WCB wamewekeza Sana ni halali Yao kuvuna walichokipanda

Bro we ni kaka mimi..by that time 200 Nenda kamwambie sikuwahi kuielewa..ila 2010 ile Mbagala daaaah...halafu badae ukimuona ndo akaua...Mpaka sasa nyimbo zangu 3 bora kutoka kwa jamaa ni Ukimuona, Mbagala na nitarejea..ANAJUA.
Moyo wangu ndiyo umetoka nikiwa mwaka wa pili, nenda kamwambia nadhani sijui nilikuwa nasubiri kwenda chuo au nilikuwa nimemaliza form six. Maana wakati ulipotoka baadae kidogo ikaja sumu ya penzi. Ila hapo Mzee kiba alikuwa ashatisha sana na mangoma kama Nakshi mrembo, na ile album yake ya cinderella ilikuwa moto wa kuotoea mbali. Conderella inatoka illikuwa nadhani 2006 mwishoni au 2007, nikiwa najiandaa kuingia kidato cha tano. Hapo Cinderella ikawa inapambana na wimbo wa Marlaw bembeleza halafu na mpenzi jini kwa mbali.
Sasa nimeanza kugundua kuwa nimezeeka aisee
 
Huyu bwana sio mshabiki wake kabisa, lakini sio yeye tu Bali mi sio mshabiki wa aina fulani ya mziki, ila wimbo wa diamond I miss your niliuelewa mno.
 
Wimbo wa Marlow bembeleza enzi unatoka nilikuwa la 7 mwaka 2007..mkuu umeshakuwa comred sasa
 
mm mkongwe mwenzio nakukumbusha tu, kuwa sumu ya penzi inatoka bado diamond hajulikani
 
mm mkongwe mwenzio nakukumbusha tu, kuwa sumu ya penzi inatoka bado diamond hajulikani
Kama zilipishana hazikupishana miezi kibao sikumbuki upi ulitangulia kutoaka ila ilikuwa mwaka huo huo nadhani. Ila nilidhani Diamond ni msanii wa msimu na Belle atakuwa mkubwa sana. Nenda kamwambie sikuwahi kuolewa huo wimbo kabisa. Nilianza kumuelewa alipotoa mbagara, nitarejea sikuuelewa sana nilikuja kuelewa moyo wangu, kizaizai , mawazo ila hapo sasa nilikuwa nimekwisha kugundua tayari huyu kijana ni moto wa kuotea mbali.
Belle kwa upande mwingine kila ngoma yake na collabo aliyofanya niliikubali kuanzia ngoma yake ya masogange, we ni wangu, collabo yake na sheta, na nyingine.
Ni kama juzi kumbe zaidi ya miaka 13 iliyopita vile kweli wakati unaenda mbio
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Wakati tunahitimu kidato cha nne personally ya P square ndo ipo kwenye chati, mi na mwanangu mmoja tulifanya unyama sana hadi ma-madam wakadata maana hawakuamini kijana mkimya na mpole kama mimi angeweza kufanya vile. Yaani walishoboka kiasi nikatamani niwengekuwa mkubwa ili niwale.

Ila bado sijakata tamaa, kuna mmoja namuwinda.
 
Moyo wangu mi nafkr niko kazini miaka ka 5 hivi.
Lakin Mbagala ndo ulianza au Moyo wangu?
 
Shikamoo daa, itakuwa mbagara. Maana Moyo wangu ulipotoka ni kama vile alibadilika akatengeneza kwaito
Marahaba mdogo wangu.
Mbagala ndo ilikuwa hit song, namkumbuka vizur na skafu yake shingoni.

Moyo wangu ilikuwa pamoja na Nimpende Nani, na hizo kina Number 1 sijui Ntampata wapi kama yule.
Huyu dogo ,Sikh ya kwanza namskia nilikiwa shabiki yake , na 15 yes later nimebaki kuwa shabiki yake.
Ana namna ya tofauti ya kufanya sanaa.
Kuanzia nyimbo , mashairi, lifestyle, now the label.

Kila kitu tu utamzungumzia kokote kwenye burudani.
Labda tu iwe mbishi wa uhalisia.
 
Sure, ninakubali sana hustles zake jamaa ameanza tunamwuona anapanda tunamuona. He is ambitious
 
Nilipokuwa nasoma mwandiko wako Tu nilijua wewe ni rika langu [emoji16]..lkn Mimi nahisi ni mkubwa kwako [emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…