.

Wakati wanarudi kutoka Kalenga baada ya kushinda vita Sykes Mbuwane akafa maji Mto Ruaha akamwacha mwanae Pangani bado mdogo.

Haukupita muda na mama yake Kleist akafa.

Kleist akachukuliwa kulelewa na Affande Plantan.

Nchi ikatulia na hawa Wazulu na Wanubi wakawa ndiyo jeshi la kulinda himaya na likaitwa Germany Constabulary na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan.

Wajerumani walikuwa wanaliheshimu sana jeshi lao na waliliweka kambini na kutoa hudumu zote muhimu.

Wakajenga shule ilipo leo Ocean Road Hospital na katika shule hii ndipo walipowasomesha watoto wa askari wao.

Kwanza waliwafunza Kijerumani na elimu zote, pamoja na ufundi kisha wakawatia katika jeshi.

Hii ndiyo sababu watoto wote wa Affande Plantan: Thomas, Schneider, Mashado na Kleist walipata elimu ya juu kwa wakati ule na wote walikuwa askari jeshi.

Hawa wote walikuwa wakizungumza Kijerumani kama maji.

Hawa watoto wa Affande Plantan pamoja na mwanae wa kulea Kleist walipata fursa kubwa na walifanikiwa sana katika maisha yao hasa baada ya WWI Waingereza walipotawala Tanganyika kuanzia 1918.

Kleist alijulikana Dar-es-Salaam kama Kleist Plantan hadi alipofariki Affande Plantan ndipo alipochukua jina la baba yake mzazi, Sykes.

Watoto hawa walitawala siasa za Dar es Salaam wakati wa Waingereza na wakajenga msingi wa kudai uhuru wa Tanganyika kupitia African Association kisha TANU.

Kleist Sykes akaasisi African Association 1929 akiwa katibu muasisi na Mwalimu Thomas Plantan alikuja akawa rais wa TAA katika kipindi cha WWII.

Schneider Plantan yeye ndiye 1950 aliyeshinikiza TAA uongozi uende kwa vijana na akafanikiwa kuwatia Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes katika nafasi ya rais na katibu.

Historia hii ni ndefu na ina mengi.

Ikutoshe tu kuwa Schneider na Kleist Affande walivaa uniform ya Kaiser kupigana vita dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia 1914 - 1918."

Haya ndiyo aliyoandika Kleist Sykes na kutuachia kama urithi wetu kabla hajafa mwaka wa 1949.

Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes hadi alipofariki 1968.

Historia ina kawaia ya kujirudia.

Vita Vya Pili Vya Dunia Abdul Sykes na Ally Sykes, watoto wa Kleist na wajukuu wa Sykes Mbuwane walivaa unifomu ya Mfalme wa Uingereza kupigana dhidi ya Wajerumani wakiwa katika King's African Rifles (KAR) 6th Battalion.

Picha hiyo ya kwanza kushoto ni Kleist Abduwahid Kleist Sykes Mbuwane, Ebby Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane, Saudtz Thomas Saudtz Plantan, Abdulwahid Ally Kleist Sykes Mbuwane.

Hawa ni vitukuu vya koo mbili hizi za Sykes Mbuwane na Chief Mohosh kutoka Imhambane, Mozambique.

Picha ya pili ni Thomas Saudtz Plantan na ya tatu ni Kleist Sykes.

Picha ya nne kulia ni Abdul Sykes na Ally Sykes katika unifomu ya KAR wakiwa Burma katika Vita Vya Pili Vya Dunia.

View attachment 2018683
Naam ! Ubongo umeshibakwa historia mujarab.
 
kwahiyo Mohamed Said unaamini wakristo wanakandamiza waislam Tanzania? waislam wanyimwa elimu? hivi, ni shule ngapi za wakristo zimeporwa ili zisiwe za mission, na zilianzishwa hata kabla hao watu wako hawajaanza kudai uhuru? hivi bila kanisa kuleta elimu hata wewe hapo uwezo wa kuandika kitabu chako ungepata wapi wakati waarabu walileta tu dini hawakuleta elimu? umeelimishwa halafu unasema umeonewa? udini umekujaaa, uliropoka sana kipindi kile cha shehe ilunga mkasababisha makanisa mengi kuchomwa zanzibar na watu kumwagiwa tindikali, haujatosheka.

kwa hali ilivyo Tanzania, mnataka wakristo wawafanyie nini ili mridhike, sema hapa hapa unataka tufanye nini? tuache kazi zote serikalini mshike ninyi? tuwapatie shule zote mshike ninyi sisi tujenge mpya? mbona chuo cha morogoro mlipewa lakini hata hakisikiki mnafundisha dini tu hamfundishi masomo? ini mtanata tufanye. sema hapahapa. umeona unavyoonyesha udini na siasa za chuki? unazeeka vibaya wewe.
Chapwa...
Nakusoma.

Huna ulijualo.
 
Naam ! Ubongo umeshibakwa historia mujarab.
Mbawa...
Kapata mshtuko si wengi walikuwa wanajua historia ya kweli ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika.

Majina anayosikia na kuyasoma hapa hajapata kuyaona popote.

Hajui vipi achanganye historia hii na hiyo inayoijua yeye.
 
huyu ni mdini na ni sumu na anaganga njaa hajawahi kua upande mmoja. anazeeka vibaya.
Bahati mbaya sana kaka, unajua achilia mbali hii historia ya juzi ya Mohamed said, bali hata ile ya Tanganyika ya Enzi hizo ilikuwa ya waislamu kabla ya kuja kina vasco dagama na hasadi zao kubomoa miji ya pwani, mimi nitaungana nawe ikiwa Mohamed said tutasikitika nae kwa kule kuwa wa Africa wa kizulu kuja kupambana na wa africa wenzao kama kina chief Mkwawa au Songea Mmbano n. K kwa hilo nitakuunga mkono ila bahati mbaya kwako ni kule kutokiri kwamba hao wakoloni ndio walikuwa wa dini wakubwa wakikristo
 
Mbawa...
Kapata mshtuko si wengi walikuwa wanajua historia ya kweli ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika.

Majina anayosikia na kuyasoma hapa hajapata kuyaona popote.

Hajui vipi achanganye historia hii na hiyo inayoijua yeye.
Kaka uhuru ulipambaniwa na kina Mkwawa kaka si hawa wazulu, ndio maana karma ikajakuwaumiza tena jamaa zako pale watu kama kk(kitwana kondo) alipokuja nae kuwa kibaraka wa wakoloni dhidi ya hao uwaitao wapigania uhuru, uhuru ni kutofungwa na fadhila walizokufanyia jamaa badala yake kueleza ukweli ' ikiwa miaka sitini hii ya uhuru nawe badowahofia kueleza ukweli hakuna mantiki ya "The untold story"
 
Makala...
Huenda hujanisoma kwa ukamilifu.

Hilo nimeliandika kwingi na nimetoa jina makhsusi naita, "Changamoto za Ukoloni."

Babu yangu Mkuu, Abdallah Mwekapopo Samitungo Mwiyuka kaingia Tanganyika akiwa askari akitokea Belgian Congo.

Sisi vitukuu wa hawa Wazulu, Wanubi na Wamanyema hatuwezi kuikataa historia hii ya wazee wetu kwani huo ndiyo ukweli wenyewe.

Lakini babu yangu Salum Abdallah kapambana na Waingereza ndani ya TANU na ndani ya TRAU.

Fanya search hapa JF utapata historia yake.
 
WAZULU WA IMHAMBANE, MOZAMBIQUE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Kisa hiki nimekitoa hapa hapa barzani nikizungumza na ndugu yangu Abdulkarim.

"Abdulkarim, jina hasa ni Saudtz Thomas Plantan.

Baba yake ni Thomas Saudtz Plantan na alikuwa Mwalimu Mkuu wa Mchikichini Primary School na kabla ya hapo alifundisha Dodoma.

Mmoja wa wanafunzi wake ni Job Lusinde aliyekuja kuwa waziri katika serikali ya Tanganyika.

Babu yake Sauti ni Chief Mohosh kutoka Shangaan Afrika ya Kusini.

Chief Shangaan na watu wake walikimbia kwao na kuingia Mozambique, Imhambane kukwepa vita vya Shaka.

Mjerumani Hermann von Wissman alifika Imhambane kijiji cha Kwalikunyi kutafuta askari mamluki waje Germany Ostafrika kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Hii ni baada ya Berlin Conference 1886.

Chief Mohosh na jeshi lake wakiongozwa na Wissman walikuja na manowari hadi Pangani na kuweka kambi hapo.

Katika jeshi hili la Wazulu alikuwapo Sykes Mbuwane ambae huko walikotoka dada yake aliolewa na Chief Mohosh.

Alikuwapo pia Ally Katini ndugu yake Sykes Mbuwane aiyekuwa kipofu.

Huyu Ally Sykes aliyekuja kuwa mtu maarufu sana jina hilo lake amepewa jina la huyu babu yake Ally Katini nduguye Sykes Mbuwane.

Huyu Sykes Mbuwane ndiye baba yake Kleist ambae mama yake ni Mnyaturu.

Kleist Sykes alizaliwa hapo Pangani 1894.

Hili jeshi lilikuwa pia na Wanubi kutoka Sudan wote wamechukuliwa na Wissman.

Wissman aliwaambia Wazulu katika mkataba wao kuwa wakishinda vita watatawala nchi kwa pamoja yaani Wajerumani na Wazulu watakuwa na madaraka sawa.

Ingawa Wajerumani waliweka ahadi hiyo jeshi hili maofisa walikuwa Wajerumani wenyewe na Wazulu walikuwa askari lakini kiongozi wao alikuwa Chief Mohosh ambae sasa akiwa katika nchi ya ugenini akabadili jina akawa Affande Plantan.

Baada ya kumshinda Abushiri ambae walimnyonga hapo Pangani jeshi likaelekea Kalenga kupambana na Mkwawa.

Vita hizi mbili zina historia kubwa lakini hapa naeleza kwa kifupi.

Wahehe wakashindwa vita na Mkwawa akajiua.

Wakati wanarudi kutoka Kalenga baada ya kushinda vita Sykes Mbuwane akafa maji Mto Ruaha akamwacha mwanae Pangani bado mdogo.

Haukupita muda na mama yake Kleist akafa.

Kleist akachukuliwa kulelewa na Affande Plantan.

Nchi ikatulia na hawa Wazulu na Wanubi wakawa ndiyo jeshi la kulinda himaya na likaitwa Germany Constabulary na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan.

Wajerumani walikuwa wanaliheshimu sana jeshi lao na waliliweka kambini na kutoa hudumu zote muhimu.

Wakajenga shule ilipo leo Ocean Road Hospital na katika shule hii ndipo walipowasomesha watoto wa askari wao.

Kwanza waliwafunza Kijerumani na elimu zote, pamoja na ufundi kisha wakawatia katika jeshi.

Hii ndiyo sababu watoto wote wa Affande Plantan: Thomas, Schneider, Mashado na Kleist walipata elimu ya juu kwa wakati ule na wote walikuwa askari jeshi.

Hawa wote walikuwa wakizungumza Kijerumani kama maji.

Hawa watoto wa Affande Plantan pamoja na mwanae wa kulea Kleist walipata fursa kubwa na walifanikiwa sana katika maisha yao hasa baada ya WWI Waingereza walipotawala Tanganyika kuanzia 1918.

Kleist alijulikana Dar-es-Salaam kama Kleist Plantan hadi alipofariki Affande Plantan ndipo alipochukua jina la baba yake mzazi, Sykes.

Watoto hawa walitawala siasa za Dar es Salaam wakati wa Waingereza na wakajenga msingi wa kudai uhuru wa Tanganyika kupitia African Association kisha TANU.

Kleist Sykes akaasisi African Association 1929 akiwa katibu muasisi na Mwalimu Thomas Plantan alikuja akawa rais wa TAA katika kipindi cha WWII.

Schneider Plantan yeye ndiye 1950 aliyeshinikiza TAA uongozi uende kwa vijana na akafanikiwa kuwatia Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes katika nafasi ya rais na katibu.

Historia hii ni ndefu na ina mengi.

Ikutoshe tu kuwa Schneider na Kleist Affande walivaa uniform ya Kaiser kupigana vita dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia 1914 - 1918."

Haya ndiyo aliyoandika Kleist Sykes na kutuachia kama urithi wetu kabla hajafa mwaka wa 1949.

Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes hadi alipofariki 1968.

Historia ina kawaia ya kujirudia.

Vita Vya Pili Vya Dunia Abdul Sykes na Ally Sykes, watoto wa Kleist na wajukuu wa Sykes Mbuwane walivaa unifomu ya Mfalme wa Uingereza kupigana dhidi ya Wajerumani wakiwa katika King's African Rifles (KAR) 6th Battalion.

Picha hiyo ya kwanza kushoto ni Kleist Abduwahid Kleist Sykes Mbuwane, Ebby Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane, Saudtz Thomas Saudtz Plantan, Abdulwahid Ally Kleist Sykes Mbuwane.

Hawa ni vitukuu vya koo mbili hizi za Sykes Mbuwane na Chief Mohosh kutoka Imhambane, Mozambique.

Picha ya pili ni Thomas Saudtz Plantan na ya tatu ni Kleist Sykes.

Picha ya nne kulia ni Abdul Sykes na Ally Sykes katika unifomu ya KAR wakiwa Burma katika Vita Vya Pili Vya Dunia.

View attachment 2018683
Inhambane na beach zake nzuri ,Xai xai na viunga vyake,nai miss Msumbiji
 
Bahati mbaya sana kaka, unajua achilia mbali hii historia ya juzi ya Mohamed said, bali hata ile ya Tanganyika ya Enzi hizo ilikuwa ya waislamu kabla ya kuja kina vasco dagama na hasadi zao kubomoa miji ya pwani, mimi nitaungana nawe ikiwa Mohamed said tutasikitika nae kwa kule kuwa wa Africa wa kizulu kuja kupambana na wa africa wenzao kama kina chief Mkwawa au Songea Mmbano n. K kwa hilo nitakuunga mkono ila bahati mbaya kwako ni kule kutokiri kwamba hao wakoloni ndio walikuwa wa dini wakubwa wakikristo
kwahiyo Tanganyika ilikuwa ya waislam, wakristo woote wa bara hawakuwepo. kabla ya uislam ilikuwa nchi ya nani labda. tunashukuru wazungu walikuja na ukristo tukajengewa na shule, wasingekuja tungekuwa maboko haram wote wasio na elimu hata hii jf isingekuwepo manake watu wangekuwa wamesoma madrasa tu hawajasoma shule dunia.
 
Chapwa...
Wewe una mamlaka gani?
Serikali inajua.

Tosheka na ukweli huu.
tangu uanze kusambaza chuki katikati ya watanzania ukiwa na shehe ilunga kipindi kile, umefanikiwa kwa lolote? moyo unakuuma moyo una uchungu bure, utakufa kabla ya wakati wako kwa magonjwa ya moyo kwasababu ya chuki na hasira dhidi ya wale unaowaita makafiri. imagine wewe hapo ulisimama kwenye muhadhara ukaita wakristo wa tanzania makafiri. umeshazeeka na umechelewa kusambaza chuki, watu wanaelewa maisha yalivyo na huwezi kuwadanganya tena.
 
Chapwa...
Ikiwa unadhani tatizo ni kuwa Waislam hawapendi shule basi wala huna sifa ya kujadili chochote na mimi.
kwani waislam wamekatazwa kwenda shule? kujenga shule? orodhesha hapa nini unataka wakristo wa Tanzania wafanye ili uridhike pengine. unasema mimi sina sifa ya kujadili na wewe, umezeeka hivyo bado unashadadia na unajadili mambo ya kizamani wanayostahili kujadili boko haramu na al shabab? kume uzee sio nywele nyeupe aisee.
 
kwahiyo Tanganyika ilikuwa ya waislam, wakristo woote wa bara hawakuwepo. kabla ya uislam ilikuwa nchi ya nani labda. tunashukuru wazungu walikuja na ukristo tukajengewa na shule, wasingekuja tungekuwa maboko haram wote wasio na elimu hata hii jf isingekuwepo manake watu wangekuwa wamesoma madrasa tu hawajasoma shule dunia.
Chapwa...
Hayo mengine ulioanzanayo hayana maana sana ila hili la elimu.

Ukisoma historia ya elimu utakugundua kuwa Waislam ndiyo waliokuwa na ujuzi wa zile zinaitwa 3Rs yaani Writing, Reading and Arithmetic.

Na alphabet zilizokuwa zinatumika ni Arabic script.

Elimu yote hii ilikuwa ikitolewa kupitia madras.

Krapf alipofika kwa Chief Kimweri Vuga alishangaa sana kumkuta Chief Kimweri na wanae wote wanajua kuandika na kusoma wakitumia herufu za Kiarabu.

Hii ilitia hasad ndani ya nyoyo yake na wakoloni walipoingia katika Pwani ya Afrika ya Mashariki jambo la kwanza walilofanya ilikuwa kupiga marufuku matumizi ya herufi za Kiarabu.

Hapo ndipo wakajenga shule Wamishionari wakishirikiana na serikali.

Na elimu ikawa inatolewa kwa ubaguzi wa imani.

Yako mengi.
 
wewe ni msambaza sumu ya chuki kwa watanzania na ninaamini basi tu kwasababu upo tz, ungekkuwa nchi zingine ungeshajiunga na makundi ya kigaidi.

sasa rafiki, kwanini pale kwenye mhadhara uliwaita wakristo "makafiri", unajisikiaje ukiwaita watanzania wenzio "makafiri".
 
Ingia Google fanya search utakuta maana nyingi.

Ukishazisoma rejea kwangu ikiwa hujaelewa.

Naona maelezo yangu ya historia ya elimu imekutuliza.

Jibiidishe kusoma utaelimika.

Hii kuja hapa upambane na mimi haitakusaidia kitu.

Wewe si wa kwanza.
 
kwahiyo Tanganyika ilikuwa ya waislam, wakristo woote wa bara hawakuwepo. kabla ya uislam ilikuwa nchi ya nani labda. tunashukuru wazungu walikuja na ukristo tukajengewa na shule, wasingekuja tungekuwa maboko haram wote wasio na elimu hata hii jf isingekuwepo manake watu wangekuwa wamesoma madrasa tu hawajasoma shule dunia.
Kwa hiyo kilwa ya karne ya tisa ile ya maghorofa na shilingi yake yenyewe ilijengwa na mzungu ewe mfia dini? Unazijua kweli Arabic numerals? Unaijua kweli historia ewe mfia dini? Hiyo hekaya kwamba hapakuwa na maendeleo kakudanganya nani? Ni kweli hufahamu kwamba mkoloni alipigana na Bwana heri upande wa pili akaingia makubaliano na makafiri? Ee masih mwana wa maryam
 
Makala,
Nina hulka moja nayo ni kuwa ninapoona mtu ameghadhibika lugha zinakosa adabu huacha mjadala.
 
nilishamsikia hata akiongea, anafanyaga kampeni ili ionekana Tanzania ilipiganiwa uhuru na watu wa dini yake, hivyo wanaotakiwa kutawala ni watu wa dini yake, sijaanza kumsikia leo wala jana. anapandikiza chuki ili ionekana watu wa dini yake wanapunjwa kiutaawala, kieliu n.k, hii nimbaya na ndiyo iliyoibua kipindi kile vijana wengi wanaharakati hadi kuchapisha vipeperushi kwamba nyerere alikuwa audui wa uislam. mtu anayepandikiza chuki hata kama ni mtu mzima hatufai hapa Tz, hivi unafikiri chuki ikisambaa kwamba waislam wanaonewa wao ndio walipigania uhuru hivyo wanatakiwa kupata share kubwa kuliko wengine, patatosha? kwani hao watu wengine hawana m chango wowote? wewe nawe naona una vimelea vya udini, mmeshachelewa. nawashauri somesheni watoto wenu ili wapate elimu washindane kwa hoja na sio kwa imani. nchi hii ni secular, ni ya kila mtu.
Na ww hutaki waislamu wajue kama wanamchango mkubwa kwenye uhuru na jinsi nyerer alivyofanya hila kuwadhulu.Ukweli unatabia ya ajabu sana hata ikichukua miaka 400 kufichwa ila utajulikana tu.Swali muhimu watu wenye akili wanalojiuliza hv Nyerere ni peke yake aliyeleta uhuru wa nchi hii?Jibu hapana alikua na wenzake .
Swali wenzie ni akina nan hapo ndio kazi ilpo
 
ajabu ni kwamba mohamed said unajifeki na kujipachika jina la mwanamke. vipi tena shehke
 
Back
Top Bottom