Wazungu kuiita Serikali yetu "Regime" ni sawa?

Wazungu kuiita Serikali yetu "Regime" ni sawa?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Maana ya regime ni nini? je, neno regime lina maana sawa na government?

Niliwasikia wajumbe wa kamati mojawapo ya European Union wakisema Tanzania kuna regime ambao alipewa hela za covid-19 wakati wenyewe wanasema hakuna covid.

Neno walilotumia ni sahihi kiasi gani?
 
Regime definition:
1. a government, especially an authoritarian one.

Authoritarian definition:
1. favouring or enforcing strict obedience to authority at the expense of personal freedom.
 
Hahahahahaha alafu file lao la ICC lipite hivihivi?

Mwaka huu lazima kuna watu wataita Maji mmaaaaa!! Umeshakuwa labeled kuwa unaongoza regime alafu ICC wakuache? Stay tuned😂😂😂
 
Regime definition:
1. a government, especially an authoritarian one.

Authoritarian definition:
1. favouring or enforcing strict obedience to authority at the expense of personal freedom.
Mh, kweli tumefika huko? du
 
Ni sawa, ni kama vile tu humu JF kambi pinzani zikikutana kuna kuitana majina kusadifu kile unataka kuachive mfano mpinzani kumpa jina kama nyumbu, CCM wakaitwa nzi wa kijani.
 
...
Niliwasikia wajumbe wa kamati mojawapo ya European Union wakisema Tanzania kuna regime ambao alipewa hela za covid-19 wakati wenyewe wanasema hakuna covid.
...
... kama kweli hilo lilifanyika; namaanisha kama kwenli Serikali ilipokea fedha za msaada za COVID-19 huku ikijua nchini hakukua na COVID huo ni utapeli wa hali ya juu kabisa wa kimfumo! Najiuliza hizo fedha Serikali ilizipokea za nini? Inaakisi jinsi tulivyo na tunavyofanya mambo yetu "kipuuzi".
 
Ma Beberu wote wanajua JPM ni chuma, chuma Cha pua na wanajua hajaribiwi. Kama boss wa migodi ya Barick duniani aliukubali mziki wa JPM akiwa na wataalamu wake Bora kabisa wa madini zaidi ya ishirini walitepeta utakuja kua ao watu wa ulaya ambao nao wanaitegemea US katika ulinzi wa nchi zao.
 
Sasa kwa taarifa yako , jiandae kukisindikiza icho chuma chako icc siku si nyingi
 
Hiyo ndio taswira yetu nje sasa, but wapo mazuzu wanashangilia, iko siku watapata akili.

Kuwanyan.ganya wapinzani ushindi wao kwa lazima ni u dikteta tu, nothing else.
 
Utawala wa nguvu za Giza huu.

"utawala wa awamu ya tano una lawiti katiba".
@ Alexander the Great.
 
Regime: Kikundi cha utawala kinachopendelea au kinacholazimisha kuabudiwa na kuogopwa zaidi huku kikiminya uhuru wa raia wake

Sasa aseme hii yetu ni Regime au sio?

Tafsiri sahihi sana, na hii ndio hali halisi tuliyonayo sasa.
 
Ma Beberu wote wanajua JPM ni chuma, chuma Cha pua na wanajua hajaribiwi. Kama boss wa migodi ya Barick duniani aliukubali mziki wa JPM akiwa na wataalamu wake Bora kabisa wa madini zaidi ya ishirini walitepeta utakuja kua ao watu wa ulaya ambao nao wanaitegemea US katika ulinzi wa nchi zao.

Zamani Nyerere alikuwa anasifiwa hivi hivi kuwa kakata mirija ya mabeberu, ana misimamo isiyoyumba na mabepari wanaililia Tanzania, tuliishia kuvaa viraka na bidhaa kama sabuni, sukari nk vilikuwa anasa. Ule ujinga tuliolishwa kuwa wakenya wanawaendekeza mabeberu, wakawa wanatuchora tu tunavyojipaka mafuta ya kupikia. Nenda huko bungeni sasa hivi ukasikie kilio cha wezi wa kura ww ccm kuhusu kukatwa posho.
 
Back
Top Bottom