Wazungu waliokuja kikazi hapa ofisini wanafurahi watanzania ni wakarimu maana wanapata treatment na attention nzuri hata kwa mabosi wakorofi.

Hata enzi za ukoloni,wapo waliowachekea na kutoa Siri za viongozi wa kimila,twende tutafika tuu!
 
wamekuja kuwafundisheni upinde wa mvua [emoji304]subirini na kuwashobokea wazungu
 
Mwafrica huiogopa hata maiti ya Mzungu, Mwafrica mtu mzima humuogopa hata Mzungu mtoto.

Kiongozi Africa akitembelewa na kiongozi Mzungu kwake ni fahari na sehemu ya mafanikio.

Binafsi nawachukulia watu wa kawaida sana.
 
Wacha wawazoee watakuwa na sifa mpya ya WaTz, wanaomba kupita kiasi.
 
Kuna siku Bank ya Stanbic aiseee adi niliona aibu mimi. Alikuja mzungu umri wa makamo kama around 50 na kabinti kakibongo naona ndio kashika mikoba kake na atakuwa anakaweka kale.

Wameingia pale bank dah wafanyakazi zaidi ya wangapi wanamgombania kumhudumia. Kuna teller ilikuwa ipo closed wakafungua kwaajiri ya kumsaidia yeye kuna mdada aliingia tena nadhani sio teller ni wale mastaafu wa ndani huko.

Akaja akaanza mhudumia fasta akaondoka. Wadada ni kujichekesha chekesha na kujibaraguza.

Asieee raia walimind sana wao wamekaa foleni hawa mbwa anakuja mzungu wanamchangamkia utadhani ni nano vile.

Ilikuwa ni aibu kubwa sana aisee.
 

Nakubalina na wewe ngozi nyeupe yeyote ikija bongo au niseme mgeni yeyote kutoka nchi nyingine wanakarimiwa vizuri sana. Nchi nyingine hakuna ukarimu wowote.Kwa kifupi TZ ni wakarimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…