WB Yaikopesha Tanzania Bilioni 284 Za Kuimarisha Jinsia na Kukabilina na Ukatili

WB Yaikopesha Tanzania Bilioni 284 Za Kuimarisha Jinsia na Kukabilina na Ukatili

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Mara zote naunga mkono Serikali kukopa na Kwa kweli Iendelee kukopa Kwa sababu Nchi zote zilizoendelea zinakopa sana.

Hoja ni aina gani ya mikopo? Mikopo ya dizaini hii sikubalini kabisa.

Aliyeelewa jinsi huo Mkopo utatekekeza hayo mambo anisaidie.👇👇

---
Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB) wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104, sawa na takriban shilingi bilioni 248, kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia nchini Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”

Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete.

Akifafanua kuhusu mikataba hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa mkataba wa dola za Marekani milioni 4, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9.5 ni msaada na Mkataba wa dola za Marekani milioni 100, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 238 ni mkopo wenye masharti nafuu.

Amesema mradi wa PAMOJA uliosainiwa una nia ya kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar.

My Take
Mikopo ya hivi sijui nani Huwa anashuri na kuipitisha.
Kuna maeneo hayana Barabara za Mikoa kwa Mikoa badala tukopee miradi tunakopea posho,duu kazi ipo.👇👇

I stand to be corrected.
 
Hapa wanadai ni sawa na Ile ya fanco phone countries,yaani Kuna deni tunalipa huko duniani Mana wazungu waliondoka kwa masharti kuwa lazima tulipwe tulichotengeneza la sivyo tunavunja ndipo tuondoke.
So Kuna Siri kubwa huko juu mpaka ufikepo ndipo uyajue.
Sie ni watumwa mpaka milele kwa Hawa jamaa weupe.
Madini wanachukua kufidia gharama za ukoloni Mana walijenga shule ,kanisa,roads nk
Jpm alisema kuwa Kuna miktaba ya OVYO

Mlijua anatania. Yaani ukiwa na roho ya ubinadamu huwezi kuwa kiongozi wa nchi hii cheki wote wanaotetea wananchi hawadumu ama tuanze kuwaorodhesha.
 
Mara zote naunga mkono Serikali kukopa na Kwa kweli Iendelee kukopa Kwa sababu Nchi zote zilizoendelea zinakopa sana.

Hoja ni aina gani ya mikopo? Mikopo ya dizaini hii sikubalini kabisa.

Aliyeelewa jinsi huo Mkopo utatekekeza hayo mambo anisaidie.👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/DDezmT7NXpU/?igsh=MXhsOTVicXMxeXNidg==
My Take
Mikopo ya hivi sijui nani Huwa anashuri na kuipitisha.
Kuna maeneo hayana Barabara za Mikoa kwa Mikoa badala tukopee miradi tunakopea posho,duu kazi ipo.

I stand to be corrected.
 
Rafiki yangu umekuwa balozi mzuri wa kumpamba mama Samiah lakini kuna siku utakuja kujutia sana kuliko ulivyoshtuka sasa.
Mara zote naunga mkono Serikali kukopa na Kwa kweli Iendelee kukopa Kwa sababu Nchi zote zilizoendelea zinakopa sana.

Hoja ni aina gani ya mikopo? Mikopo ya dizaini hii sikubalini kabisa.

Aliyeelewa jinsi huo Mkopo utatekekeza hayo mambo anisaidie.👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/DDezmT7NXpU/?igsh=MXhsOTVicXMxeXNidg==
My Take
Mikopo ya hivi sijui nani Huwa anashuri na kuipitisha.
Kuna maeneo hayana Barabara za Mikoa kwa Mikoa badala tukopee miradi tunakopea posho,duu kazi ipo.

I stand to be corrected.
 
Sijaona kama kulikuwa na ulazima wa mkopo huu mh waziri wa fedha, kuna vitu vingi sensitive zaidi ya hilo tunaweza kuvikopea... kama nchi sidhani kama tumekosa pesa ya kupambana na masuala ya ukatili, maana suala la ukatili linaanzia kwa viongozi wa chini kabisa hadi viongozi wa ulinzi na usalama, na wanalipwa kwa kazi hiyo (wakuu wa wilaya) n.k... Huu ni sawa na mkopo bubu, wamekopa hela za kulipana posho kwenye zile kampeni bubu.
 
Serikali inekosa dola milioni 4 kweli mpaka ikope?
Huwa naona kwenye Bajeti wanasema wazi kiasi watakachokopa ila hawasemi watakopa specifically Kwa Ajili ya nini.

Labda Mwigulu atueleza kama Jinsia ni gia ya kupatia hela ila zitafanya miradi ya maana vinginevyo wanatuaibisha na sio sawa.
 
Dola milioni 4 ni mkopo wa mfanyabiashara mtu binafsi, si mkopo wa nchi.
 
Nimeona Mwigulu anakenua meno kukopeshwa amepata fedha za kulipana posho na kununua V8, hii nchi tunaongozwa na watu wa ajabu sn, kwa rasilimali tulizonazo kweli mtu mwenye akili timamu anaweza kwenda kukopa?
 
Back
Top Bottom