Wazungu na matajiri wanawezaje kula hivi?

Wazungu na matajiri wanawezaje kula hivi?

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Kiukweli najiuliza matajiri na wazungu wamewezaje kula matunda tu kama msosi wa jumla hasa usiku?

Yaani eti anakula matunda tu analala!

Nikaona isiwe ishu, acha name nijaribu.
Saa 2 nikala matunda nikaelekea kulala.

Yaani usiku nipo kitandani nasikia watu ndotoni wanasema RIP. Nikaamka nikaanza kutazama bati, mpaka kufikia kumkosoa fundi aliyepaua.

Wadudu nao tumboni wanaulizana huyu jamaa leo vipi? Hali ama?

Nikaona isiwe kesi nisije pelekwa hospital bure kutundikiwa dripu wakadhani mie mgonjwa. Ikabidi tuu nisonge ugali usiku.

Najiuliza hawa watu tajwa wanaishije kwa kula hivyo vijitunda kisha wanalala vizuri tu?

Nimekoma aseeh
 
Kiukweli najiuliza matajiri na wazungu wamewezaje kula matunda tu kama msosi wa jumla hasa usiku?

Yaani eti anakula matunda tu analala!

Nikaona isiwe ishu, acha name nijaribu.
Saa 2 nikala matunda nikaelekea kulala.
Yaani usiku nipo kitandani naskia watu ndotoni wanasema RIP..
Nikaamka nikaanza kutazama bati, mpaka kufikia kumkosoa fundi aliyepaua...

Wadudu nao tumboni wanaulizana huyu jamaa leo vipi? Hali ama?

Nikaona isiwe kesi nisije pelekwa hospital bure kutundikiwa dripu wakadhani mie mgonjwa..
Ikabidi tuu nisonge ugali usiku.

Najiuliza Hawa watu tajwa wanaishije kwa kula hivyo vijitunda kisha wanalala vizuri tuu? Nimekoma aseeh
Hilo mbona linawezekana! Sema mazoea nayo yanachangia, we ulitakiwa ule chakula kidogo mno tofauti na siku zote then utupie matunda mdogo mdogo utajikuta umezoe. Ila kama upo shamba usile tunda afu ulale.
Mi matunda nakula na nalala vizuri tu!
 
Mkuu hayo matunda mbona ntamaliza mwembe mzima?

Labda nisonge ugali niutulize in case of emergency..
 
Kwanini unakula matunda pekee halafu unalala ilhali una mawazo na kipato chako ni duni!?
Hizo menu ni za watu wasio na mawazo. Mawazo ni moja ya kisababishi cha mmeng'enyo wa haraka wa chakula.
Sasa umejikuta na mimeng'enyo double huwezi lala asilani.
 
hahahahahahaha mkuu haujala kabisa mchana maisha yenyewe ya kulenga kwa manati alafu ule matunda yenyewe mawili tu kwa kuvizia vizia ili kuweka bajeti yako ndogo huwezi kufikisha asubuhi kabisa maana minyoo inaweza kukupiga hata vibao
Nambie tajiri unaishije kwa kula hivi?

Kiukweli minyoo ni ndugu zangu wa damu siwezi waacha..
 
Majority ya Wazungu wanakupiga pande kubwa la steki na mash potatoes +veg na glass moja kubwa ya bia au wine,huyu ndiyo wa kwanza kusikia anashiba kwa matunda tu.
 
hahahahahahaha mkuu haujala kabisa mchana maisha yenyewe ya kulenga kwa manati alafu ule matunda yenyewe mawili tu kwa kuvizia vizia ili kuweka bajeti yako ndogo huwezi kufikisha asubuhi kabisa maana minyoo inaweza kukupiga hata vibao
Nadhani unaelewa mkuu yaani minyoo inakuuliza "ndugu yetu hata Wewe "??
Tuwaachie matajiri haya
 
Back
Top Bottom