Wazurulaji wanaolengwa kukamatwa na RC Makonda ni akina nani?

Wateja wa biashara mbalimbali utawatofautishaje na wazurulaji!
 

Ngoja CORONA imtembele hakika atakaa kimyaa
 
Kwahiyo mnataka kusema tatizo ni msambwanda..?
 
RockCarnegie,
Sisi huku kwanza wazurulaji tumeanza na wanafunzi walioondolewa shuleni wakarudishwa nyumbani. Wanafunzi hawa wamedhani wako likizo hivyo kushinda mitaani wanarandaranda. Kundi hili halitoki kutafuta rizki mitaani bali wapo mitaani wakitembea kwa mafamba huku na kule. Tumewaelekeza wasalie nyumbani wasaidie wazazi wao shughuli za hapa na pale pamoja na kujisomea ili kupunguza msongamano.

Pili, mikusanyiko ya watu wazima isiyo ya lazima. Watu wanaenda hospitali kumuona mgonjwa mmoja hiyo 6:30-8:00, hao nao ni wazururaji. Ili kuepusha msongamano, aende mmoja apeleke mahitaji basi.

Kwenye maeneo ya magulio, mama anaenda na kichanga cha miezi minne; hao haturuhusu. Pia msongamano hospitalini hasa kwenye clinic za watoto haturuhusu nao ni uzururaji.

Ieleweke kuwa uzururaji unaoelezewa kwa janga hili ni tofauti na ule uliozoeleka, huu una tafsiri pana zaidi na lengo kuu ni kupunguza msongamano wala hauhusu kazi. Kama kuna kazi waweza kufanya bila kuchangamana na makundi ya watu wengi fanya hivyo.
 
Hao wanaoamka wakiwa hawana ramani ya kazi ndio hao wanaoishia kusimama sehemu moja watu wengi na kutengeneza mazingira ya corona kusambaa kirahisi.

Ukienda pale Makumbusho utaona makundi ya watu wamejikusanya, wanachokifanya ni kuyajadili maumbo ya wanawake na kuchora ramani za wizi. Ni rahisi sana ugonjwa kusambaa kwa aina ile ya mikusanyiko isiyo ya lazima.
 
Mkiwakamata mtawapeleka wapi?
Huko vituoni si kutajaa na kutakuwa na msongamano
Naona sahv Hao wazurulaji muwapeleke mabibo hostel

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa akiwa kamata atawapeleka wapi wakati serikali imetoa maelezo kwa polisi, mahakana na magereza kutoa dhanana kwa makosa yanayo dhaminika bila usumbufu ili kupunguza msongamano mahabusu na magerezani kama sehemu ya kukabiliana na korona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy hana tatizo tatizo lipo kwa baba amemdekeza mno mtoto wake kuna siku atakuja kumvuta msuli ndipo ataona madhara ya kudekeza
Hamaanishi lolote cha msingi Fanya unaloona sahihi
Hivi unajua huyu jamaa hanaga kumbukumbu ya anavyovisema.
Tatizo ni hao akina Ummy mwalimu wanaompaga nafasi ya kusalimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…