Lara mdogo wangu mziki wa bongo flava is a very complicated yaaani kuna kitu kinaitwa System ndio ambayo ilikuwa ina control the music for the last decade...
hiyo system ilikuwa inacontroliwa na baadhi ya watu ambao siwataji sasa hivi kwa sababu zangu binafsi..
hao watu ndio waliowaondoa kwenye ramani kina nature, sugu, jay, na kwa taarifa yako hao watu walitaka kumuondoa kwenye ramani diamond baada ya kuhitilafiana nao baadhi ya mambo...
na ndio wakamwingiza mtu fulani wa kum replace ila sema sasa kwa dimond wamefeli...
so they speak lugha ya diamond
hivi unajua kuna kituo fulani cha redio mjini hapa hakipigi nyimbo ya diamond kwa miaka kadhaa sasa hivi?
why??
jiulize
tuje issue ya kina nature unajua kuwa kuna watu wa enzi zetu hatuwaelewi kina nerdy, rayvanny, harmonize na wenzake
sie tunawaelewa kina nature, jay, doro, kr, na kina fanani... tunamiss watu hao na yes tukirudishiwa watu hao tutanunua kazi zao na tutakwenda kwenye shoo zao ndio maana mdogo wangu katika biashara kuna kitu kitu kinaitwa market segmentation wewe na wavaa supra msipoenda kwenye shoo za kina nature, msiponunua kazi zao jua kuna watu watataka kazi zao na kuna watu wanazimiss...
daimond anataka kufanya kitu kama hicho....
na hata kwenye record label kubwa duniani mfano hizo ulizotolea mfano umetolea mfano cashmoney
je unajua walimsign msanii Mysticak ambaye hakutoa nyimbo yeyote tokea 2001 album yake ya mwisho iliyoitwa Tarantula na around 2011 cashmoney walimsign ?
unajua kwanini market segmentation strategies
hao hao cashmoney wamemsign paris hilton wewe nyimbo za paris hilton hata moja unaijua?? huijui kwanini?? sio taste yako ya msanii na huyo paris hilton mara ya mwisho kutoa album ni mwaka 2006 ambapo aliitoa self titled album
umeongelea issue ya age eti juma nature ana 40 hawezi ku dub Atlantic Records sio wapumbavu kumsign Phil Collins kizee cha miaka 69 na kina Tony braxton,Missy Eliot wakati wao wana wasanii kama kina gratitude, King Floyd, Jojo, washkaji zangu matchbox twenty na etc unajua kwanini?
Market Segmentation why?? wanajua kabisa kwa vijana wa 20s watanunua kazi za kina paramole, wauza unga na ma negro watawasikiliza kina maino na lupe fiasco, wadada wa miaka 30s manegro watamsikiliza missy eliot, wazee wa 50s,kwenda juu Phill collins ofcourse
Hivyo hivyo kwa Capitol nao sio wajinga kuwa na vizee Red Hot Chilli Papper , Chingy, Dilated People, Faith Evans, Foo Fighters, Ice Cube wakati wana vijana kama kina Bastile, Alter Bridge, Coldplay na wengine wengi
tena hawa capitol ndio wanachekesha Frank Sinatra amefariki siku nyingi lakini mkataba wake bado wanau renew kila ukiisha wana sign a new contract why?
mwaka 2012 wamesign kuwa ndio wasimamizi wa kundi la the beatles worldwide wakati ni kundi ambalo hali exist anymore are they stupid?? no my dear they are very clever more than you think..
hao Red Hot chilli paper katika billboard katia Billboard album yao mpya hii kuna nyimbo inaitwa Dark Neccessities ile kuingia tu inapanda fasta sana kuelekea chati za juu wiki hii imekuwa ya nane wiki iliyopita imekuwa ya 10 hapo maana yangu stressed out ya 21 pilots inashuka kwa kasi sana so wazee ni wazee tu naona madogo wanawapisha wazee
Hitimisho langu ni hili kuna tatizo kubwa sana kwenye MEDIA za Tanzania hasa watangazaji wa vipindi vya burudani wanaujua mziki kidogo sana yaani wana cycle ndogo mno katika kuujua mziki
mtu ambaye anaujua mziki pekee ni massoud massoud ila hawa wengine hawa hamna kitu east africa wana kipindi chao cha gheto wanasema wanapiga nyimbo za nje ila wao utakuta wanapiga nyimbo za naigeria nje ya afrika watampiga drake, tyga, fetty wap, wamemaliza ukiwauliza unawajua bastile, awolnation, avicii, hozier, foster the people wanabaki wametoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango Queen FIFI anajitahidi lakini sio kwa kiwango kikubwa baado sana amebase sana kwenye trap music
xxl ya clouds fm kule ndio ushuzi mtupu wasipopiga all the way up ya fat joe wanahisi bado hawajapiga nyimbo Kennedy the remedy ndio khaaaaa kuna siku mtu aliomba nyimbo ya neck of the woods ya birdman ft lil wayne eti yeye akamrekebisha akasema nyimbo inaitwa uptown Kumbe yeye ndio kakosea nyimbo inaitwa neck of the woods
haya kina mamy na adam mpaka leo hawajui kuwa major lazer ni KUNDI wao wakipiga nyimbo ya major lazer wanasema eti huyu jamaa anaitwa major lazer wanashindwa kuelewa major lazer ni kundi la kina diplo na jillionaire
huu upeo mdogo wa media kuchagua wasanii wa kuwapiga ndio kunawafanya wasanii wengine nyimbo zao zisiwe zinaonekana Tanzania sana
leo hii watu wanamjua Tekno kuliko Hozier, leo hii Tanzania watu wanamjua yemi alade kuliko Kelly Clakson, watu wanamjua AKA kuliko 21 pilots, watu wanawajua dbanji kuliko Skrillex watu wanamjia wizkid kuliko Avicii na mie wala siwashangai ni kwa sababu media zetu zimewafanya hao watu wawe maarufu kuliko hawa
ile nyimbo ya homecoming ya kanye west ft cris martin watangazaji fulani walisema kanye west kamshirikisha undergroud chris martin wakati chris martin ni superstar kuliko kanye west
bob ft hailey williams nyimbo ile ya airplane watangazaji fulani nao wakasema bob kamshirikisha undergroud yaani wamesahau kuwa hailey williams ni superstar kuliko B.o.b au hawakuwa wanajua masikini
so hilo ndio tatizo tunalili face sasa hivi
anachokifanya DIMOND ni kitu ambacho label zote kubwa duniani unazozijua wewe zinafanya alichofanya WCB ndio Interscope wamefanya kumsign MADONA na bado wana SERENA GOMEZ
ndicho walichokifanya Columbia kumsign Celine Dion wakati wana kina Katharine Macphee
ukistaajabu ya diamond na WCB utayaona ya MERCURY records kuwa sign U2 wakati wana Justin Bieber