WCB Wasafi wamebaki wakiwa..Tatizo ni nini?

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Kwa wasiofatilia mambo wanaweza shangaa naposema WCB wamebaki wakiwa. Yes, sababu awajawai toka kwenye public na kukiri haya mambo nayoenda kuyasema hapa.


Ni wazi kama utafanya tafiti yako ya uongo na kweli utagundua media zote kubwa za bongo zimesusa kupiga nyimbo za WCB iwe Tv na Radio.

Mwanzoni WCB walikuwa na mgogoro na EATV lakini kwa sasa unazidi kuenea si Clouds media wala EFm kote awachezi nyimbo za Wcb.

Ata supporters wao wakubwa na wenye ushawishi kwenye mitandao especially tweeter na Instagram wamewapotezea.

Inawezekana yote haya yanatokea sababu watu wanaona kijicho na mafanikio ya Wasafi lakini pia haya yanaweza kutokea sababu mapungufu yaliyopo WCB.

Kwa sasa WCB ni kama ukoo kambale kila mtu ana ndevu.

Nimemskia juzi Tale anatamka hadharani kuwa awatanyenyekea media yoyote itayotaka kuwakwamisha akarudia hiyo kauli mara nne..ilo ni tatizo tayari, awajafika uko wanapodhani wamefika. Wanakuja na Tv yao lakini bado awajafika pale wanapodhani.

Mara nimesikia dansa wa Diamond kawatishia uhai watangazaji wa shilawadu mpaka kuwaumiza. Mpaka sasa uongozi wa wcb awajasema lolote kuonyesha kutounga mkono kitendo hicho.

Nimeona mpiga picha wao anamshambulia mkongwe wa muziki Ray C akimuita marehemu wa muziki.

Na mengine mengi, yote haya yanaonyesha kiburi cha mafanikio kimejaa pale WCB si viongozi mpaka wafagiaji wote nyota zinawaka mpaka wamejisahau wamevimba vichwa wameota mapembe.

Wamesahau msingi mkubwa wa mafanikio ya Diamond mpaka anafika hapo na kuifikisha hapo Wasafi ni UNYENYEKEVU.

Inawezekana kuna mambo wanakumbana nayo yanawalazimu kufikia hatua hii ila lazima waelewe biashara ya Entertainment ni biashara ya kibepari.

Naomba hii timu ijitafakari wakati wanauanza mwaka, kuna kitu hakipo sawa.

Mwl Nyerere alitunga kitabu kinaitwa Tujisahihishe, mkipata nafasi kitafuteni mkisome mtajifunza kitu kuhusu kujisahihisha... Kujisahihisha sio kujishusha.

Mtaenda Hyatt mtaenda Mwembeyanga but you still need media houses & media people.

Ni mtazamo tu, kiroho safi!
 

Sasa km clouds hawapigi nyimbo kisa anaurafiki na Rc. Yaani Ruge anataka adui yake awe adui wa kila MTU. Si utoto huu...Clouds wanataka kumcontrol kil msanii hata Diamond awe chini yao kitu ambacho jamaa hataki. Yaani Ruge anataka kujifanya yeye ndiyo injia wa mziki mjini. One day Yes utashuka tu. Haiwezekani wasanii wawe chini ya Media. Ni ushithole tu.

Majizo hapigi nyimbo za wasafi kisa Diamond alikuwa ana anatembea na mzazi mwenzake.( mobeto). Yaani tena huu utoto mkubwa sana.

EATV wanachuki diamond kitambo sana.. Ugomvi binafsi wa dulla na diamond na ukaongezea hii zaidi. Eatv wanamaind diamond anawadharau. But viblogu vyao uchwala km vya yule sam misago vinamtangaza diamond.

Diamond kushushwa kazi sana..watampunguza nguvu tu but siyo kumshusha.


Ushithole wa Africa haukwepeki na upo kila sehemu. Binasfi huwa siangalii TV za Tanzania zaidi ya azam two taarifa ya habari tu. Mambo mengine IG,jamii forum inatosha
 
MKuu usicheze na Media,Media zina nguvu sana,zinaweza kukushusha na ukapotea kabisa kwenye ramani,utabaki kupigwa kwenye bajaji na bodaboda tu.
 
Mtu akiwa winner sana,wananchi wanapata fatigue nae..WCB is the victim of their own success!

Tatizo sio WCB ni hao wananchi...they are tired now,they want them to loose...Wananchi bwana,sometimes are schizophrenic....halafu always wananchi wanajiona wapo sahihi kumbe wapo delusional tu..get scared of stupid people in large quantities kama wananchi...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miaka michache nyuma kuna siku nilikuwa namsikiliza Guru, rapper wa Gangstarr alikuwa anahojiwa.

Mtangazaji baada ya kumuhoji akamuuliza. Nimesikia una beef na Fifty Cent, tueleze kuhusu hiyo beef.

Guru akawa kama kashangaa, akasema beef gani? Mimi na Fifty tuko poa tu, hatuna beef. Namuheshimu sana Fifty, anafanya kazi nzuri etc.

Guru anavyokandya kwenye nyimbo zake nilikuwa nafikiri angemtukana Fifty.

Na angemtukana ingezia bonge la beef.

Lakini alijionesha kwamba yeye ni OG anayejua "Code of The Street".

Kwanza si kila beef lazima itangazwe na ikuzwe. Kuna vibeef vingine wadau wanakaa chini na kuvimaliza mtaani tu.

Pili hata kama wewe ni OG kiasi gani au matawi kivipi, inakubidi kujua kuishi na watu strategically ili usijiharibie kazi.

Tangu siku hiyo nikamuangalia Guru kuwa si OG tu, bali nibsavvy businesman pia.

Tatizo kibongobongo mtu akishafika level fulani anaona kashamaliza kila kitu.
 

Mkuu Alwatan

Tumekutana tena!

Guru (Keith Edward Elam) alishakufa tangu tarehe 19th April 2010.

Huenda ume-refer interview yake ya kitambo sana,ila ulivyoongea ni kama jamaa yupo hai hivi.

Na pia naomba nikubishie,hakuna documented beef kati ya Guru na 50Cent,naweza kusema umedanganya 100%!

Long story short,kama ni kweli naomba uweke link ya hiyo interview hapa wazi kabisa kuni-prove wrong.Im 100% sure huna hiyo link na haipo!

Thanks
 
SHILAWADU kuna mtu alikula kipigo na jamaa wa wcb? uzi wake upo hapa jf naomba link
 

Mimi na wewe hatukutani. Wewe unanifuatafuata.

Wapi nimesema Guru yupo hai?

Niliposema kuna documented beef ni wapi? Unajua kusoma?

Link unayotaka niweke ni ya nini?

Ulivyoandika ni kama mtu mwenye utapiamlo wa akili ambaye hajui kujieleza.

Unasema hakuna interview ambayo Guru anakataa kwamba hana beef na Fifty au hakuna interview inayoonesha Guru ana beef na Fifty?

Unaelewa kwamba unapoandika "hakuna documented beef" ni kitu tofauti na "hakuna interview kuhusu beef"?

Hii lugha unayoiborongaboronga unaielewa?

One way of spotting an illiterate nincompoop is their liberal use of "100% sure".
 
Mziki wenyewe kiujumla naona kwa sasa umepoa sana show hawapati wasanii vidili dili vya kwend sauth vimepungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…