Wazungu wa Afrika Kusini wakata kata kata ofa ya Trump ya ukimbizi Marekani.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Baada ya jana Trump kusaini amri ya kukata msaada kwa South Africa pamoja na kuruhusu kupewa hifadhi ya ukimbizi Marekani kwa wazungu wa Africa Kusini(Boers) anaosema wananyanyaswa na serikali ya Africa Kusini, wazungu wenyewe wa huko wamepuuzilia mbali hatua hizo wakipaza sauti kila kona kwamba wanaishi vizuri Africa Kusini na hawana haja ya ukimbizi kwenda kuishi Marekani!

Wazungu wa Africa Kusini hadi wale wanaoonekana kuwa bado na ukaburu wamekataa kata kata kwamba wanabaguliwa nchini humo! Elon anamdanganya sana Trump.

 
Huyu Trump akumbuke kuchamba kwingi.... Watu sasa wanamwona kama zuzu, full kuropoka
 
Anawaambia waende huko US ili aiwekee vikwazo SA
 
Aibu wameipata, polepole tutaelewana tu...😜
 
Trump ana akili fupi sana anadhani kila mtu anatamani kuishi Marekani wazungu wa Africa Kusini
Matajiri wanashikiria uchumi wa Africa Kusini waondoke wakakae kwenye nyumba za mbao Texas😬
Au California wachomwe moto? Trump na huyu Musk ni wapumbavu sana
 
Waziri wa sasa wa kilimo huko bondeni ni Kaburu,

Wanaanzaje kukimbia nchi huku chama chao DA kikiunda serikali ya mseto.

Musk kama anawenda nduguze,awasaidie wakiwa huko huko ili waing'oe ANC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…