Wazungu wana uchawi wa "small scale"?

CreditAnalyst

Haya mambo yapo sana, naona haujabahatika kukutana na behind the scenes.
 
Kumbe na wao wamo.
 
Biashara zao ni ubora wa bidhaa na huduma. Tz biashara haziendi kwa kuwa umasikini umezidi, watu hawana pesa za kutumia. Nchi zilizoendelea kuna ajira na kupelekea watu wengi kuwa na uwezo wa kufanya manunuzi, hivyo biashara zinashamiri.
Ase ndio maana umasikini ni mbaya.
 
Wazungu wanaongoza kwa uchawi na wana majini makali sana.
Biashara ya kuuza majini inalipa sana mitandaoni na wengi ni matapeli basi wazungu wanaibiwa sana tu huko,unakuta mtu ana kila kitu lakini bado anapoteza hela zake kutaka kununua jini alifuge. Na hata hivi vitabu vya kishirikina vinauzwa sana mitandaoni na wazungu wananunua.
 
Yaani wazungu wachawi balaa nakumbuka Kaka yangu mpendwa alikuwa narafiki yake mkongo miaka ya 1998 huko wanauza vinyago vilivyotumika katika uchawi naushirikina bei ilikuwa nzuri na moja katika biashara iliyompelekea Kaka kuanza kutajirika ni hii.

Wananunua vinyamkera vinyago kwa waganga, wazee wa jadi na kwengineko na kuwauzia wazungu kutoka Ufaransa na hao wazungu walivyokuwa nyoko ukienda kuchonga kinyago kipya au kinunua hakija tumika katika mambo ya ushirikina au mambo ya jadi hawanunui.

Wazungu wachawi kwenye kila sekta usikute wanatupita hata sisi wa Afrika.
 
Uchawi wa biashara mojawapo kati ya mengi ni kuanza kuwa na wazo jipya la biashara na sio kuiga kwa jirani. Lkn pia kujiangalia wewe una nini hasa upande wa uwezo na udhaifu wako lkn pia angalia fursa na matishio ya unachotaka kukifanya.

Hapo utajua una rasilimali zipi, una lengo gani na hatua zipi za kufuata kufikia malengo yako.

Ni vyema ukaandaa mpango wa biashara yako na kuwatambua wateja na washindani wako. Chunguza "gap" ambalo lipo ktk biashara za wenzako ambapo wateja wanahitaji lijazwe.

Na mengine mengi wataalamu wa masuala ya biashara watajazia.

Haya mambo ya kwa wataalamu ni mbwembwe tu na ni kuongeza gharama za mtaji wa biashara bila sababu.

Mtazamo!
 
Hichi kitu naona kama ni Cha kweli kabisa, wazungu ni wachawi ila wanakinga za kutosha kuzuia wasilogeke. Ndo mana enzi za ukoloni babu zetu walipata shida sana na uchawi wao kwa wazungu ulidunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazungu ni nani? Define hiyo term "mzungu".

Unajuaje huyu mzungu, na huyu si mzungu?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Ndio mkuu, yani cha kwanza ni Guard, biashara isiingilike kwa dumba. Yani kama mtu anataka kukuaribia, ashindwe. Pili mambo na mipango yako inabidi uvipe assurance ya kuprosper.
Sehemu kubwa ya hayo mambo ni imani zetu tu kwenye ushirikina,si kweli kwamba lazima uende kwa wataalamu ili ufanye biashara wapo watu wanafanya biashara pasina kufanya ushirikina na biashara zao zipo vizuri tu na wapo ambao hadi wanafirisika kwa kutumia hela kwa waganga na hakuna walichopata.
 
Wazungu ni nani? Define hiyo term "mzungu".

Unajuaje huyu mzungu, na huyu si mzungu?

Tuanzie hapo kwanza.
We nae sio kila kitu ubishi tu,hilo neno linajulikana huwa linatumika kukusudia watu gani sasa sijui kuna haja gani ya kubishana katika hilo. Nenda kwenye jukwaa la lugha ukafundishe hilo neno vizuri.
 
Uwo mchongo kaka ako bado anapiga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…