WCB Wasafi kusaini wasanii wapya wawili, mashahidi wao watatoka BASATA na COSOTA

WCB Wasafi kusaini wasanii wapya wawili, mashahidi wao watatoka BASATA na COSOTA

Cosota na Basata nao watakuwa hawaja uwelewa?Manake pale wanasheria wapo.

Ila naona wana discuss mikataba ya label ya WCB, ila wanasahau za label nyingine, hapo ndipo unapojua chuki zao kwa WCB wamezificha kwenye mikataba.

Cha ajabu hao wanaolalamikiwa kunyonywa wapo vizuri kuliko wasanii wa label nyengine, cha ajabu hawajiulizi why wasanii wa WCB wapo vizuri kuliko wengine.
Hii nchi ina watu wa ajabu kinoma na ndio maana no wonder ni moja ya nchi za watu maskini duniani,watu wamejaa husda na chuki zisizo na msingi na hata wasanii wanaojitoa WCB wanajua hili ndio maana wakitoka wanaanza kutafuta public sympathy kwa watu wenye husda na WCB hili waendelee kuhit..

Mtu kama Harmonize point yake sijui ni nini mara aseme alikuwa ameridhika na asilimia 40 za Wcb ila kilichomuondoa ni figisu za kina Sallam mara tena aseme ananyonywa na mkataba alisaini mwenyewe yaan fujo tupu,label kubwa duniani hasa zile zinazomilikiwa na Universal(Universal inamiliki zaidi ya asilimia 98 ya soko la music zikiwemo label kubwa za music kama Def Jam ma interscope records na nyinginezo) huwa zinatoa around asilimia 13 mpaka 28 za mapato kwa wasanii aheri asilimia 40 za wcb na mikataba huwa ni ya maisha, utakuta msanii marekani anamilikiwa na label tano moja inahusika na publishing,nyingine recording let say na zote zinamkata asilimia za production hiyo ndio dunia ya kibepari inavyoenda
 
Ndio hivyo lebo imechuja lakini inasain wasanii wapya wawili nchi nzima inawasubiri wasanii wa lebo iliyochuja
Tuibie siri ya kambi mwana, ni ma underground au maarufu hao wasanii wawili? Au na wee insider unasubiri suprise kama sisi?
 
Sasa ukipambana mwenyewe utapata lini billion 1 [emoji23][emoji23][emoji23] wakati Wasafi wakikunyonya kwa miaka 5 tu billion moja hii hapa na biashara kadhaa ziko zina operate. Jina kubwa sokoni
Akili mtu wangu
 
Wapunguze muda wa mkataba.

Miakataba ya miaka mingi ni mikataba ya kikoloni.

Kibiashara mkataba usizidi miaka 5
Biashara ya mziki sio kulima,unaweza ukampa miaka mitano na ndani ya miaka mitano akawa hajarudisha kitu.

Hivi ww unavyo ona leo hii Cheed,Killy,K2GA nk wakikamilisha miaka 5 watakuwa tayari washarudisha hela?

Kwenye mikataba kuna security hata uoande wa mwekezaji, huko kwenye madini kwenyewe tunachopata hakivuki 30% na hapo unaweza ukakuta wana miaka kama kumi wamechimba kwa bila kulipa gawio wala kodi, ili kurudisha hela yake ya uwekezaji.
 
Fafanua mkuu
Waliingia mkataba wa muda mchache na Rosa lee wa miaka kama 2 kilichotokea ni kwamba ile pesa waliowekeza haikurudi ndani ya hiyo miaka baada ya huo msanii mkataba wake kuisha mwisho wa siku Navykenzo wakala hasara kitu ambacho Wasafi hawataki kukifanya maana uwekezaji wao ni mkubwa Sana wakisema wamsign msanii kwa miaka michache return yao itarudi vipi?
 
Back
Top Bottom