mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,222
- 4,689
Kwa wasiofatilia mambo wanaweza shangaa naposema WCB wamebaki wakiwa. Yes, sababu awajawai toka kwenye public na kukiri haya mambo nayoenda kuyasema hapa.
Ni wazi kama utafanya tafiti yako ya uongo na kweli utagundua media zote kubwa za bongo zimesusa kupiga nyimbo za WCB iwe Tv na Radio.
Mwanzoni WCB walikuwa na mgogoro na EATV lakini kwa sasa unazidi kuenea si Clouds media wala EFm kote awachezi nyimbo za Wcb.
Ata supporters wao wakubwa na wenye ushawishi kwenye mitandao especially tweeter na Instagram wamewapotezea.
Inawezekana yote haya yanatokea sababu watu wanaona kijicho na mafanikio ya Wasafi lakini pia haya yanaweza kutokea sababu mapungufu yaliyopo WCB.
Kwa sasa WCB ni kama ukoo kambale kila mtu ana ndevu.
Nimemskia juzi Tale anatamka hadharani kuwa awatanyenyekea media yoyote itayotaka kuwakwamisha akarudia hiyo kauli mara nne..ilo ni tatizo tayari, awajafika uko wanapodhani wamefika. Wanakuja na Tv yao lakini bado awajafika pale wanapodhani.
Mara nimesikia dansa wa Diamond kawatishia uhai watangazaji wa shilawadu mpaka kuwaumiza. Mpaka sasa uongozi wa wcb awajasema lolote kuonyesha kutounga mkono kitendo hicho.
Nimeona mpiga picha wao anamshambulia mkongwe wa muziki Ray C akimuita marehemu wa muziki.
Na mengine mengi, yote haya yanaonyesha kiburi cha mafanikio kimejaa pale WCB si viongozi mpaka wafagiaji wote nyota zinawaka mpaka wamejisahau wamevimba vichwa wameota mapembe.
Wamesahau msingi mkubwa wa mafanikio ya Diamond mpaka anafika hapo na kuifikisha hapo Wasafi ni UNYENYEKEVU.
Inawezekana kuna mambo wanakumbana nayo yanawalazimu kufikia hatua hii ila lazima waelewe biashara ya Entertainment ni biashara ya kibepari.
Naomba hii timu ijitafakari wakati wanauanza mwaka, kuna kitu hakipo sawa.
Mwl Nyerere alitunga kitabu kinaitwa Tujisahihishe, mkipata nafasi kitafuteni mkisome mtajifunza kitu kuhusu kujisahihisha... Kujisahihisha sio kujishusha.
Mtaenda Hyatt mtaenda Mwembeyanga but you still need media houses & media people.
Ni mtazamo tu, kiroho safi!