Kama zilipishana hazikupishana miezi kibao sikumbuki upi ulitangulia kutoaka ila ilikuwa mwaka huo huo nadhani. Ila nilidhani Diamond ni msanii wa msimu na Belle atakuwa mkubwa sana. Nenda kamwambie sikuwahi kuolewa huo wimbo kabisa. Nilianza kumuelewa alipotoa mbagara, nitarejea sikuuelewa sana nilikuja kuelewa moyo wangu, kizaizai , mawazo ila hapo sasa nilikuwa nimekwisha kugundua tayari huyu kijana ni moto wa kuotea mbali.
Belle kwa upande mwingine kila ngoma yake na collabo aliyofanya niliikubali kuanzia ngoma yake ya masogange, we ni wangu, collabo yake na sheta, na nyingine.
Ni kama juzi kumbe zaidi ya miaka 13 iliyopita vile kweli wakati unaenda mbio