Muuliza swali, jibu lake ni vyakula wanavyokula tangia wakiwa Wadogo kupelekea kuwa hivyo mimi nilikuwa na ndugu yangu kabisa alienda Austria amekaa muda tulipokutana naye alikuwa na harufu hiyo of course siyo harufu nzuri hata chembe kama hujaizoea ila ukiizoe unaona fresh tu.
Japo, mwingine anaweza sema kuwa ni lotion ama perfume kitu ambacho siyo kweli kwa sababu wazungu wako selective sana inapokuja issue ya vipodozi na lotions hadi sabuni ni lazima family doctor ama apate ushauri kutoka kwa daktari kuhusu vitu hivyo kabla hajavitumia.
Na haiwezikani wazungu, wote wakatumia sabuni na lotion brand moja siyo rahisi na haiwezekani kwa sababu, wazungu wanazo sabuni na lotion na perfume nyingi sana kiasi kwamba hawawezi kufanana.
Kwa hiyo basi chanzo chake ni vyakula kwa sababu kama asilimia 99% hivi nimehakikisha ni vyakula hasa vyakula vya makopo (canned food).
Mimi ndiyo hicho ninachoelewa na pia, nimebahatika kukaa na aina tatu za jamii ya wazungu (nimekaa nao kule kwao ), (walio kuja huku Africa , waka kaaa kwa muda fulani), na wanaoishi huku Africa yaani wazungu ambao wazazi wao ni wazungu ila watoto wamezaliwa huku na wamekaa huku Africa muda wote sasa katika makundi hayo matatu hayo harufu zao ni tofauti.