Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Ukiambiwa Harmonize alikuwa amesainiwa kwa miaka 15 masikio yatapokea hiyo sauti lakini akili itakataa kuamini au kuelewa hicho ilichopokea toka masikioni. Yani mkataba wa kazi wenye muda wa MUONGO NA NUSU? Tungekuwa ulaya tungeuita ni "CONTRACT FROM HELL".
Tuseme alisainiwa ana miaka 20, ina maana mpaka anafikisha miaka 35 lazima awe chini yao. Hapo katikati akiwa na miaka 22 mpaka 30 ndio muda wa kupiga kazi kwa nguvu na kutengeneza future yake. Sote tunajua lifespan ya soko la muziki huwa ni ndogo, huwezi kuwika zaidi ya miaka 10. Usipotumia muda vizuri ndani ya miaka hiyo basi ishakula kwako.
Kibaya zaidi boss wao pia anafanya kazi ileile ya kuimba, na hawezi kukubali hao alowaajiri wampite. Kwa maana hiyo msanii hawezi fikia ile maximum peak yake kwa sababu yuko limited na masharti ya kutompita boss wake.
Mikataba ya namna hii ni mibovu kwa sababu inamgeuza msanii husika kuwa mwajiriwa wa lebo husika. Yani mkataba unakuwa haumruhusu kujiendeleza yeye kama yeye bali kuiendeleza lebo.
Hii inafanya kama mko wengi kwenye lebo wote mbweteke na kuondoa ushindani na ubunifu kwa sababu hata ufanye kazi kwa bidii vipi mafanikio yote inabeba lebo wewe unabaki ni ile % mloandikiana tu.
Pia hii inaleta mgongano wa kimaslahi kwenye lebo kwa sababu anayefanikiwa ataona kama wenzie wanamnyonya jasho lake.
Ndani ya WCB bosi mmojawapo ambaye ni Diamond Platnumz pia ni msanii. Kwa hiyo kusainiwa pale ni kama mchezaji kucheza na kocha wake uwanjani na wote wanataka kila mmoja afunge. Yani ni sawa na wewe uajiriwe kwenye kampuni halafu baadae ufungue kampuni kama ile uloajiriwa. Lazima mchukiane na boss kwani hatopenda kupitwa hasa akigundua unampiku mbinu za kibiashara.
Ndio maana vijana wa WCB wamepigwa pini hakuna kumpita boss wao DP.
Katika dunia ya sasa ni ujinga wa hali ya juu kusaini wasanii kwa kufuata mfumo wa miaka. Wenzetu waliondelea wanamanage kazi za wasanii hawamanage wasanii. Yani the more unavyopiga kazi kubwa na kutoa kazi kali kali ndio unajikuza wewe sio lebo yako.
Sasa hapa bongo eti unawasaini wasanii na kuwalipa mshahara kwa mwezi, unawatafutia na nyumba za kupanga na ki-premio cha 10M ili kuwazuga.
Ndio maana kazi za WCB zikitoka wanaipigia promo weeeeh, mpaka kwa kutumia kiki za ajabu ajabu zinazokinzana na maadili yetu ili tuu kuipa nguvu kazi yao. Lakini unakuta hiyo kazi haivuki hata mpaka wa Namanga pale.
Ndio maana tumeshuhudia hata Diamond mwenyewe akiporomoka kwenye soko la muziki Afrika. Hapati nominations tena kwenye tuzo mbalimbali sababu hakuna kipya alichonacho kulinganisha na mwanzo alivyokuwa anafanya kazi kwa kujituma.
Yani mikataba ya lebo za muziki tanzania haina tofauti na ule mkataba wa bandari ya bagamoyo. Kwa hali hii sijui sekta gani itapiga hatua kwa haraka Tanzania kama urasimu wa mikataba umekamata sekta zote[emoji24][emoji24][emoji24]