Wazungumzaji wa lingala na kiswahili cha kikongo tupeane phrases za Lingala

Utanilipa au ni furahisha genge?
 
Haa...napenda kikongo mimi,lugha yao iko romantic sana. Hebu mmoja anipe verse yoyote ya jb mpiana kwa tafsiri ya kiswahili hasa kutoka ule wimbo wa feux d'amour

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Maana yake mwisho wa mapenzi... Kuna sehemu anasema. Bota na ndenge masua eponana... Yaan ona meli inavyoondoka Bandarini
 
Kumisaka ngai Kiba, Pesaka ngai lokumu Nazali mwasi ya liboso na la vie na yo Kosambwisa nga boye te,
Ata okomi na mbongo Basi tokeseni; ya lisuma mpe ya ba chance

Nipe heshima yangu Kiba, mimi ni mke wako wa kwanza acha kunidharau hivyo, Hata ukipata pesa, kuna wanawake watakaokuletea mikosi; na wengine bahati
 
Nimepata sentensi hapo,,, Sherry kitoko nangai - mwanamke wangu mzuri
(Ngoja nimpost shemeji yenu Whatsapp na status hiyo)
Watu hatuchelewagi nilishamposti jana,wacha acheke,anasema utakuwa chizi wewe soon😄😄
 
Moja ya records za mwisho za Franco kabla hajaaga dunia

Les Rumeurs

Mboka epanzani sango eh eh
Majungu yanaendeshwa mjini kunihusu

Mboka epanzi ngai sango eh
Majungu yanaendeshwa mjini kunihusu

Balobi, akoti lopitalo eh
Wanasema nipo hospitali

Balobi, ba moni ye na Ngaliema eh
Wanasema nimeonekana Ngaliema eh (Ngaliema ni hospitali kubwa Kinshasha)

Balobi, akende Bruxelles oh
Wanasema nimekwenda Brussels (Kwa matibabu)

Balobi, ba moni ye na Anvers oh
Wanasema nimekenda Anvers oh (Anvers ni moja ya hospitali kubwa Brussels)

Balobi, akende Paris eh
Wanasema nimeenda Paris

Balobi, ba moni ye na Geneve
Wanasema nimeonekana Geneva

Balobi, akende na America eh
Wanasema nimeenda America eh

Parti Etat, efuteli ye ticket oh
Amepata tiketi ya kuondokea oh

Balobi, akende Paris eh
Ameenda Paris eh

Balobi, ba moni ye na Geneve
Ameonekena Geneva

Balobi, akende na America
Amekwenda America

Parti Etat, efuteli ye ticket oh
Amepata tiketi ya kuondokea oh

Verse 1
Swela obota ngai, ngai makila mabe maman
Swela ulinizaa, nilizaliwa na damu mbaya (akimaanisha mikosi)

Ebele ya bato oyo, ba lingi ngai te
Watu wengi hawanipendi

Lelo na moni na miso maman
Leo nimeona kwa macho yangu

Nasala nini mokili
Nitafanya nini ulimwenguni

Zairois alingaka se na tango ya bisengo eh
Wazaire wanakupenda wakati wa raha (bisengo ni raha)

Malade ba kangi yo
Ukipata maradhi yo (malade ni maradhi)

Akomi ko seka yo eh
Wanaanza kukucheka eh (Koseka ni kucheka)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…