WCB na mikataba ya ajabu: Ndio maana muziki wa Tanzania hauendelei

WCB na mikataba ya ajabu: Ndio maana muziki wa Tanzania hauendelei

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Ukiambiwa Harmonize alikuwa amesainiwa kwa miaka 15 masikio yatapokea hiyo sauti lakini akili itakataa kuamini au kuelewa hicho ilichopokea toka masikioni. Yani mkataba wa kazi wenye muda wa MUONGO NA NUSU? Tungekuwa ulaya tungeuita ni "CONTRACT FROM HELL".

Tuseme alisainiwa ana miaka 20, ina maana mpaka anafikisha miaka 35 lazima awe chini yao. Hapo katikati akiwa na miaka 22 mpaka 30 ndio muda wa kupiga kazi kwa nguvu na kutengeneza future yake. Sote tunajua lifespan ya soko la muziki huwa ni ndogo, huwezi kuwika zaidi ya miaka 10. Usipotumia muda vizuri ndani ya miaka hiyo basi ishakula kwako.

Kibaya zaidi boss wao pia anafanya kazi ileile ya kuimba, na hawezi kukubali hao alowaajiri wampite. Kwa maana hiyo msanii hawezi fikia ile maximum peak yake kwa sababu yuko limited na masharti ya kutompita boss wake.

Mikataba ya namna hii ni mibovu kwa sababu inamgeuza msanii husika kuwa mwajiriwa wa lebo husika. Yani mkataba unakuwa haumruhusu kujiendeleza yeye kama yeye bali kuiendeleza lebo.

Hii inafanya kama mko wengi kwenye lebo wote mbweteke na kuondoa ushindani na ubunifu kwa sababu hata ufanye kazi kwa bidii vipi mafanikio yote inabeba lebo wewe unabaki ni ile % mloandikiana tu.

Pia hii inaleta mgongano wa kimaslahi kwenye lebo kwa sababu anayefanikiwa ataona kama wenzie wanamnyonya jasho lake.

Ndani ya WCB bosi mmojawapo ambaye ni Diamond Platnumz pia ni msanii. Kwa hiyo kusainiwa pale ni kama mchezaji kucheza na kocha wake uwanjani na wote wanataka kila mmoja afunge. Yani ni sawa na wewe uajiriwe kwenye kampuni halafu baadae ufungue kampuni kama ile uloajiriwa. Lazima mchukiane na boss kwani hatopenda kupitwa hasa akigundua unampiku mbinu za kibiashara.

Ndio maana vijana wa WCB wamepigwa pini hakuna kumpita boss wao DP.

Katika dunia ya sasa ni ujinga wa hali ya juu kusaini wasanii kwa kufuata mfumo wa miaka. Wenzetu waliondelea wanamanage kazi za wasanii hawamanage wasanii. Yani the more unavyopiga kazi kubwa na kutoa kazi kali kali ndio unajikuza wewe sio lebo yako.

Sasa hapa bongo eti unawasaini wasanii na kuwalipa mshahara kwa mwezi, unawatafutia na nyumba za kupanga na ki-premio cha 10M ili kuwazuga.

Ndio maana kazi za WCB zikitoka wanaipigia promo weeeeh, mpaka kwa kutumia kiki za ajabu ajabu zinazokinzana na maadili yetu ili tuu kuipa nguvu kazi yao. Lakini unakuta hiyo kazi haivuki hata mpaka wa Namanga pale.

Ndio maana tumeshuhudia hata Diamond mwenyewe akiporomoka kwenye soko la muziki Afrika. Hapati nominations tena kwenye tuzo mbalimbali sababu hakuna kipya alichonacho kulinganisha na mwanzo alivyokuwa anafanya kazi kwa kujituma.

Yani mikataba ya lebo za muziki tanzania haina tofauti na ule mkataba wa bandari ya bagamoyo. Kwa hali hii sijui sekta gani itapiga hatua kwa haraka Tanzania kama urasimu wa mikataba umekamata sekta zote[emoji24][emoji24][emoji24]

Screenshot_20190825-215746.jpeg
 
Ndio leo kausoma huo mkataba kauelewa kwani? siku zingine ilitumika ki spanish kwenye huo mkataba? Amepata wa kumtafsiria sio?

Kama anaondoka aondoke kwa amani,kujitetea kwa ujinga kama huu hakumfanyi apande juu ila ataonekana Punguani alie elimika after get into relation with sarah na huyo jembe ni jembe.
 
Mbona povu mkuu?

Ndani ya mwaka hata diamond hawezi kuona ndani kwa harmonize iwe kwa music ama kiki labda hela tuu, kam story nilizopata kwa chanzo kinachoaminika zikiwa za kweli...waliloga morogoro msenge kaenda kuloga chitoholi kosa visa nikose visa maaamae
kama akimzidi kwa hela..kuna nini hatomzidi?
 
We jamaa una matatizo au uko nyuma sana hilo mbona linajulikana toka wanatoa ngoma ya Aiyola wewe ulikuwa bado uko Nyangwinde?
.
Mikataba kama hii wala si ya kwanza sikutukani umechelewa sana kuja mjini 2pac shakur alisaini mkataba wa maisha, Dr dre pia alisaini mkataba wa maisha kabisa 2pac huko aliko anajua kilichompata baada ya kuleta ujuaji. (R.I.P)
.
Hata hivi sasa una habari Kanye west ana mkataba wa maisha wa kufanya kazi ya muziki bila kuacha?
 
But hao wanajiongeza wana ngoma nyng sana zpo studio hata wakifa utasikia daily nyimbo zao znakua znatambulishwa ila kibongo bongo sidhani
 
We jamaa una matatizo au uko nyuma sana hilo mbona linajulikana toka wanatoa ngoma ya Aiyola wewe ulikuwa bado uko Nyangwinde?
.
Mikataba kama hii wala si ya kwanza sikutukani umechelewa sana kuja mjini 2pac shakur alisaini mkataba wa maisha, Dr dre pia alisaini mkataba wa maisha kabisa 2pac huko aliko anajua kilichompata baada ya kuleta ujuaji. (R.I.P)
.
Hata hivi sasa una habari Kanye west ana mkataba wa maisha wa kufanya kazi ya muziki bila kuacha?
Tupac alisaini mkataba wa maisha na lebo gani mkuu?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu nzuri.

Tupac alisaini mkataba wa miaka 3 tuu.

images-3.jpeg
 
Nakala ya mkataba ipo wapi au hisia?

Drake yupo YCMB zaidi ya miaka 10 ,Kanye West yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z zaidi ya miaka 10,Emininem yupo chini ya label ya Dr Dree zaidi ya miaka 20 kwa hiyo mimi sioni ajabu.

Mimi naona swala la Harmonize,tuliache muda utaongea ,maanake hizi nyingine ni Chai tu.
 
Tupac alisaini mkataba wa maisha na lebo gani mkuu?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu nzuri.

Tupac alisaini mkataba wa miaka 3 tuu.

View attachment 1190063
Ndio maana nilikwambia umechelewa sana kuja mjini, unaniita muongo wakati hujui lolote.
.
Nilikuwa najaribu kukupa tu taarifa kuwa mikataba ya wasanii wote wa Wasafi inajulikana na ni 10 years kila mmoja isipokuwa dada mtu na wala sio 15 yrs.
.
2pac amar shakur alichapwa risasi na BIG Notorious akalazwa baadae akabambikwa kesi ya ubakaji Suge Knight akaingilia kati baada ya mshikaji kuhukumiwa akamtoa jela na kumpa mkataba wa maisha kufanya kazi chini ya lebo yake.
.
1996 akaanza kuleta ujuaji hadi kuanz kuvaa vyeni vyenye kutambulisha he's own coming music label yani baada ya kuanza vile tu hakuchukua muda (R.I.P) king.
.
Sasa wewe unaleta hizo forged contract za kishamba suge Knight bado yu hai na ashaongea sana kwenye interviews mbalimbali tafuta interview yake ya mwisho kafanya kwenye kipindi cha Power breakfast huko (U.S).
.
Nimekuuliza na swali je unajua Kanye west ana mkataba wa kufanyia watu muziki maisha yake yote?
.
Unajua Rihanna atatamba huko kotee ila Rock nation atarudi tu?
 
Dunia ipi unayoizungumziwa ww

Watu wanapewa mikataba ya maisha we unaona ajabu miaka 15 tu

Afu usitake niaminisha kwamba kunamtu yupo WCB anaweza fanya vizuri zaidi ya diamond.hata nje ya WCB labda unitajie ww na hv kati ya mond na harmo nan anacollable nyingi za nje kuliko mwenzie? Ingekuwa kubaniwa hzo collaboration nani angeziruhusu ikiwa bosi hapendi msanii yeyote awe juu yake.

Alafu pia kumbuka nje ya lebble ya WCB harmonize alikuwa na Manager wake.
 
Back
Top Bottom