Wazungu: "Samatta si mchezaji wa EPL", wamfananisha na panya

Wazungu: "Samatta si mchezaji wa EPL", wamfananisha na panya

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Baadhi ya shabiki wa 'kilabu' ya mpira wa miguu ya Aston Villa wameshikwa na hasira baada ya kupata habari kuna uwezekano wa mshambuliaji wa timu yao Mbwana Samatta kwenda kujiunga na timu ya Galatasaray ya Uturuki mwishoni mwa msimu 2019/2020.
Walirusha ujumbe wa kejeli na dharau kwenye kurasa za mtandao wa twitter ilipo taarifa za tetesi hizo.

Wasome hapo chini. Mmojawapo alimfananisha na panya wanaokimbia kwenye jahazi linalozama.

" Seems like Rats leaving a sinking ship to me... hey ho. "__Maca Brazier

Mwingine adai kwa maoni yake hana kiwango kizuri kutosha kucheza ligi kuu Uingereza

"I'll pack his bags. Weak, lack of movement and no killer instinct. Not good enough for the Prem IMO" __Johno

Samagoal baki Aston Villa kama watabaki ligi kuu kisha wapigie magoli ya kutosha wakutambue wewe ni nani, na kwanini walikutafuta na kulipa dau lile kwa Genk.

Heshima yako kubwa sana.

Samatta-PanyaAkimbiaJahazi.PNG

Samatta-2.PNG
 
Hiyo sentensi ya "rat" hapo hujaielewa vizuri

Tanzania hatujui Kiswahili,hatujui Kingereza,lugha zetu za asili hatujui,yaani hii ndio evidence yenyewe!
Nimepokea maoni yako.
Ahsante

BTW, nimetumia uandishi wa kuvuta mjadala, hapo anaweza kuwa alimaanisha kwa maoni yake Samatta anawakimbia Aston Villa FC sababu wanashuka daraja. Nilielewa hivyo lakini nilichagua kutafsiri nilivyo tafsiri awali.
 
pili tukubali tuu kuwa huyu ndugu yetu umri umemtupa mkono ingawa mwili unamdanganya danganya! na ni vizuri akaanza kutundika buti lake kwa kucheza ligi ambazo hazina mikimiki kama ya uturuki, marekani, na mwishoni uarabuni
 
Mtoa mada naomba nikukosoe kidogo. Hasa hapo kwa "Like Rats leaving a sinking Ship".
Huo ni kama msemo tu.Una maana yake hautafsiliwi moja kwa moja.
Ngoja nikutolee wewe kama mfano.Chukulia upo vizuri una marafiki wengi wengi.Ila bahati mbaya ukateleza maishani ukaanza kuwa na maisha ya kifukara hivi na hao marafiki wakaanza kukukimbia.Hapo sisi wambea wa huko nje tutaanza kusema"His former friends have deserted him like rats leaving a sinking ship".
Kwenye hiyo post ni hivyohivyo tu.Huyo shabiki anaona tetesi za kuondoka kwa Samatta ni mwanzo wa wachezaji wao wengi kuondoka Aston Villa(sinking ship) maana anahisi timu yake yaweza shuka daraja.
rats-leaving-a-sinking-ship-vector-id487626606.jpeg
 
" Seems like Rats leaving a sinking ship " nani ni 'Rats', nani ni 'sinking hole' …..soma viizuri huo mshororo
Mtoa mada naomba nikukosoe kidogo. Hasa hapo kwa "Like Rats leaving a shipping Ship".
Wakuu nisomeni vizuri hapa nilivyomjibu mdau aliyetangulia kukosoa tafsiri.
Nilifanya makusudi lengo kuvutia mjadala, mtu akiona hivyo anashawishika kuja kusoma na pengine kuchangia.
Kwani hamjifunzi uandishi kama wa zile channel matata za Youtube kama ya Ophoro au ile ya Jiwee? Tofauti ni maudhui tu lakini mbinu ni hiyo hiyo.
Hujawahi kusoma habari "Waziri akamatwa kwa kuiba kuku", ukisoma habari unakuta kuna mtu anayeitwa Juma Waziri huko Bunju Tegeta kibaka tu wa mtaani kaiba kuku na siyo waziri kama mbunge mwenye cheo cha uwaziri?
Nimepokea maoni yako.
Ahsante
BTW, nimetumia uandishi wa kuvuta mjadala, hapo anaweza kuwa alimaanisha kwa maoni yake Samatta anawakimbia Aston Villa FC sababu wanashuka daraja. Nilielewa hivyo lakini nilichagua kutafsiri nilivyo tafsiri awali.
 
Wakuu hapo juu nisome vizuri nilivyomjibu mdau aliyetangulia kukosoa tafsiri.
Nilifanya makusudi lengo kuvutia mjadala, mtu akiona hivyo anashawishika kuja kusoma na pengine kuchangia.
Kwani hamjifunzi uandishi kama wa zile channel matata za Youtube kama ya Ophoro au ile ya Jiwee? Tofauti ni maudhui tu lakini mbinu ni hiyo hiyo.
Hujawahi kusoma habari "Waziri akamatwa kwa kuiba kuku", ukisoma habari unakuta kuna mtu anayeitwa Juma Waziri huko Bunju Tegeta kibaka tu wa mtaani kaiba kuku na siyo waziri kama mbunge mwenye cheo cha uwaziri?
Nimekuelewa mkuu.Ila nimefanya kwa faida ya wengi.Maana kuna baadhi ya watu wanaweza kulibeba hivyohivyo.
 
Nimepokea maoni yako.
Ahsante

BTW, nimetumia uandishi wa kuvuta mjadala, hapo anaweza kuwa alimaanisha kwa maoni yake Samatta anawakimbia Aston Villa FC sababu wanashuka daraja. Nilielewa hivyo lakini nilichagua kutafsiri nilivyo tafsiri awali.
Asikuzingue tafsiri ndio hio hio
 
Back
Top Bottom