Wazulu wa Imhambane, Kwalikunyu - Msumbiji katika kupigania Uhuru wa Tanganyika

Sasa herufi za Kiarabu zinahusiana nini na Uislamu?
 
Kwa hakika ni vizuri kumshukuru sana Mohamed Said juhudi zake za kutujuza kuhusu historia ya nchi yetu. Histora ya Afrika, hususan ya Tanganyika ni pungufu mno haijaelezwa kwa ukamilifu. Huyu mwenzetu anatuletea maandiko hata ushuhuda ambao umefichika. Ila tukubaliane kuwa simulizi sahihi ni kitu kimoja ila maana ya simulizi, tafsiri na matumizi ya simulizi ni vitu viwili tofauti na hiyo tofauti lazima pande zote zikubali kuwa hakuna mwenye ukiritimba. Hivi akina Sykes walipokuwa wanapigana na Chief Mbano, kwa mfano, si hii ilikuwa Mzulu mwingine anapigana na mwenziwe ila mmoja katua Pangani meli kuingia Tanganyika mwingine kaja kwa mguu kutoka Zululand Afrika ya Kusini? Simulizi inaweza kuwa sahihi, je? Lakini jambo la kujivunia hapo ni lipi? Je, kweli Waislam wanaamini kwa dhati kabisa kuwa Nyerere hakuwathamini na kutambua mchango wa Waislam hapa Tanzania? Kwani alipotaifisha shule na hospitali alikuwa anataka kuwanufaisha akina nani? Mimi nilisoma Sekondari ya Mission Alliance Rungwe mwaka 1965 kabla ya shule kutaifishwa. Pale niliwakuta wanafunzi Waislam wengi wakitokea Iringa wakilazimishwa na wenyewe waende na wakae kwenye madarasa yao kujifunza elimu ya dini ya Kiislam wakati wa vipindi vya dini ambavyo hata sisi Wakristo tulilazimishwa kujifunza! Pia waliwezeshwa wakati wa Mfungo wa Ramadhan kutimiza hiyo Ibada. Headmaster wetu alikuwa Mzungu na alifanya hivyo akijua kuwa huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Rais Nyerere wakati huo. Haya kuhusu mchango wa Waislam katika kupigania uhuru kutowekwa dhahiri kwa maandishi, kwani hapa Tanzania hilo ni geni? Sasa hivi huwa mnaelezwa mchango wa watu binafsi au kundi kwenye masuala mengi ya kheri,iwe ushindi wa vita, elimu, afya au masuala ya maendeleo mengine. Mimi najua mashujaa kadhaa ambao wamezikwa kawaida wakati viongozi wao hata robo ya mchango wao hawakuufikia. Historia na michango yao imefichika. Sifa zinakwenda Serikalini au kwa Rais wa wakati huo kumbe pengine hawakuchangia hata kidogo kufanikisha jambo lenyewe, ilikuwa juhudi binafsi ya mtu au kundi la watu. Kwa mfano, hivi sasa orodha ya Makatibu wakuu bora, askari bora, daktari bora waliowahi kutokea katika historia ya nchi hii iko wapi ? Kwenye nchi zilizojiita za ujamaa ndiyo ilikuwa marufuku kabisa kusifu mtu au kikundi ila "Zidumu fikra za kiongozi" husika ndiyo ulikuwa wimbo uliokubalika na kuzoeleka. Huo ndiyo urithi wetu. Tusigombane bure. Wakristo, Waislam na wengine wote tumekuwa na mchango kadri ya kila mmoja wetu alivyojaaliwa na Mola wetu! Tuendelee kuishi pamoja na kushirikiana.
 

Ok, kumbe kwa asili akina Abdul Sykes walikuwa wazulu. Nimenote kitu leo.
 

Unaimuita mwenzako mfia dini wakati na wewe Ni mdini. Eti makafir. Makafir walikuwa wapi?. Acheni kilujiona Bora kuliko dini zingine.
 

Kasome historia vizuri. Nyerere alimshinda Abdul Sykes kwa Kura kwenye ukumbi wa annatouglo Dar. Kama Sykes angeshinda siku hiyo basi ndio angekuwa Baba wa Taifa leo.
 
Peter...
Kweli shule zilitaifishwa lakini kwa bahati mbaya sana pakawa na tatizo katika nafasi za Waislam kwenda sekondari kufikia chuo kikuu.

Hili ni tatizo kubwa na hapa tushajadili sana.

Rais Mkapa alipochukua urais katika mkutano aliofanya na Waislam Diamond Jubilee Hall kuna mengi alielezwa na yeye akasema kuwa kama Waislam wana ushahidi wa kisayansi kuwa wanadhulumiwa na watendaji ndani ya serikali wautoe.

Hii ndiyo sababu ya Hamza Njozi kuandika kitabu, ''Mwembechai Kiliings...'' (2002).
Yaliyoelezwa mle ndani yaliishtua serikali.

Kitabu kikapigwa marufuku.
 
kwani Tanganyika ya zamani ilikuwa pwani tu, haikuwa na mikoani? nijuavyo mimi, Tanganyika ya zamani ilijaa waislam upande wa pwani, na wapagani waliochanganyana na wakristo mikoani huko. kuna route chache ambazo waarabu walipita kibiashara, huko ndiko walijenga uislam. angalia kwamfano route ya katikati, kuanzia bagamoyo, dodoma kondoa, tabora hadi ujiji kigoma, ni sehemu zile tu walipita waarabu walijenga uislam. nje ya hapo wamebaki wapagani hadi leo. kuna maeneo hapa tanzania unatembea kilimita hata 100 hukuti msikiti, huko mikoani. ni makanisa. kwahiyo ukisema Tanganyika ilikuwa ya waislam, ujue waislam walitawala tu pwani (along the coast), huko mikoani hawakuwepo hadi waarabu walipopita. na hata hivyo idadi yao sio nyingi kiivyo, wanaongezwa tu na Zanzibar, ukisikia waislam Tanzania ni asilimia fulani, jua na wazanzibar ambao wanakaribia 2m wapo ndani. wakijitenga na bara waislam watakuwa minority. trust me.
 
kuna wakati nafikiria kwamba, kama kweli nyerere atakuwa alifanya hivyo, basi namshukuru sana sana, kwasababu kwa namna baadhi yenu hasa kina mohamed said mnavyotuchukia mngeshika nchi mapema, sasaivi Tanzania ingekuwa ya kiislam. na mngeshatuchinja wote. asante nyerere (kama kweli alifanya hivyo). hivi kwa chuki zenu za aina hii mngetawala tungeishi kweli. Ashukuriwe Mungu kwa kumtumia Nyerere.
 
Kasome historia vizuri. Nyerere alimshinda Abdul Sykes kwa Kura kwenye ukumbi wa annatouglo Dar. Kama Sykes angeshinda siku hiyo basi ndio angekuwa Baba wa Taifa leo.
Economist.
Bahati mbaya sana Mwalimu hakueleza vipi aliingia katika nafasi ya juu ya TAA.

Mwalimu hakupata hata kusema kuwa aliingia katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953 kwa kugombea nafasi hiyo dhidi ya Abdul Sykes aliyekuwa Secretary na Act. President wa TAA kuanzia 1951.

Mwalimu hakupaa kusema kuhusu uhusiano wake na Abdul Sykes na Hamza Mwapachu.

Hii ni historia ambayo kwa mara ya kwanza ilielezwa na Judith Listowel katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Mimi nilipokuja kuandika kitabu cha Abdul Sykes (1998) ndiyo nikaeleza kwa kirefu kuhusu kutafutwa kiongozi wa TAA 1953 na kuundwa kwa TANU 1954.

Katika hili wazalendo wawili, Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walihusika sana.
Abdul yeye alitaka nafasi ya rais wa TANU ikamatwe na Chief David Kidaha Makwaia.

Hamza Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere.

Hawa watu wawili walipokubaliana kuwa Nyerere ndiye achukue uongozu wa TAA 1953 na iundwe TANU 1954 hili jambo likawa ndilo limepita.

Na Abdul alisaidia Nyerere kushinda uchaguzi wa rais wa TANU uliofanyika Arnautoglo tarehe 17 April 1953.

Kamati ya ndani ilikubaliana kuwa Nyerere ndiye atakaeongoza harakati za kudai uhuru chini ya TANU kwa hiyo achaguliwe katika uchaguzi ule wa 1953 na 1954 TANU inaundwa na Mwalimu ataongoza harakati za kudai uhuru.

Katika uchaguzi ule Julius Nyerere ''alishinda'' na uoongozi wa TAA ulikuwa kama hivi:

J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias naWaziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer na Ally K. Sykes Assistant Treasurer; Wanakamati Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.[1]

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Sasa hapo hakuna suala la Abdul Sykes kushinda uchaguzi ule kwa kuwa makubaliano yalikuwa Nyerere akabidhiwa uongozi 1953 TANU iundwe na Nyerere aongoze mapambano ya kudai uhuru.

Ndiyo sababu unaona TANU ilipoundwa mwaka wa 1954 kadi no. 1 Julius Kambarage Nyerere, kadi no2. Ally Kleist Sykes na kadi no. 3 Abdulwahid Kleist Sykes.

Bahati mbaya sana Nyerere hakupata kueleza historia hii.
Sijua kwa nini.

 
Chapwa...
Unasema tu maneno kama yanavyokuja akilini bila kufikiri na kujua athar ya maneno yako.

Tuwe pamoja hapa na usome historia ya wazee wangu vipi walimpokea Nyerere na wakamweka mbele kama kiongozi wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Utatujua na huenda ukabadili fikra zako.
Angalia picha hiyo hapo chini:


Chapwa...
Hili suala ni nyeti sana lakini nitakuwekea yale niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) uongeze maarifa yako:

Religious Distribution in Tanzania

In order to appreciate the impending danger we need to agree that Muslims are a majority[18] in Tanzania and in any civil upheaval large numbers carry psychological advantages.

The government has over the years been making deliberate efforts to conceal this fact and to portray to the world that Muslim-Christian religious distribution is more or less the same and at times to give an impression that Tanzania is a Christian nation and Muslims are a minority.

[19]The government to say the least has been very evasive on this question.[20] When the government went into its first census after independence the government did not envisage that the results would show Muslims as a majority. In the 1957 census Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. Ten years after in 1967, in the post-independence census Muslims were 30%, Christians 32% and local belief 37%.

Reasons were not given for this sudden decrease of Muslims or the growth of pagans. It is on record that the 1967 statistics were doctored to show that Muslims were trailing behind Christians in numerical strength.[21]D.B. Barret gives statistics which show Muslims as a minority: Muslims 26%, Christians 45% and local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 have Muslims at 40%, Christians 38.9% and local belief 28%. Africa South of the Sahara shows that Muslims are a majority in Tanzania at 60% this figure has remained constant in all its subsequent publications since 1991.[22]
 
Kazi kweli kweli! 20/70?
ni udini udini tu.
Naanza kuamini kuwa Manchurian wapo na sio hadithi za abunuasi.
 
Kazi kweli kweli! 20/70?
ni udini udini tu.
Naanza kuamini kuwa Manchurian wapo na sio hadithi za abunuasi.
Syll...
Harakati za kudai uhuru zilikwenda vizuri sana kwa umoja na mshikamano wa hali ya juu kabisa.

Ikutoshe tu kuwa kwa kuwa madai mengi dhidi ya Waingereza yalikuwa yakipitishwa kupitia African Association viongozi wa wakati ule Mzee bin Sudi President na Kleist Sykes Secretary waliona si siwa walitaka AA isiguswe na hisia za Waislam na Uislam ibakie "apolitical."

Kwa ajili hii wakaunda Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika mwaka wa 1933.
Bila ya kuijua historia hii utahangaika sana.

Hutojua kwa nini leo tumejikuta katika hali hii.

Unatakiwa ujue kwa nini Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alifukuzwa chama mwaka wa 1958.

Unatakiwa ujue historia ya Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Suleiman Takadir katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ujue historia ya kupigwa marufuku EAMWS nk. nk.
Vinginevyo hakika utahangaika.

Bahati mbaya tunajifanya kama vile historia hii na watu hawa hawakupata kuwepo katika kupigani uhuru wa Tanganyika wala hawakupata kuwa viongozi wakuwa katika TANU.


Mzee bin Sudi aliishi hadi 1972 na nimuasisi wa African Association 1929.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…